Ni vizuri kumwambia mkeo kiwacho Cha pesa unacholipwa kazini?

Ni vizuri kumwambia mkeo kiwacho Cha pesa unacholipwa kazini?

1. Tulisema USIOE.
2. We umeoa.
3. Tukasema Usimwambie we Mfanyakazi wala Mfanyabiashara.
4. We umemwambia.
5.Tukasema usimwambie Kipato chako, akiuliza sana toa sifuli mbili kwenye kipato chako.
6. We unataka umwambie.
7. Mawili yatatokea. Either utaachwa?
8. Au tuambie kabisa mwili wako tukazike wapi?
 
Pesa inabaki salama na ni njia rahisi na nzr ya kujenga uchumi na maendeleo katika familia,... Matumizi sahihi na yenye tija lazima yawe na msimamizi mkaguzi wa mahesabu, atayeweza kukuhoji namna ya matumizi yako sahihi uliyoyafanya. Kumwambia kiasi unachopata si kumkabidhi awe nacho, lah!.. Ukiwa nacho kwa siri kinakupa room ya kukifanyia matumizi ya hovyo, kama kuhonga, kunywea kupita kiasi nk. NI SAHIHI NA VEMA KUMWAMBIA kwa nia njema ya kujenga uchumi na maendeleo ya familia, mimi imenisaidia saaana!
 
Huko kwenye ndoa stress hua mnazitafuta wenyewe, kias unacholipwa anaestahili kujua ni aliekusomesha tu
😂😂 na kuna ambao hata hao waliowasomesha hawajui watoto zao wanalipwaje.
 
Kama ni mwajiriwa hata usipomuambia si atajua tu!
 
We mwambie tu ukikuta taarifa zimezagaa mtaaa mzima usije kufungua Uzi mwingine hapa
 
Ni sawa umuambie Kwa sababu asije akawa na expectations kubwa kumbe unalipwa laki 7.
Ukimwambia mshahara ishini within the salary.Mimi mama yenu anajua mshahara wangu,anajua pin ya ATM card me mwenyewe siijui.
changamoto ni hapo ukitaka Hela ya kuhonga huna ujajanja mpaka ukamuone Mkeo.
Kitu kizuri kuhonga huwezi kuhonga maana pesa zinajulikana na Mkeo.
Nawaambia ngono inamaliza zana pesa.Lodge 30k tena ya kawaida binti atataka kusuka 30k msuko wa kawaida,vinywaji kama anakunywa savanna 5 ni 25k,chakula 15k,mkimaliza mpe nauli 50k .
Angalia hiyo garama yoote ya Nini?kama muhasibu ni mke je unazitoaje kutoka Kwa danga kwenda kwake?
Naomba mtafakari vizur na muwe na akili.
 
Ni vizuri kumwambia mkeo kiwacho Cha pesa unacholipwa kazini?
Kama yeye amekwambia kiasi anacholipwa yeye, basi si vibaya na wewe kumwambia. Ila kama hajakwambia......sijui itakuwa unawashwa na nini mpaka umwambie.
 
Haina haja ya kumuambia
Kwani bajeti ya kila mwezi ni wewe unaepanga na unajua zinaenda wapi

Ukimwambia iko siku atakuuliza mbona umepunguza matumizi?
Wakati wewe umefanyia mengine
 
Ni sawa umuambie Kwa sababu asije akawa na expectations kubwa kumbe unalipwa laki 7.
Ukimwambia mshahara ishini within the salary.Mimi mama yenu anajua mshahara wangu,anajua pin ya ATM card me mwenyewe siijui.
changamoto ni hapo ukitaka Hela ya kuhonga huna ujajanja mpaka ukamuone Mkeo.
Kitu kizuri kuhonga huwezi kuhonga maana pesa zinajulikana na Mkeo.
Nawaambia ngono inamaliza zana pesa.Lodge 30k tena ya kawaida binti atataka kusuka 30k msuko wa kawaida,vinywaji kama anakunywa savanna 5 ni 25k,chakula 15k,mkimaliza mpe nauli 50k .
Angalia hiyo garama yoote ya Nini?kama muhasibu ni mke je unazitoaje kutoka Kwa danga kwenda kwake?
Naomba mtafakari vizur na muwe na akili.
Maana yake hapo kama unamla mara 2 (X 2) kwa mwezi - utenge bajeti ya Tshs. 300,000.
 
Back
Top Bottom