Ni wakati muafaka BoT kuchapisha Noti zenye picha na sura ya Rais Samia kuweka historia kwa vizazi na vizazi

Ni wakati muafaka BoT kuchapisha Noti zenye picha na sura ya Rais Samia kuweka historia kwa vizazi na vizazi

Ndugu zangu Watanzania,

Kwa kila jambo na wakati wake na majira yake kwa sababu maalumu.huu ni wakati na muda muafaka kabisa kuchapisha noti zitakazokuwa na picha na sura ya Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Hii ni katika kuweka historia itakayo dumu na kukumbukwa vizazi na vizazi na kuwa Sehemu ya historia ya Taifa letu. Rais Samia kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu Mwenyewe ameweka historia ya kipekee kabisa kwa kuwa Mwanamke wa Kwanza kushika nafasi ya Urais hapa Nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Rais Samia ni Mwanamke na Mama aliyelivusha Taifa katika wakati mgumu sana katika Historia ya Taifa letu.ikumbukwe kuwa ameshika Nchi katika kipindi ambacho Uchumi wa Dunia ulikuwa umetikisika kuwahi kushuhudiwa katika Historia ya Dunia ukiachana na ule uliotokea miaka ya 1930-1945 ambao ulisababishwa na mambo mbalimbali kama tunavyojifunza katika Historia.

Rais Samia amepokea nchi wakati Dunia ikishuhudia viwanda vingi vikiwa vimesimamisha uzalishaji ,ukosefu mkubwa wa ajira,mdororo wa kiuchumi kutokana na kupungua kwa shughuli za kiuchumi na uzalishaji,kupanda au mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa muhimu kama vile mafuta ya petroli na dizeli ambavyo ni injini ya uchumi,kupanda kwa bei ya Mbolea,mzunguko mdogo wa pesa mitaani na mengine mengi sana.

Ambavyo hivyo vyote vilichochewa na ugonjwa wa COVID-19 pamoja na vita vya ukrein.lakini kwa umadhubuti,uhodari, uimara ,ushupavu ,akili kubwa , maono makubwa na Uweza wa mwenyezi Mungu tulishuhudia Mama huyu shupavu na madhubuti akilivusha Taifa kwa kuchukua hatua mbalimbali. kama vile kutoa Ruzuku ya Billion mia moja kila mwezi katika nishati ya mafuta,kutoa Ruzuku ya Billion mia mbili hamsini katika mbolea hali iliyoshuhudia bidhaa hizo zikishuka bei.

Ndio Maana tuliona na kushuhudia wakenya wakivuka mpaka na kuingia Tanzania kununua mafuta kutokana na bei kuwa ndogo Nchini ukilinganisha na Nchini kwao.hali ya kiuchumi Nchini ilikuwa nzuri ukilinganisha na nchi yoyote ile hapa barani Afrika.lakini wakati akifanya haya Dunia ilishuhudia Mama huyu aliyeinuliwa na kupewa kibali na Mungu akitoa maelfu ya ajira kwa vijana,kujenga miundombinu,kusogeza huduma karibu ya wananchi,kuongeza bajeti katika kila wizara kama ambavyo tuliona katika kilimo kuongeza bajeti kutoka Billion 250 hadi Billion 970.

Tuliona akifanya juhudi kubwa ya kufungua nchi yetu ikiwa ni pamoja na kuvutia wawekezaji pamoja na watalii kupitia royal tour iliyopelekea ongezeko la watalii kufikia Millioni 1.8 kwa mwaka.tuliona bei ya mazao Kama vile korosho ikipaa bei tena hasa baada ya kufanya ziara rasmi Nchini India na kukutana na makampuni na wafanyabiashara wa korosho.

Hayo na mengine mengi sana yalifanya Taifa na nchi yetu kusalia imara na yenye utulivu wa hali ya juu katikati ya hali mbaya ya kiuchumi iliyoikumba Dunia nzima.lakini sisi tukawa katika kisiwa chetu cha utulivu na ustahimilivu wa kiuchumi chini ya Jasusi wa uchumi Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Najuwa wenye upeo mdogo wataanza kujadili habari za gharama za kuchapisha pesa hizo,na wengine watasema siyo mahitaji ya watanzania.lakini niwaambieni tu kuwa faida aliyoliletea Taifa letu ni kubwa sana.asingetumia akili tungekuwa tumesambaratika kama Taifa.hali ya umaskini na uchumi ingekuwa mbaya sana hapa nchini.na tusingeona kuendelea kwa miradi mikubwa kama Bwawa la Mwalimu Nyerere lenye kutupatia megawati 2115 wala kuzinduliwa kwa reli ya SGR na usafiri huo wa treni ya umeme.

Tumpeni heshima yake huyu Mama ,tuache wivu na chuki binafsi,tuache ubaguzi kwa misingi ya Udini,ukabila,ukanda na jinsia .Mama yetu anastahili kupewa heshima hiyo ya kuchapisha noti zenye sura na picha yake.View attachment 3136898

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 

Attachments

  • IMG_2941.jpeg
    IMG_2941.jpeg
    42.5 KB · Views: 3
  • IMG_2939.jpeg
    IMG_2939.jpeg
    14.2 KB · Views: 2
  • IMG_8869.jpeg
    IMG_8869.jpeg
    53.9 KB · Views: 3
Hapana, nakupinga kwa hoja, acha ujinga, Marais wote waliopita kuanzia Mkapa, Kikwete, Magufuli, wote hawakuweka sura zao katika noti, na sio hawakufanya kazi kubwa, acha kujitungia mambo yako hata Mh. Rais akisoma habari hizi anachukia

Wewe unakaa kwenye keyboard, mawazo yako yasiyo na mantiki unapost post tu, achana na hayo mawazo potofu
Hakuna hoja yoyote ile uliyoandika.umeelewa msingi wa hoja yangu au umekurupuka zako tu kutoka usingizini?
 
Soma andiko ndio utaelewa vizuri na hiyo akili yako ndogo.unafahau Ureno ipo kwenye mpango wa kutoa shilingi itakayo kuwa na picha ya Christiano Ronaldo katika kutambua mchango wake kwa Taifa lake?
Huo ndio unaitwa upumbavu. Yaani ukiwa mjinga unaweza kuelimika.
Kama ureno wanataka kufanya hivyo ndio muige huko?
Kwa nini musiige maendeleo yanayofanwa na mataifa mengine munaiga upuuzi?

Haya tuambie Rais yupi hajaonyesha mchango wake katika hii nchi?

Ficha upumbavu wako hata kidogo.
 
Huo ndio unaitwa upumbavu. Yaani ukiwa mjinga unaweza kuelimika.
Kama ureno wanataka kufanya hivyo ndio muige huko?
Kwa nini musiige maendeleo yanayofanwa na mataifa mengine munaiga upuuzi?

Haya tuambie Rais yupi hajaonyesha mchango wake katika hii nchi?

Ficha upumbavu wako hata kidogo.
Nimegundua huna akili kabisa wewe.hoja yangu ipo wazi kabisa sababu za kutaka kufanyika jambo hilo.
 
Nimeelezea mengi zaidi ya maendeleo.ndiye mwanamke wa kwanza kushika Urais hapa Nchini.niambie ni Mwanamke yupi mwingine aliyeshika Urais hapa Nchini zaidi ya Rais Samia?
Na unafahamu kuwa sio mwanamke wa kwanza kuwa Rais Duniani?
Wenye akili hilo haliwashangazi kabisa.
Wanaelewa kuwa mwanamke anauwezo wa kushika nafasi yoyote kama mwanaume.
 
Back
Top Bottom