East African Eagle
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 3,759
- 2,211
Nakubaliana nawewe kuhusu majimbo lakini sikubaliani na wewe kuhusu majina ya majimbo. Mtazamo wangu ni
Jimbo la Kaskazini, Arusha, Manyara, Kilimanjaro.
Jimbo la Pwani: Dar, Pwani, Tanga.
Jimbo la kati: Dodoma, Singida Morogoro
Jimbo la kanda ya ziwa: Mwanza, Kagera, Geita, Mara,shinyanga
Jimbo la kusini: Lindi, Mtwara, Ruvuma
Jimbo la magharibi: Kigoma, Rukwa,tabora
Jimbo la nyanda za juu: Mbeya, Iringa
Naona sasa Chadema mnataka kuigawa nchi, Kwa hiyo kila COUNTY itakuwa na rais wake?
1. _umeisahau mikoa mipya ,
2. _majina uliopendekeza kwa majimbo hayo yataleta mgogoro umetumia vigezo gana kupendekeza
3 naunga mkono hoja but marekebisho ni muhimukwani baadhi ya majimbo yatakuwa nyuma kimaendeleo kwa sababu ya uhaba wa rasilimali
Wazo zuri sana japo nimeona mitazamo tofauti ya wachangia hoja. Nchi yetu ni kubwa sana na hii inaweza kuleta maendeleo kwa kiasi chake, lakini pia kufanya watu wanufaike na rasmali zao zenye zinapatika kwa eneo lao. Binafsi mfumo huu naupenda sana unaleta radha katika maendeleo, mfano CHADEMA mfumo wa kanda umesaidia sana kukipeleka chama kwa UMMA zaidi mafanikio ni makubwa kwa muono wangu.
Ili kusonga mbele kama Taifa na kuleta maendeleo sawa kwa watu tubuni Majimbo since our Country is large tuingie kwenye mfumo huu. Na iwe hivi: Mwanza, Kagera, Geita, Mara liwe jimbo liitwe hivi BUKOBA STATE or COUNTY, Shinyanga, Tabora Katavi yaitwe TABORA STATE. Dodoma, Singida Morogoro, Yaitwe DODOMA DC STATE. Dar, Pwani, Tanga Yaitwe DAR ES SALAAM STATE. Lindi, Mtwara, Ruvuma, Yaitwe COASTAL STATE. Arusha, Manyara, Kilimanjaro Yaitwe KIRIMANJARO STATE. Kigoma, Rukwa, Yaitwe WEST STATE. Mbeya, Iringa, na mkoa mwingine hapo nimeusahau Yaitwe GREEN STATE, UNGUJA STATE na PEMBA STATE. Mimi naona hivyo, unaweza kuborasha ili kuweka usawa wa rasmali kwa STATES au COUNTIES zote.
Mfumo wa majimbo una changamoto kubwa mno
Uchukulie umeme unazalishwa kidatu.Jimbo la kidatu litataka lifaidike na huo umeme kuwa ni wao sababu unatoka kidatu.Tatizo linakuja watu wa kidatu hawana pesa za kuweka mitambo ya kuzalisha umeme.Na hawana dhamana ya kuweka kwenye mabenki ili wakope pesa za kuweka mitambo.Kitakachotokea watabaki na maji yao ya kuzalisha umeme kwenye jimbo lao.
Hata gesi na mafuta ni hivyo hivyo.Mitaji yake inahitaji nguvu ya kitaifa kuimudu si kijimbo.Na hata wakitaka kuuza hiyo gesi au umeme itabidi kuingia mikataba na kila jimbo ya kuuziana umeme na jimbo likubali kutoa ardhi kwa ajili ya miundo mbinu ya nguzo n.k jimbo moja likigoma laweza kwamisha majimbo mengine kukosa huo umeme sababu jimbo lingine laweza sema staki umeme wako wa maji nitatumia wa kwangu wa makaa au upepo na sitaki upitishe nguzo kwenye ardhi yangu.Sababu ardhi ni mali ya majimbo
Dar esalaam mfano yaweza sema mapato yote ya bandari ni yangu sababu iko kwangu.Wengine wakasema usipate shida sawa baki nayo lakini sisi jimbo la kigoma hatutengenezi barabara wala reli ya kupeleka mizigo yako kongo.Tutatumia bandari za angola na hatukupi ardhi ya barabara kwa ajili ya wafanyabiashara wako wa kongo wanaotaka kutumia bandari yako ya dar es salaam.
Ukienda mikoa inayozalisha chakula kwa wingi mfano nyanda za juu kusini waweza goma uzia majimbo mengine chakula wakaamua kupeleka chakula chote zambia na hakuna jimbo litawafanya chochote.Sababu kila jimbo ni mmiliki wa njia zake kuu za uchumi lina sera zake na mambo yake na bunge lake.
Hiyo ni mifano michache tu.
Ni rahisi kuimba majimbo,majimbo lakini uendeshaji wa serikali za majimbo ni kizungumkuti
wazo lako siyo jipya. soma hapa: theeastafrican.co.ke/OpEd/letters/Devolved-system-of-govt-may-just-be-what-Tanzania-needs/-/434756/2207574/-/fd6qut/-/index.html
Ili kusonga mbele kama Taifa na kuleta maendeleo sawa kwa watu tubuni Majimbo since our Country is large tuingie kwenye mfumo huu. Na iwe hivi: Mwanza, Kagera, Geita, Mara liwe jimbo liitwe hivi BUKOBA STATE or COUNTY, Shinyanga, Tabora Katavi yaitwe TABORA STATE. Dodoma, Singida Morogoro, Yaitwe DODOMA DC STATE. Dar, Pwani, Tanga Yaitwe DAR ES SALAAM STATE. Lindi, Mtwara, Ruvuma, Yaitwe COASTAL STATE. Arusha, Manyara, Kilimanjaro Yaitwe KIRIMANJARO STATE. Kigoma, Rukwa, Yaitwe WEST STATE. Mbeya, Iringa, na mkoa mwingine hapo nimeusahau Yaitwe GREEN STATE, UNGUJA STATE na PEMBA STATE. Mimi naona hivyo, unaweza kuborasha ili kuweka usawa wa rasmali kwa STATES au COUNTIES zote.
