Ni vipi Mungu anahusika kuwaleta duniani watu wanaozaliwa na ulemavu unaofanya maisha yao kuwa Jehanamu, Ni baraka yake kuwa hivyo ?

Ni vipi Mungu anahusika kuwaleta duniani watu wanaozaliwa na ulemavu unaofanya maisha yao kuwa Jehanamu, Ni baraka yake kuwa hivyo ?

Mtu akizaliwa na afya iwe ana ujinga ama maskini huyu anaweza kujielimisha kuondoa ujinga na kutumia nguvu ama bidii yake kujondokana na umaskini ila kwa walemavu hali huwa ni tofauti sana ?

Nashangaa sana hii ishu na ninaomba nifafanuliwe, Mungu anahusikaje na je ni baraka kuzaliwa hivi kwa mtu / mnyama ambae anaingia duniani bila hata dhambi ?

Walemavu ni wengi sana ila ni vile kwasababu inakuwa ngumu kwao kutoka ndio maana hata tunaowaona ni wachache,

Nayaongea haya kwa uhalisia na wala si kiburi cha uzima, watu hawa wanateseka sana hapa duniani, Wenye hali hizi waliofanikiwa kiuchumi wapo ila ni wa kuhesabika na jihudi walizotumia laiti wangekuwa wazima basi wangefanikiwa mara 10 zaidi.

Mtu anazaliwa haoni, yani hata kusoma Biblia / Koran hawezi

Mtu anazaliwa hasikii, hata kwenda kanisani / Msikitini haambulii kitu

Mtua nazaliwa na ulemavu wa akili, ni changamoto

Mtu anazaliwa haoni wala hasikii, hapa hawezi kujifunza chochote maana njia zote za kupokea ujumbe zimezibwa

Mtu kazaliwa na magonjwa yenye maumivu makali / maisha yake ni maumivu tu
Kijana mambo ya Mungu mwachie Mungu mwenyewe, maana hakuna mtu atakaekupa jibu lenye uhalisia wa kile unachojiuliza.

Mambo ya Mungu ni mambo ambayo yapo nje ya uwezo wa binadamu kuyafahamu.

So wewe kama umezaliwa bila ulemavu wa kuonekana basi mshukuru Mungu na ujibidiishe kutafuta ugali wako kupitia pumzi yake aliokupa bure.

Kuandika thread ya aina hii humu ni njia moja wapo ya kutaka kuwafanya walemavu waliopo humu hasa wale wasiokuwa na imani thabiti waanze kumchukia Mungu wao kwa kuona kuwa walionewa katika uumbaji.
 
MUNGU haumbi kiumbe mwenye ulemavu ,shetani uanza kuwagusa viumbe Toka katoka tumbo za mama zao ili kuharibu nyota zao
 
Mungu Anatuonesha utukufu wake kk viumbe wake ya KwaMBA yeye ndiye mkamilifu,na wewe unae jiona mkamilifu angeweza kukuumba ukawa mlemavu na mlemavu akawa mzima.
Hivyo ukamilifu ni wake Mungu pekee.
Ingependeza uwe unasoma post nzima neno kwa neno kabla hujakurupuka kukimbilia kukomenti
 
MUNGU haumbi kiumbe mwenye ulemavu ,shetani uanza kuwagusa viumbe Toka katoka tumbo za mama zao ili kuharibu nyota zao
Huyo Mungu muweza wa vyote na mwenye upendo wa kweli ana achaje huyo shetani aguse kiumbe chake anacho kiumba???

Kwamba, Wakati shetani anaharibu nyota za watu huyo Mungu haoni na hajui????
 
Ingependeza uwe unasoma post nzima neno kwa neno kabla hujakurupuka kukimbilia kukomenti
Kwani kusoma uelewe kilichoandikwa yapasa iwe mara ngapi mkuu maana naona kama unanifokea wakati huo ni mtazamo wangu.
 
Kwani kusoma uelewe kilichoandikwa yapasa iwe mara ngapi mkuu maana naona kama unanifokea wakati huo ni mtazamo wangu.
kuna sehem nimeandika "Nayaongea haya kwa uhalisia na wala si kiburi cha uzima"

Wewe umekurupuka kuandika nimejiona mkamilifu ni ushahidi tosha hukusoma post nzima ama ulisoma haraka haraka bila kuelewa
 
Mungu Anatuonesha utukufu wake kk viumbe wake ya KwaMBA yeye ndiye mkamilifu,na wewe unae jiona mkamilifu angeweza kukuumba ukawa mlemavu na mlemavu akawa mzima.
Hivyo ukamilifu ni wake Mungu pekee.
Huyo Mungu anapata faida gani akipewa utukufu?

Anapata faida gani kuumba binadamu mwenye ulemavu??

Kwani yeye Mungu Hajijui kwamba ni mkamilifu hadi sisi wanadamu tumwite mkamilifu???
 
Kila kitu ni utukufu wa Mungu...wameumbwa jinsi walivyo ili kazi zake zi dhihirishwe miongoni mwetu.....si unaona umepata wasaa
wa kumtafakari uweza wake
Kwamba ilikuwa ni lazima kazi zake zidhihirike kupitia hao walemavu? Yaani walemavu na wale wote wenye madhila kama hayo ndiyo watolewe kafara/wabebe gharama za kudhihirisha hizo kazi kwa watu wengine?
 
