Ni wakati muafaka sasa nchi ikaendeshwa kwa majimbo

Mleta mada ungeelezea kwanza kwanini serikali za mitaa zimeshindwa kutimiza jukumu la kuleta hayo maendeleo mikoani. Kwamba serikali za majimbo ndizo zitaweza.
 
Samahani dogo. Umesema NGORONGORO NI MBUGA KUBWA KULIKO ZOTE DUNIANI.... Hebu rekebisha kwanza hapo.
 
Samahani dogo. Umesema NGORONGORO NI MBUGA KUBWA KULIKO ZOTE DUNIANI.... Hebu rekebisha kwanza hapo.
kwa mjibu wa sharia haiwezi kuwa unavyodhani kuwa wengine watakataa rasilimali kwenda kwenye jimbo lao , ipo mifano mingi ambavyo sera hii imefanikiwa sana hasa nenda india kulikuwa na jimbo la GUJARAT ambalo lilikuwa maskini sana na kame kutokana na kuwa na jangwa lakini walipata kiongozi bora ambaye kwa sasa ni waziri mkuu wa india ambaye alihakikisha GUJARAT inapata maendeleo ya kutosha pamoja na kwamba jimbo lilikuwa kame alichokifanya ni kuhakikisha kuwashawishi wawekezaji kwenda kuwekeza GUJARAT kwa bei nafuu ukilinganisha na majimbo mengine leo GUJARAT inamafanikio makubwa yaliyopelekea hata huyo kiongozi wao kupata nafasi ya kuwa waziri mkuu wa nchi kutokana na ubunivu
 
Mleta mada ungeelezea kwanza kwanini serikali za mitaa zimeshindwa kutimiza jukumu la kuleta hayo maendeleo mikoani. Kwamba serikali za majimbo ndizo zitaweza.
kwakua serikali za mitaa hazina mamlaka kamili bali zimekuwa mawakala wa serilikali za halmashauri na halmashauri nazo kuwa wakala wa serikali kuu. upo hapo
 
kwa mjibu wa sheria haiwezi kuwa unavyodhani kuwa wengine watakataa rasilimali kwenda kwenye jimbo lao , ipo mifano mingi ambavyo sera hii imefanikiwa sana hasa nenda india kulikuwa na jimbo la GUJARAT ambalo lilikuwa maskini sana na kame kutokana na kuwa na jangwa lakini walipata kiongozi bora ambaye kwa sasa ni waziri mkuu wa india ambaye alihakikisha GUJARAT inapata maendeleo ya kutosha pamoja na kwamba jimbo lilikuwa kame alichokifanya ni kuhakikisha kuwashawishi wawekezaji kwenda kuwekeza GUJARAT kwa bei nafuu ukilinganisha na majimbo mengine leo GUJARAT inamafanikio makubwa yaliyopelekea hata huyo kiongozi wao kupata nafasi ya kuwa waziri mkuu wa nchi kutokana na ubunivu
 
Tanzania tuna majimbo mawili na yanasumbua kama nini.Kuna jimbo la Tanganyika na Jimbo la ZAnzibar.Kilichopo unakijua.Ukianzisha majimbo mengi zaidi ya ZAnzibar unaelewa mziki wake utakavyokuwa mmzito.Hili la Zanzibar tu pasua kichwa.
Zanzibar ni habari nyingine-lakini hiyo haituzui sisi Tanganyika kwenda na majimbo yetu halafu Zanzibar ikakutana na serikali ya Tanganyika. Katiba yao inasema ni nchi hawawezi kukubali kuwa jimbo au waonekane kuwa ni sawa na jimbo.
 
Wazo zuri ila kuna kitu kimoja sijakielewa au hujaweka sawa ikiwa serikali za majimbo zitajiamlia mambo yao kuanzia kwenye kodi mpaka mipango ya maendeleo yao na kijamii, nini utakuwa wajibu wa serikali kuu mbili serikali kuu itapataje mapato yake ikiwa kila jimbo linajiamlia mambo yake na kupanga Mipango take kimaendeleo???
 
Nadhani hii habari ni sawa ili usimamizi wa fedha uwe rahisi katika miradi ya maendeleo.Mfumo tulionao unaruhusu 10% nyingi sana.Hivyo kufanya miradi kutofikia malengo ama kuwa chini ya kiwango.
 
Kuna watu wanasema mikoa mingine itadumaa,kwani kwa mfumo huu si udumavu uko vilevile isipokua Dodoma inayojengwa na serikali? Bora kuwa na Count gvnt kama wakenya ili fedha ya majimbo igawiwe sawa.Sasa hivi 60%ya bajeti inaenda Dar,Ar na Mwanza tu.wapi maendeleo hapo?
 
