Ni wakati sasa Tanzania iwe na wabunge 185 tu. Wabunge 199 wapunguzwe wote wanalitia hasa Taifa hawana masaada kabisa

Ni wakati sasa Tanzania iwe na wabunge 185 tu. Wabunge 199 wapunguzwe wote wanalitia hasa Taifa hawana masaada kabisa

Hivi ukisema halmashauri ni 185 ina maana kuna wilaya hazina halmashauri?..au wilaya pia zipo 185?na set up ya Zanzibar ikoje?
Wana halmashauri ngapi?
Zanzibar kuna bunge la wawakilishi nadhani tittle yangu ndiyo imekosewa pengine ingekuwa tanzania bara
 
Hivi ukisema halmashauri ni 185 ina maana kuna wilaya hazina halmashauri?..au wilaya pia zipo 185?na set up ya Zanzibar ikoje?
Wana halmashauri ngapi?
Na ndio maana pia nimetumia halmashauri sijasema wilaya mkuu
 
Naunga mkono hoja. Pia na vile vyeo vya kupeana ulaji na vya kisiasa kama vya Wakuu wa Mikoa na Wilaya, navyo viondolewe. Havina tija yoyote ile kwa Taifa zaidi ya kuchezea tu kodi za Watanzania.
 
Kabla ya mapendekezo yako lazima kwanza tufahamu kazi za mbunge.Mimi ninaweza kupendekeza pia kuwepo na mbunge mmoja kwa kila mkoa inatosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndio maana nikakwambia kwa bandiko kama hili kuniuliza swali na namna hii nastaajabu kwa sababu mimi nimesema mbunge kila halmashauri kitu ambacho kipo pia katika halmashauri nyingi sasa hayo ya kazi za mbunge sio wajibu wangu kukutajia tembelea tovuti ya bunge ujifunze na uniambie ni kwa namna gani kukiwa na mbunge mmoja kila halmashauri kuta athiri hizo kazi za bunge kama hoja yako inavyo taka kuelekea.
 
Na ndio maana pia nimetumia halmashauri sijasema wilaya mkuu
Mimi nimeuliza ili nijue
Binafsi pia sijui
Je kuna wilaya hazina halmashauri?
Kama tuna halmashauri 185 na wilaya ziko ngapi? Au kila wilaya ina halmashauri?
 
Kabla ya mapendekezo yako lazima kwanza tufahamu kazi za mbunge.Mimi ninaweza kupendekeza pia kuwepo na mbunge mmoja kwa kila mkoa inatosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na hata hiyo hoja yako ya mbunge mmoja kila mkoa nayo naona ina faa tu. ili madiwan ambao ndio walio karibu kabisa na wananchi wawe wafikisha taarifa kwa muwakilishi wao mmoja wa mkoa kule bungeni ambaye naye atapata taarifa na mahitaji ya wananchi kwa kutoka kwa wenyeviti wa halmashauri .

Sasa kama mkoa mmoa una wilaya 4 au tano na mkoa wenye wilaya nyingi sana hazizid 9 sasa kwani hawa wenyeviti wa halmashauri 9 kwa pamoja nao wanakaa na mbunge wao mmoja wa mkoa ambaye ataenda kuwawakilisha bungeni . Mi naona hata hiyo inawezekana kabisa.
 
Mtazamo wako ni mdogo sana, tataizo hujui nini kazi ya Bunge. Na hii yote imetokana na jinsi Ndugai alivyoliharibu ndio maana umefikia huko. Wabunge ndio wapo kwa ajili ya wananchi, sasa ukitaka wapunguzwe eti kuokoa matumizi, Kuna siku utasema hata wanajeshi wapunguzwe.
Ndiyo ! Hayo ni maoni yangu ya dhati kabisa ili kupunguza matumizi ya fedha za umma

Tanzania ina halmashauri 185 tu ambazo zingetosha kabisa kuwakilishwa na mbunge mmoja mmoja kila halmashauri wakisaidiwa na madiwani

Kuwa na wabunge 384 kwa nchi kama tanzania ambayo ina changamoto nyingi za kimaendeleo kwa wananchi ni matumizi mabaya kabisa ya pesa za umma

Hawa wanao itwa wabunge wa viti maalumu wooote ni wakuondolewa wamekuwa mzigo kwa taifa na hawana faida chanya kwa watanzania

Wabunge wote wawe wakuchanguliwa na wananchi na taratibu za kuwapata hawa wabunge pia ziangaliwe upya nchi ina matatizo mengi sana inahitaji wabunge wachapa kazi na wenye nia ya dhati kutatua kero za watanzania na sio kupata wabunge wenye ubingwa wa kujibizana bungeni kwa maneno machafu na kejeli.

