Elections 2015 Ni vigumu sana kupata Rais mwenye sifa bora 2015

Kati ya watu wasiojielewa hapa nchini ni wewe...hiyo namba 8 ndio umedhihirisha umbumbumbu wako....urais siyo mali ya familia mkuu....la msingi wananchi ndio wamfahamu na kumkubali na sio JK kumfahamu
 
Kabila dogo ndio lina sifa gani, au tutumie vigezo gani kupima udogo na ukubwa wa kabila?
 
Tutaendelea kupeana nyepesi wakuu lakini mambo yanaonekana yako verry serious kuliko kawaida.Wenye nchi hawataki kufanya makosa.Mmmh,2015 noma!
 
Toa uchafu wako apa. Tunataka mtukuka na muadirifu ata kama atatoka kwenye kabila kubwa kama nyakyusa, sukuma,chaga au chaga. Hatutaki sikia ujinga wa nyinyiem wanaojipangia
 
Andiko lako limejaa ubaguzi, na kamwe watanzania hatuko tayari kuingia katika vita ya ukabila (rejea namba 2)....pili sio lazima rais JK amjue rais wa 2015 kumbuka urais sio taasisi ya kifamilia na ya kujuana, ile ni taasisi kwa ajili wa kutumikia wananchi..
 
CCM?ili iweje?Hivi Tanzania bila ccm haiwezekani siyo au tatizo ni vichwa vyetu mgando.Watanzania tunataka tufikie wapi/tuwe na hali gani ndiyo tuamini kuwa mchawi wa maendeleo yetu ni ccm.
 

Ni kweli anaitwa Jaka Mwambi anatoka Uruguruni kabila lisilokuwa na makuu,
 
Hii post nimeiona Tanuru la Fikra linashabikiwa na watu wa Membe...watanzania tukemee huu ubaguzi wa wazi kabisa eti kabila dogo! Jamani uchaguzi wa 2015 usituingize katika vita ya kikabila...rais mzuri ni yule mwenye kufanya maamuzi magumu katika kutumikia wananchi aijalishi ni kabila gani....awe mchaga or msukuma....
 
Mkuu Ana Maanisha JOKA LA MDIMU HUYU LA KULE MTAMA. SIJUI KAMA KABILA LAKE DOGO MIMI HATA SIJAMUELEWA
Hawwa vijana wa Membe wasichokijua ni kwamba wanamwaribia tu...kama kwenye hilo andiko limejaa ubaguzi mkubwa wa kikabila(civil wars nyingi Africa zimetokana na swala la ukabila,kwa kabila kubwa kuzarau kabila dogo, au kabila dogo lenye mamlaka kuzarau na kukandamiza kabila kubwa) sasa hawa watu wa Membe wanataka tuelekee huko, jamani before hamjapost muangalie madhara katika nchi..... Issue ya pili ni hiyo ya kujuana (namba 8) eti JK awe anamjua jamani inamana sisi wananchi tumefikia hatua ya kutoa ikulu kuwa sehemu ya kifamilia? Hapana we are not desparate kupata 2015 president kiasi hicho....
 
Toa uchafu wako apa. Tunataka mtukuka na muadirifu ata kama atatoka kwenye kabila kubwa kama nyakyusa, sukuma,chaga au chaga. Hatutaki sikia ujinga wa nyinyiem wanaojipangia

Wabaguzi kama hawa watu wa Membe tuwakemee na kuwaogopa kama ukoma.....itaingiza hii nchi kwenye machafuko makubwa sana....Nadhani hawatambui madhara ya ukabila ila mbona yapo wazi katika bara letu inamaana haoni au kapuuzia tu! Please and please watanzania tukemee watu kama hawa wa Membe wanaotugawa kwa ukabila (kubwa na dogo), na sijui kabila kubwa ni lipi na dogo ni lipi na katumia criteria gani?
 
Salaam wanajamvi!
Tukielekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwakani(2015), majina kadhaa yamekuwa yakitajwa kujaza nafasi itakayoachwa wazi na Rais Dr Kikwete.Nikiwatazama,waheshimiwa hawa, Sita, Membe, Lowasa, Wasira,
Nchimbi,Januari, Kigwangara,Pinda,Mwandosya, Sumaye, Migiro, Tiba n.k ukiwaacha wale wa upinzani, Wamekuwa sio kivutio kwa watu wengi wasioridhishwa na kasi ya maendeleo ya nchi, nidhamu ya viongozi, uwezo wa kiutendaji wa watumishi wakuu wa Umma na uvunaji wenye tija wa rasilimali za nchi.

Ukiacha vikundi vidogo vidogo vinavyowaunga mkono, watu walio wengi wanaona bado hakuna mwenye Haiba na Uwezo kwa nafasi hiyo.Watu wanalazimika kusema nafuu flani kuliko flani, hii inaonesha hakuna wanayeridhika naye bali wanalazimika kufanya chaguo pengine kwa kutokuona kama kuna Watanzania wengine wenye Haiba na uwezo kwa nafasi hiyo. Sina haja ya kufafanua udhaifu wa kila moja ila kwa ujumla sioni kiongozi hata mmoja mwenye kujiamini, mtendaji mzuri,mbunifu,mwenye maono, mwenye akili za kutosha(sina maana ya Elimu), mwenye uhodari wa kuongea anayeweza kujenga hoja akaeleweka na kuiletea heshima nchi yetu.

Ebu tusaidiane wanajamvi wenzangu kuibua na kufahamishana vichwa vya maaana(watu competent), walio ndani na nje wanaoweza kutusaidia, tuwashawishi wajitokeze kwa chama chotechote na tuwaunge mkono, tuachane na hao jamaa juu, ni wepesi muno bajamani.Sio lazima mtu awe amepata kuwa waziri au mbunge ndo kiwe kigezo cha kuwa rais!
 
Nchi yetu haina tatizo na nafasi ya Rais ina tatizo na mtenfaji mkuuu yaani Waziri Mkuuu... hivyo tupige kampeni waBunge wakati ukifika wasikubali waziri mkuu legelege.
 
Nchi yetu haina tatizo na nafasi ya Rais ina tatizo na mtenfaji mkuuu yaani Waziri Mkuuu... hivyo tupige kampeni waBunge wakati ukifika wasikubali waziri mkuu legelege.

Hilo nalo ni wazo zuri!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…