Hizi akili ndo zinarudisha nyuma maendeleo ya nchi. Nyie watu wa dizaini hii mnatuchelewesha sana nyie.. Mxeeuuuuuuu
 
itakuwa kama icon ya nchi kama kutuwakilisha kwenye mataifa mengine , msimamizi mkuu wa majimbo , vyanzo vyao vya mapato vitakuwa kama kodi za kitaifa kutoka kwenye majimbo, misaada ya wahisani , n.k
 
Zanzibar ni habari nyingine-lakini hiyo haituzui sisi Tanganyika kwenda na majimbo yetu halafu Zanzibar ikakutana na serikali ya Tanganyika. Katiba yao inasema ni nchi hawawezi kukubali kuwa jimbo au waonekane kuwa ni sawa na jimbo.
Ukianzisha majimbo katiba pia unatakiwa ubadilishe isomeke Tanganyika ni nchi inayoundwa na majimbo ambayo yanakuwa huru na yenye raisi wake (gavana wa jimbo) ambaye huchaguliwa na wananchi wa jimbo husika chini ya tume yao huru ya uchaguzi ya jimbo lao ambayo haiingiliwi na Magufuli kama ile tume ya uchaguzi ya Zanzibar ambayo haiingiliwi.Kuanzisha majimbo ni kuigawa nchi vipande vya nchi ndogo ndogo nyingi zenye raisi wao (gavana wa jimbo) ambaye hateuliwi na raisi wa nchi wala hawajibiki kwake.Akivurunda raisi hana nguvu za kumgusa maana kale ni kainchi kengine.
 
Nakubaliana na wewe isipokuwa sio lazima raisi wa JMT awe na uwezo wa kumgusa kila mtu kutokana na nguvu za uraisi. Hapo itabidi tuwe na institutions zinazodeal na cheks and balances ndani ya kila jimbo. Hii habari ya kuwa na raisi ambaye nchi nzima inafuata kile akipendacho haiendani na filosofia ya majimbo. Kuwa na majimbo haina maana kuwa viongozi wake watatenda watakayo (katiba itafafanua nafasi ya kila mmoja wetu) na kuna vyombo vya dola ambavyo vinamamlaka yake. Kosa katika jimbo linaweza likatakiwa kushughulikiwa na serikali kuu.
 
.Sasa hivi 60%ya bajeti inaenda Dar,Ar na Mwanza tu.wapi maendeleo hapo?
Kwani hiyo mikoa ya DAR,arusha na mwanza inaingiza asilimia ngapi ya mapato ya nchi? Hiyo 60% wanayopewa wanapunjwa ukilinganisha na mapato wanayoingiza.Mikoa mingine inaendelea kwa expense za mikoa hiyo mitatu ambayo ina shughuli nyingi za kiuchumi za kuingiza pesa.Na penye shughuli nyingi za kiuchumi za kuingiza pia huwa na gharama kubwa za bajeti za kuendesha huo uchumi.Sipingi mikoa mingine kupelekewa fungu kubwa lakini kuna mikoa haina shughuli za kiuchumi za maana.Hata ukiwajengea barabara ya lami wanaweza ishia kuitumia kuanika mazao kwenye hiyo barabara sababu hamna magari yanayotumia hiyo barabara kiuchumi.

kUNA Maeneo waweeza mfano toa milioni mia kwa ajiri ya vikundi vya akina mama au vijana kujiajiri au kuanzisha biashara hizo pesa usishangae zikarudishwa zote kwa kukosa watu
 
Unajua YEHODAYA Nchi haiwezi kuitwa imeendelea kwa kujenga miundombinu sehemu moja ya Nchi.Unapojaza vitu sehemu moja,matokeo yake watu nao hujaa sehemu hiyo.Hivyo Hutakaa useme kuwa tayari nimejenga ila utakuwa unajenga na kubomoa,which is happening in Dar today! Maendeleo hugawanywa Nchi nzima ili kurahisisha maisha ya wananchi.Usitarajie TZ kuendelea kwa kujenga mikoa hiyo niliyotaja tu, nawapongeza sana Chuo cha SAUT kwa kuelewa hili na sasa tunaona mchango wao mkubwa kwenye kuendeleza mikoa.
 
Naunga mkono hoja... hoja ya mikoa mingine kufa kiuchumi ndo inatufikisha hapa... Hata nchi zilizosaidia nyingine kifedha kupata uhuru ndio nchi masikini hadi leo...hoja ingekuwa kweli kuna jimbo naliona likitoa misaada ya kifedha kwa majimbo mengine
 
nakuunga mkono tukiwa na selikali za majimbo tutakuwa tumetatua tatizo la muundo wa muungano, jimbo state)laweza kuwa na mikoa mitatu au mine, twaweza kuwa na majimbo kumi tu zanzibar inclusive yakiongozwa ma magorvenor wateule wa raisi,lakini mikoa iongozwe na wakuu wa mikmag
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…