Tukiokoa pesa ambayo ingetumika kwa wabunge 199 kuwalipa posho na gharama zinginezo ilihali hawana tija yeyote kwa taifa itasaidia sana kuboresha changamoto nyingi sana

Piga hesabu posho na marupupu yoote wanayo lipwa wabunge hao kwa kipindi chote cha ubunge wao pesa hiyo ingejenga madarasa mangap na vituo vya afya vingapi

Yawezekana kuna wakati Mh. Rais anapata wakati mgumu ku alocate fedha za kutatua changamoto za watanzania kwa sababu pesa nyingi zinahudumia wanasiasa ambao kimsingi hawana tija wala michango chanyana ya kimaendeleo kwa wananchi wanao wazunguka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbunge atakiwa kuwa mtu mwenye hekima.Kujaza watu wengi bungeni kwa gharama ya walipa kodi ni UFISADI.Wengi wao wanataka ubunge kama kinga au fursa.
Hivi kwa serikali hii ya CCM,mbunge ana kazi gani?
Sioni faida yake kwa utawala wa sasa.Kwani maamuzi yote anayamaliza Raisi Magufuli pammoja na Waziri Jaffa wa TAMISEMI.
Kama kweli mnataka bunge,linatakiwa lisifanye kazi ya serikali,lifanye kazi ya bunge,liweze kungata serikali.
 
Wabunge wa kuteuliwa ni muhimu, kumbuka katiba inasema ili uwe waziri ni lazima uwe mbunge! Wananchi wakichagua vilaza wote raisi atatoa wapi mawaziri?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja. Pia na vile vyeo vya kupeana ulaji na vya kisiasa kama vya Wakuu wa Mikoa na Wilaya, navyo viondolewe. Havina tija yoyote ile kwa Taifa zaidi ya kuchezea tu kodi za Watanzania.
Wabunge viti maalum,wakuu wa mikoa,wilaya na makatibu tarafa ni wanasiasa ambao siyo wanasiasa wasio na kazi rasmi.Kazi wanayoifanya hasa ndiyo sababu ya uwepo wao ni kuhakikisha CCM ni salama na inaendelea kuwepo ili washibe.
Huu ni ufujaji wa Mali ya umma.Tunapokosa maendeleo tunalalamikia mabeberu wakati mirija hii tunailea wenyewe.
Tudai Katiba Mpya tuikarabati nchi yetu,maana ni yetu sote na siyo Mali ya CCM.
 
Mtazamo wako ni mdogo sana, tataizo hujui nini kazi ya Bunge. Na hii yote imetokana na jinsi Ndugai alivyoliharibu ndio maana umefikia huko. Wabunge ndio wapo kwa ajili ya wananchi, sasa ukitaka wapunguzwe eti kuokoa matumizi, Kuna siku utasema hata wanajeshi wapunguzwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huenda wewe ni mbunge ndio maana unang'ang'ana kusema eti kazi ya bunge

Ni ujinga ulio pitiliza eti kupinga kwa kwa kigezo cha kazi ya bunge hakuna asiye jua kazi za bunge na zinafundishwa hata mashuleni tangu primary kama sikosei

Kazi za bunge hazimaanishi zinahitaji wabunge rundo ambao hawana hata tija wala masaada na hakuja kazi zinazo lazimisha kuwa na wabunge 384

Na haimaanishi wakibai wabunge 185 hawataweA kutekeleza majukumu yao huo utakuwa ni utetezi wa mtu mwenye akili ndogo kama wewe mwenyewe

Wabunge 185 wanatosha kabisa kutekeleza majukumu na kazi zote za kibunge tena kwa ufanisi mkubwa sana kuliko kuwa na utitiri wa wabunge ambao 75% ya wao hawana faida yeyoye ile wala mchango wowote wa taifa zaid ya kulitia hasara

Na wanaweza kutimiza majuku na kazi zao hata wakiwa chini ya hapo kwa sababu kazi za bunge zipo bayana na hata kwenye tovuti ya bunge zipo hivyo nazijua vizuri sana tena nadhan zaid yako Mh mbunge.

