Ni wakati sahihi, kwa Rais Samia kuongea na mabalozi wote na jumuiya za kimataifa!

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
20,561
Reaction score
24,428
Kwa vyovyote hawa ndugu zetu wasiotakia mema taifa letu, watakuwa wamesambaza vipeperushi vya hovyo katika jumuiya mbali mbali za kimataifa, ili mradi tu, malengo yao ovu, yatimie ikiwepo extensions za ukaazi wao wa kikimbizi huko ughaibuni, pia ikiwepo kutafuta huruma ili wamiminiwe fedha kwa ajili ya matumbo yao!,
Ni hekima, kukaa nao, na kuwaelewesha kinachoendelea, na jitihada za serekali juu ya kutatua haya yaliyojitokeza.
-WASALAAM
 
Mie huwa sifahamu hofu ya Watawala kwa nchi kama Tanzania yenye Wananchi matahira.Hawa Watanzania ninao wajua mimi hata uwaingizie vidole machoni hawaelewi chochote tupo kama makondoo.

SAMIA afuate nyendo za Kikwete acha waongee weee mwishowe watatulia maana ninajua kwa kufanya action hakuna anayeweza na uzuri ni kuwa mifumo ya kiutawala ya hii nchi Rais ndio kila kitu ku control ni rahisi-uhitaji hata kuua na kuteka watu.

80% ya watanzania hawaelewi hata haki zao za msingi,20% ndio hao wasomi waoga na wengi wao hata upeo wao ni zero-yani mtu ukishindwa kuongoza nchi kama Tanzania nchi gani hapa Duniani utaweza kuiongoza.Mie hata Magufuli nilimshangaa kutumia force kwa nchi kama Tanzania bado sana.
 
Mkuu Jino la mamba kuwa mkweli, wewe mwenyewe unakiri kuwa kuna jambo lililojitokeza la kutatua.

Huoni kuwa jambo hilo lipo peupe kujua, hata halihitaji vipeperushi kutoka kwa wapinzani kuwasambazia washirika wetu.

Acha unafiki, wewe unaona serikali kuwaita mabalozi kuwaambia kuwa kuna shida hapa ni sawa, ila wapinzani wao kupaza sauti kuwa twafa, wewe unaona nongwa!!!

Yaani mtu umpige kipigo cha kuuwa mwanae, halafu umzuie kulia! Kweli crocodiletooth!!
 
Ndugu yangu
Unahangaika na mtu ambaye tayari Mungu ameshaachana naye kitambo.

Muache aendelee kuongozwa na shetani akiamini anamsaidia sana
 
Comments reserved
 
Mama alishapwaya kitambo hata wao wanajua.....mwepesi sanaa.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…