Inaonesha una tatizo la kupoteza kumbukumbu.
Nakukumbusha, usisahau tena. CAG Musa Assad aliulizwa na Marehemu Magufuli, "CAG kuna hela 1.5 trilioni imeibiwa?". Musa Assad akasema, hapana.
CAG huwa hatoi taarifa kuwa kuna pesa kiasi fulani imeibiwa bali hueleza pesa iliyokusanywa au kupelekwa mahali, lakini pesa hiyo ama haikuonekana imetumika wapi, ama haipo mahali popote, ama imetumika bila kufuata utaratibu. Jeshi la Polisi na TAKUKURU, wao ndio wana wajibu wa kutamka kuwa pesa hiyo imeibiwa, na imeibiwa na nani.
Kwa hiyo marehemu aliuliza swali ambalo alikuwa anajua jibu lake litakuwa hapana. Kwa sababu si kazi ya CAG kusema pesa imeibiwa.
Taarifa ya CAG ilisema kuna pesa 1.5 trilioni ambayo ilikusanywa lakini haipo benki na haionekani kwenye matumizi. Rais alitakiwa kumwuliza CAG, "je, kuna pesa 1.5 trilioni haijulikani ilikoenda". Hapo tuna uhakika jibu la CAG lingekuwa ni ndiyo.