Ni wakati muafaka sasa nchi ikaendeshwa kwa majimbo

Joined
Sep 17, 2014
Posts
67
Reaction score
24
Ili kusonga mbele kama Taifa na kuleta maendeleo sawa kwa watu tubuni Majimbo since our Country is large tuingie kwenye mfumo huu. Na iwe hivi:

1. Mwanza, Kagera, Geita yawe BUKOBA STATE

2. Shinyanga, Tabora na Katavi yaitwe TABORA STATE.

3Dodoma, Singida na Morogoro yaitwe DODOMA DC STATE.

4. Dar, Pwani na Tanga yaitwe DAR ES SALAAM STATE.

5. Lindi, Mtwara na Ruvuma yaitwe COASTAL STATE.

6. Arusha, Manyara na Kilimanjaro yaitwe KIRIMANJARO STATE.

7. Kigoma na Rukwa yaitwe WEST STATE.

8. Mbeya, Iringa na Songwe yaitwe GREEN STATE,

9. UNGUJA STATE

10. PEMBA STATE.

Mimi naona hivyo, unaweza kuborasha ili kuweka usawa wa rasmali kwa STATES au COUNTIES zote.


 
Hapo Utaleta Usawa Wa Mgawanyo Wa Rasmali Ingawaje Kuna Watu Hawataelewa Maana Yake
 
Umetumia vigezo vipi? usitupotezee muda. Eleza kitu kinachoeleweka. What? Why? How?



 
Naona sasa Chadema mnataka kuigawa nchi, Kwa hiyo kila COUNTY itakuwa na rais wake?
 
..... Siungi Mkono Majina Kama Bukoba State, Knjaro Na Mengne Yanayowakilisha Jina La Mkoa.
 

Ccm hawataki kuona kitu kama hicho
 
Mfumo uliopo sasa ni mzuri sana kwani unawezesha maeneo madogo madogo kama mikoa kufanya kazi kama state badala ya kuwa na maeneo makubwa ambayo yataleta utendajiji hafifu.

Ndio maana tunaanzisha mikoa na wilaya mpya ili kusogeza huduma na kuondoa urasimu
 

Serikali za majimbo ni mfumo ufaao kwa wale walioshindwa kuunda taifa moja hasa baada ya kutoka vitani.Marekani walipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe hadi basi.Wakaona waweke mfumo wa majimbo ambao kila bwana la vita litakuwa na jimbo lake halafu wawe na serikali ya shirikisho tu.Ndio kisa cha marekani kuwa na serikali za majimbo.Marekani ni nchi nyingi ndani ya nchi.Hizi nchi ndogo ndogo zinaitwa majimbo.

Urusi nao walipoanza kutwangana wakaona hawawezani wakaanzisha serikali za majimbo na kuwa na serikali ya umoja ile ya putin.

Afrika kusini nao walitwangana weee baadaye wakakubali yaishe nao wana serikali za majimbo.


Kenya pia baada ya vita za kikabila ilibidi waunde serikali za majimbo zenye magavana n.k ili kugawana madaraka kwa kila bwana la vita la kikabila.Wameshindwa kuunda Kenya moja.

Tanzania tuliweza kufanya nchi moja toka mwanzo hivyo majimbo yakamezwa sababu kila waanzisha serikali walitaka wote nchi moja tu.

Tatizo wengi ni watu wa ku-copy vitu bila kusoma historia ya kwa nini kulikuwepo majimbo? Mtu akienda USA akatembelea kule akapewa pizza na kuongeleshwa kingereza kidogo akirudi nchini anakuwa bila kutafakari utasikia sera ya chama chetu ni majimbo nimeona USA!!!!!

Nchi kama somalia na sudan kusini mojawapo ya namna ya kutatua matatizo yao ya kisiasa ni kuunda serikali ya majimbo ambayo kila jogoo la vita linapewa eneo linakokubalika halafu kunakuwa na serikali ya shirikisho.
Kuunda serikali ya majimbo kwa nchi kama tanzania ni kuisambaratisha nchi na kurudi kule kwenye ukabila na umaeneo.
 

Na kwanini isiwe Jimbo la Bukoba badala Bukoba State? yaani kwanini tutumie neno State na SIYO Jimbo?
 
Ulichoandika kina akisi msimamo wa January Makamba kuhusu sera ya majimbo
 
We mjinga sana, kenya wana marais wangapi? Haupo mfumo huu huko kenya? USA kuna marais wangapi...hivi vipropaganda vyenu vya kip umbafu huwa vinawasaidia nini, mshe nzi kabisa wewe

Naona sasa Chadema mnataka kuigawa nchi, Kwa hiyo kila COUNTY itakuwa na rais wake?
 
Kuwepo kwa mfumo wowote wa kiutawala ukiwemo wa majimbo lazima kuendane na mambo ya msingi kwa maslahi ya taifa: ULINZI NA USALAMA, UTAWALA WA SHERIA, UMOJA, USIMAMIZI NA MGAWANYO WA RASLILMALI, HUDUMA ZA MSINGI, NA UENDELEZAJI UCHUMI WA TAIFA kwa faida ya wananchi wote. Sijui kama Tz tumeimarika kiasi cha kuchukua mfumo wa utawala kama huu.
 

Nakubaliana nawewe kuhusu majimbo lakini sikubaliani na wewe kuhusu majina ya majimbo. Mtazamo wangu ni

Jimbo la Kaskazini, Arusha, Manyara, Kilimanjaro.
Jimbo la Pwani: Dar, Pwani, Tanga.
Jimbo la kati: Dodoma, Singida Morogoro
Jimbo la kanda ya ziwa: Mwanza, Kagera, Geita, Mara,shinyanga
Jimbo la kusini: Lindi, Mtwara, Ruvuma
Jimbo la magharibi: Kigoma, Rukwa,tabora
Jimbo la nyanda za juu: Mbeya, Iringa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…