Ubora wa kazi hupimwa kwa kazi husika kupitia kwenye mlolongo ufuatao:
1: Kuweka lengo la kazi husika/matokeo.
2: Kutanabaisha ubora wa kazi husika itakapokuwa imekamilika, unataka iwe na vigezo vipi?
3: Kutanabaisha hatua mahsusi za utendaji kazi husika na wahusika (SOP).
4: Kutekeleza kazi husika kwa kufuata taratibu mahsusi zilizowekwa hatua kwa hatua.
5: Kupima matokeo/evaluation ya kazi dhidi ya vigezo vya ubora uliotarajiwa/ vilivyowekwa pale juu.
NB: Mzunguko huu huanza upya kwa kuzingatia matokeo yaliyopatikana kwa kuimarisha au kurekebisha baadhi ya hatua ndani ya utekelezaji.
Pia, kwa baadhi ya maeneo ya kazi kuna vitengo mahsusi vya kuweka ubora na kufatilia ubora wa kazi kila wakati.