It should be pigeonholed as Eastern province (Morogoro,Pwani,Dar);Western Province (Kigoma,Tabora,Mara);Lake Province (Mwanza,Shinyanga,Kagera);Northern province (Manyara,Arusha,Tanga,Kilimanjaro);Central province (Dodoma,Singida);Southern highlands province (Rukwa,Katavi,Ruvuma,Iringa,Mbeya);Southern province (Lindi,Mtwara,Mafia);And finally Islands province (Unguja,Pemba).
Mfumo wa majimbo una changamoto kubwa mno
Uchukulie umeme unazalishwa kidatu.Jimbo la kidatu litataka lifaidike na huo umeme kuwa ni wao sababu unatoka kidatu.Tatizo linakuja watu wa kidatu hawana pesa za kuweka mitambo ya kuzalisha umeme.Na hawana dhamana ya kuweka kwenye mabenki ili wakope pesa za kuweka mitambo.Kitakachotokea watabaki na maji yao ya kuzalisha umeme kwenye jimbo lao.
Hata gesi na mafuta ni hivyo hivyo.Mitaji yake inahitaji nguvu ya kitaifa kuimudu si kijimbo.Na hata wakitaka kuuza hiyo gesi au umeme itabidi kuingia mikataba na kila jimbo ya kuuziana umeme na jimbo likubali kutoa ardhi kwa ajili ya miundo mbinu ya nguzo n.k jimbo moja likigoma laweza kwamisha majimbo mengine kukosa huo umeme sababu jimbo lingine laweza sema staki umeme wako wa maji nitatumia wa kwangu wa makaa au upepo na sitaki upitishe nguzo kwenye ardhi yangu.Sababu ardhi ni mali ya majimbo
Dar esalaam mfano yaweza sema mapato yote ya bandari ni yangu sababu iko kwangu.Wengine wakasema usipate shida sawa baki nayo lakini sisi jimbo la kigoma hatutengenezi barabara wala reli ya kupeleka mizigo yako kongo.Tutatumia bandari za angola na hatukupi ardhi ya barabara kwa ajili ya wafanyabiashara wako wa kongo wanaotaka kutumia bandari yako ya dar es salaam.
Ukienda mikoa inayozalisha chakula kwa wingi mfano nyanda za juu kusini waweza goma uzia majimbo mengine chakula wakaamua kupeleka chakula chote zambia na hakuna jimbo litawafanya chochote.Sababu kila jimbo ni mmiliki wa njia zake kuu za uchumi lina sera zake na mambo yake na bunge lake.
Mwenye maji ziwa victoria aweza goma yasitoke kwenda mikoa mingine kwa sababu ajuazo yeye na usimfanye kitu kwani yako kwake.
Hiyo ni mifano michache tu.
Ni rahisi kuimba majimbo,majimbo lakini uendeshaji wa serikali za majimbo ni kizungumkuti
It should be pigeonholed as Eastern province (Morogoro,Pwani,Dar);Western Province (Kigoma,Tabora,Mara);Lake Province (Mwanza,Shinyanga,Kagera);Northern province (Manyara,Arusha,Tanga,Kilimanjaro);Central province (Dodoma,Singida);Southern highlands province (Rukwa,Katavi,Ruvuma,Iringa,Mbeya);Southern province (Lindi,Mtwara,Mafia);And finally Islands province (Unguja,Pemba).
Na wewe unatuletea kitaarifa kwa ku-quote kigazeti chochezi cha EAST AFRICAN cha kijangili ambacho hata usajili hakina ambacho kimefungiwa tanzania.
Ipo Kazi kubwa ya kufanya kuwaelimisha hawa watu,ni wabishi lakini hakuna wanalijua.Kenya, USA na nchi zingine wanaongoza kwa kutumia majimbo chini ya magavana
Je wana maraisi wangapi wa nchi? Fikiria kabla ya kuandika chochote
Hayo unayoyaongea yalishawahi kutokea ktk nchi gani duniani inayotumia mfumo wa mfumo wa majimbo? watanzania bana mnapenda kuwa na hofu juu ya kitisho cha kufikirika!Hivi jimbo litagomaje umeme usipelekwe ktk majimbo mengine ikiwa majimbo yote hayo yanawajibika kwa katiba moja ambayo ndiyo dira ya kila kitu ya taifa?Unataka kusema kila jimbo litakuwa na uhuru kamili pamoja na katiba yake yenyewe?
Marekani kafuatilie kila jimbo lina katiba yake.Ndio maana majimbo mengine yanaruhusu ushoga mengine hayataki na wameweka kwenye katiba zao.
> Ahaa sisi hatutaki kuwa kama United States ila ndo maana tuna rasmali watu ambao wanaweza kutusaidia ambao ni sisi wenyewe kuwa na mfumo wetu wa majimbo bila kukopi popote na siyo lazima tufanane vyote tujishughulishe hatuigi tufanye yetu.