Kijana mambo ya Mungu mwachie Mungu mwenyewe, maana hakuna mtu atakaekupa jibu lenye uhalisia wa kile unachojiuliza.

Mambo ya Mungu ni mambo ambayo yapo nje ya uwezo wa binadamu kuyafahamu.

So wewe kama umezaliwa bila ulemavu wa kuonekana basi mshukuru Mungu na ujibidiishe kutafuta ugali wako kupitia pumzi yake aliokupa bure.

Kuandika thread ya aina hii humu ni njia moja wapo ya kutaka kuwafanya walemavu waliopo humu hasa wale wasiokuwa na imani thabiti waanze kumchukia Mungu wao kwa kuona kuwa walionewa katika uumbaji.
Huyo aliyesema mambo ya Mungu yapo nje ya uwezo wa mwanadamu, Alifahamu vipi kwamba huyo Mungu yupo?

Na alifahamu vipi kwamba mambo ya huyo Mungu yapo nje ya uwezo wetu wanadamu???
 
kuna sehem nimeandika "Nayaongea haya kwa uhalisia na wala si kiburi cha uzima"

Wewe umekurupuka kuandika nimejiona mkamilifu ni ushahidi tosha hukusoma post nzima ama ulisoma haraka haraka bila kuelewa
Hebu rejea post zangu utakuwa umenielewa vibaya.
Hakuna mahala nimeandika unachonishutumu nacho
 
Huyo Mungu anapata faida gani akipewa utukufu?

Anapata faida gani kuumba binadamu mwenye ulemavu??

Kwani yeye Mungu Hajijui kwamba ni mkamilifu hadi sisi wanadamu tumwite mkamilifu???
Mungu huyo huyo ambaye unaonahafanyi haki ana uwezo wa kuondoa species zote zilizopo duniani na akaleta species nyingine kabisa ambavyo wala hata hazifikiriki.
Huo ndio ukuu wa mungu.
 
Upo sahihi !!yote hayo ni kwamba tunakuwa wazina wa afya na viungo kwa neema zake kuna wengine hawapo hivyo..

Kila kitu kushukuru kwani hata mimi ningekuwa kipofu ila kwa neema zake tu nipo mzima...Bado tunaishi ila safari ni ndefu life is uncertainty sijui kesho yangu ndo maana wahenga wanasema "Hujafa hujaumbika " Mungu ndo muweza wa yote
 
Wanasema kila kitu ni utukufu wa Mungu, watu wote wanaozaliwa wameumbwa kwa baraka yake,
Mungu hakuwaumba wanadamu wakiwa na ulemavu. Ulemavu ni matokeo ya dhambi ya Adamu na Hawa walipomkataa Mungu

Waroma 5:12 BHN​

12. Kwa njia ya mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, nayo ikasababisha kifo. Hivyo kifo kimeenea katika jumuiya yote ya binadamu, kwa maana wote wametenda dhambi.

Mungu anatutakia mema sikuzote

Isaya 35:5Biblia Habari Njema (BHN)​

Hapo vipofu wataona tena,na viziwi watasikia tena

Ufunuo 21:3-4 BHN​

3. Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka katika kiti cha enzi ikisema, “Tazama! Maskani ya Mungu kati ya watu. Atakaa kati yao, nao watakuwa watu wake, naye atakuwa Mungu wao.

4. Yeye atayafuta machozi yao yote; maana kifo hakitakuwako tena, wala uchungu, wala kilio, wala maumivu; maana ile hali ya kale imepita!”
 
Mungu huyo huyo ambaye unaonahafanyi haki ana uwezo wa kuondoa species zote zilizopo duniani na akaleta species nyingine kabisa ambavyo wala hata hazifikiriki.
Huo ndio ukuu wa mungu.
Alishindwaje kuumba hizo species zenye kumtii yeye tu na zenye kufanya mema tu,

Badala yake Kaumba species zenye kufanya mema na maovu kwa wakati mmoja na yeye hutaka mema tu?????

Anaweza yote kweli huyo Mungu???
 
Hakuna kitu katiri duniani Kama mungu, chunguza maisha ya wanyama mbugani utaniambia,

Hakuna kitu yenye roho mbaya duniani Kama mungu,muulize farao,waulize sodoma kawaulize gomora,waulize wenyeji wa kanaani,walicho fanywa na waisral

Hakuna kitu chenye wivu duniani Kama mungu kawaulize waizrael wakiwa jangwani baada ya kujifanyia ng'ombe wa shaba na kumwabudu mungu aliwa fanya Nini?

Mungu alimpiga ugumba Sara akaja kumpa mtoto akiwa na miaka 90

Mungu alimpiga upofu zakayo ili yesu mwanae aje achukue maujiko

Mungu alimuumba adamu akiwa mkamilifu aliishi vema na kufuata Sheria zake lakini akaona sio poa akamletea Eva ili amwangushe na Adam akapewa rb ya maisha

Mungu aliuwa watu wote sodoma na gomora. Kisha akamwacha yule mzee luthu na mabinti zake wawili tu

sjui ili iweje? Yani baba na mabinti na hakuna mwanaume mwingine mabinti wakala chakula Cha mama yao AF ni dhambi binti kutembea na mzazi mpaka leo

Lakini mungu ni mwenye upendo

Mungu ni mwenye rehema

Mungu ni nuru yetu na tuifwate🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom