Chozizwa2020
JF-Expert Member
- Apr 8, 2021
- 912
- 853
Mkuu, ulikuwa huwajui? Hao wanafisadi hadi mali zao. Ziko wapi zile shule za secondary za Wazazi na ile miradi mikubwa mikubwa, sasa kweli watashindwa hizi mali za Watanganyika.Tangu mwaka 1977 CCM iko madarakani na wakati wote huo mpaka sasa ufisadi na mafisadi ndiyo mtindo wa kuendesha nchi kutoka CCM. Kama kuna mtu anaweza kutuambia kwa uhakika ni wakati gani kulikuwa hakuna Ufisadi na mafisadi ndani ya CCM, atuambie tujue!!
UFISADI NI SERA YA CCM IPO NA ITAENDELEA KUWEPO CCM NA UFISADI INAWEZEKANATangu mwaka 1977 CCM iko madarakani na wakati wote huo mpaka sasa ufisadi na mafisadi ndiyo mtindo wa kuendesha nchi kutoka CCM. Kama kuna mtu anaweza kutuambia kwa uhakika ni wakati gani kulikuwa hakuna Ufisadi na mafisadi ndani ya CCM, atuambie tujue!!
Hahaaaaa!!kuficha ripoti Za CAG ndio unasema hakukuwa na ufisadi,zile pesa alizopiga Kigwangala ilikuwa ni awamu ipi?na kwa taarifa yako hakuna awamu pesa zimepigwa kama awamu ya tano.Awamu wa tano hakukuwa na watu wa namna hiyo kiasi cha kujitokeza hadharani kulikuwa na nidhamu kubwa sana kwa mali za umma sasa hivi watu waomoa maana sio kuiba
Awamu ile kulikua na kikundi kidogo cha kifisadi, waliondoa lile genge kubwa la chukua chako mapema!! Wakaona ili twende saw na slogan ya uzalendo ni kuua genge kubwa la kifisadi na kutengeneza circle ndogo ya kifisadi!!Awamu wa tano hakukuwa na watu wa namna hiyo kiasi cha kujitokeza hadharani kulikuwa na nidhamu kubwa sana kwa mali za umma sasa hivi watu waomoa maana sio kuiba
Hakuna!Tangu mwaka 1977 CCM iko madarakani na wakati wote huo mpaka sasa ufisadi na mafisadi ndiyo mtindo wa kuendesha nchi kutoka CCM. Kama kuna mtu anaweza kutuambia kwa uhakika ni wakati gani kulikuwa hakuna Ufisadi na mafisadi ndani ya CCM, atuambie tujue!!
Unaota. Au ulikuwa hujazaliwa?Awamu ya 2
Inaonesha una tatizo la kupoteza kumbukumbu.Kwa sababu alikuwa mpumbavu, wewe mtu umeulizwa, ni kweli kuna upotevu wa 1.5 t? Unakataa, sasa hiyo ni nini kama siyo ujuha?
Ufisadi ulianza baada ya Mwalimu kuachia ngazi 1985 . Enzi za Mwalimu labda udokozi kidogo ulikuwepo !!Tangu mwaka 1977 CCM iko madarakani na wakati wote huo mpaka sasa ufisadi na mafisadi ndiyo mtindo wa kuendesha nchi kutoka CCM. Kama kuna mtu anaweza kutuambia kwa uhakika ni wakati gani kulikuwa hakuna Ufisadi na mafisadi ndani ya CCM, atuambie tujue!!
Acha uongo Nchambi alikutwa na kesi ya mabilioni ila aliachiwa kwa faini ya 10% ya alichoiba. Hata Mwanyika alikuwa na kesi ya kutuletea hasara ya matrillion ila aliachiwa kwa kulipa billion 2 pekee. Hapo Bado Kuna mafisadi waliotajwa kwenye ripoti ya Bashiru sikuona JPM akichukua hatua mpaka anafariki. Bado NIDA Ufisadi wa kutisha watu tokea 2016 hatuna ID huyo JPM alifanya Nini?? Kingine ufisadi wa mabilioni ya electronic passports kwani JPM hakuwepo?Awamu wa tano hakukuwa na watu wa namna hiyo kiasi cha kujitokeza hadharani kulikuwa na nidhamu kubwa sana kwa mali za umma sasa hivi watu waomoa maana sio kuiba
Mkuu una busara sana, kama ingalikuwa ni uwezo wangu huyo "KIMA" aliyemuita Prof. Assad ningemtandika hata makofi. Kwanza haelewi ethics za taaluma ya kihasibu zaidi kukurupuka tu akidhani yule ni Prof. wa mchongo kama yule mama wa "Suluhisho" aliyepewa PhD ya mchongo.Inaonesha una tatizo la kupoteza kumbukumbu.
Nakukumbusha, usisahau tena. CAG Musa Assad aliulizwa na Marehemu Magufuli, "CAG kuna hela 1.5 trilioni imeibiwa?". Musa Assad akasema, hapana.
CAG huwa hatoi taarifa kuwa kuna pesa kiasi fulani imeibiwa bali hueleza pesa iliyokusanywa au kupelekwa mahali, lakini pesa hiyo ama haikuonekana imetumika wapi, ama haipo mahali popote, ama imetumika bila kufuata utaratibu. Jeshi la Polisi na TAKUKURU, wao ndio wana wajibu wa kutamka kuwa pesa hiyo imeibiwa, na imeibiwa na nani.
Kwa hiyo marehemu aliuliza swali ambalo alikuwa anajua jibu lake litakuwa hapana. Kwa sababu si kazi ya CAG kusema pesa imeibiwa.
Taarifa ya CAG ilisema kuna pesa 1.5 trilioni ambayo ilikusanywa lakini haipo benki na haionekani kwenye matumizi. Rais alitakiwa kumwuliza CAG, "je, kuna pesa 1.5 trilioni haijulikani ilikoenda". Hapo tuna uhakika jibu la CAG lingekuwa ni ndiyo.
Lini CAG aliwahi sema Kuna upotevu wa 1.5 Trillion. Alichosema ni kwamba pesa ilikusanywa hiyo 1.5 ila haikupita mfuko mkuu wa serikali yaani Hazina. So unaweza kusanya pesa ukazitunza kwingine Sasa maadam sio mfuko mkuu wa serikali ni ngumu kujua ilitumikaje au kama kweli iliofanya shughuli iliyokusudiwa ni audit query. Sasa Jiwe akauliza eti CAG Kuna ufisadi wa trillion 1.5? Obvious Jibu ni NO. ila angeuliza je unajua ilipo trillioni 1.5 obvious angejibu Haijulikani.Kwa sababu alikuwa mpumbavu, wewe mtu umeulizwa, ni kweli kuna upotevu wa 1.5 t? Unakataa, sasa hiyo ni nini kama siyo ujuha?
Mantiki kubwa sana hii!!Sasa Jiwe akauliza eti CAG Kuna ufisadi wa trillion 1.5? Obvious Jibu ni NO. ila angeuliza je unajua ilipo trillioni 1.5 obvious angejibu Haijulikani.
Serikali ni kama gari, anayeendesha (Chama cha siasa) ndiyo huamua gari lielekee wapi. Maamuzi yanayofanywa na CCM ndiyo hutekelezwa na watendaji wa serikali. Pia watendaji wa Serikali hawaruhusiwi kuwa wanachama wa chama cha siasa ingawa kwa wizi, CCM huvumilia watendaji hao wa serikali kuwa wanachama wao!!Kwani watendaji wote serikalini ni wanaccm?