Maana kujua kazi za bunge halafu huzitekelezi ni sawa nankuto zijua kabisa
 
Wabunge wa kuteuliwa ni muhimu, kumbuka katiba inasema ili uwe waziri ni lazima uwe mbunge! Wananchi wakichagua vilaza wote raisi atatoa wapi mawaziri?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii sio sababu maana kama idadi ya wabunge itabadilishwa maana yake hata vigezo vya kupata wabunge hao pia vitabadilishwa na historia inaonesha ni mawaziri wachache wakuteuliwa wamepaform vizuri.

Na wakati huo tambua kwamba waziri ni kiongozi wa mpito tu kwenye wizara hivyo uwepo wake au kuto kuwepo kwake hakuta athiri chochote kwenye wizara husika maana mtendaji mkuu ni katibu mkuu wa wizara ambaye ndiye anatakiwa awe na taaluma stahiki inayo husiana na wizara husika ingawa ni muhimu sana waziri awepo katika wizara maana ndio mfumo bora wa utawala ulio zoeleka na tulio rithi kwa wakolono

Kifupi kuna reformation kubwa sana inatakiwa ifanyike kwenye mfumo wa utendaji na chain of command katika nchi ya tanzania.
 
Kuna watu wapo bungeni miaka yote hata kuongea huwezi sikia wakiongea, au wanaongea mara moja kwa miaka mitano na hiyo nafasi waliyopewa wanamwaga upuuzi. Ukweli bora wapunguzwe tu. Ingekua mimi ningeenda extreme kabisa wabaki chini ya 150. Kama kila mwananchi ana representative wake inatosha kabisa, mtu moja kurepresent watu wengi si mbaya USA yenyewe ina senators 100 bungeni, kama wanahitajika wengine wangewekwa ila sio kwa mshahara wa mbunge, wangekua chini ya wabunge main na wakalipwa maybe 2/3 au hata 1/2 ya mshahara wa mbunge.

Wabunge wangekua wanapiga kazi kweli nisingelakamika ila kutokana na kwamba wengi wamekaa tu bora wapungue kupata ubunge iwe competition kubwa kuleta watu competitive peke yake
 
Kabla ya kusema hawapigi kazi,unazifahamu kazi na mamlaka ya bunge la Tanzania?
Kazi na utendaji wa Bunge la Tanzania unaweza kulifananisha na House of Representatives ya US?
Kuna watu wapo bungeni miaka yote hata kuongea huwezi sikia wakiongea, au wanaongea mara moja kwa miaka mitano na hiyo nafasi waliyopewa wanamwaga upuuzi. Ukweli bora wapunguzwe tu. Ingekua mimi ningeenda extreme kabisa wabaki chini ya 150. Kama kila mwananchi ana representative wake inatosha kabisa, mtu moja kurepresent watu wengi si mbaya USA yenyewe ina senators 100 bungeni, kama wanahitajika wengine wangewekwa ila sio kwa mshahara wa mbunge, wangekua chini ya wabunge main na wakalipwa maybe 2/3 au hata 1/2 ya mshahara wa mbunge.

Wabunge wangekua wanapiga kazi kweli nisingelakamika ila kutokana na kwamba wengi wamekaa tu bora wapungue kupata ubunge iwe competition kubwa kuleta watu competitive peke yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja. Pia na vile vyeo vya kupeana ulaji na vya kisiasa kama vya Wakuu wa Mikoa na Wilaya, navyo viondolewe. Havina tija yoyote ile kwa Taifa zaidi ya kuchezea tu kodi za Watanzania.
Naunga hoja mkono.
 
Back
Top Bottom