Ni wakati sasa wa kubadili Falsafa za Mwalimu Nyerere na kuchunguza na kuhoji mienendo yake

Nyerere alikuwa na dosari zake, lakini Nia yake ilikuwa nzuri, NI Raisi pekeye TZ aliyeondoka madarakani akiwa Hakujitengenezea au kujibambikiza Mali. Lakini sijui kwanini tunailaumu Zanzibar, Sultan Tumempindua Sisi, Karume na maraisi wao Wote tumewaweka vitini Sisi, Znz tumeishikilia na kuingangania Sisi, na tunaolalamika NI Sisi.

Fursa tuonazo kama Znz wanafaidika nazo, Sisi ndio tulizozileta na ili tuu waukubali muungano. Kama hautufai njia NI Raisi na wao pia wataifurahia, na NI KUWAPA UHURU WAO KWA KUVUNJA MUUNGANO
 
Badala ya kumwita mtu" illiterate" ,unamwita mtu " msikivu".
Yule mdada mmoja( mzungu) alikua anamsifu sana Samia jana.
Anasema,"you can take a girl out of Zanzibar,but you can't take Zanzibar out of a girl.'
Mimi sijamsifu rais huyu,lakini pia bado sijampinga.
Kwa sababu ukimsifu mtu,utaambiwa tupe sababu kumi. Ukimkashifu,utaambiwa tupe sababi kumi kwa nini umemkashifu.
Kama rais huyu atapata matatizo,nitasoma katika gazeti,as a complete surprise, as it was in the case of Magufuli.
Kwa vile it is not safe kuwasema vibaya viongozi waliopo madarakani sasa hivi,unataka kuwasema vibaya viongozi wa zamani.
Sasa,mimi nipo kijijini,na hapa, I am just 50 metres from the grave.
Umesema mwenyewe Nyerere alikuwa left- wing politician. Kwa hiyo it is irrelevant kumtaja sasa kwa sababu hiyo siyo siasa yetu sasa.
 
Kwa maana ya kuwa Tanganyika inaitawala Znz ?
 
Mnahangaika sana na urais wa Samia, akija mtu wa bara hizi nyuzi zinapotea. Chuki za kipuuzi hazitusaidii kwani huyo Samia anafanya mengi ya maana yenye kugusa maisha ya watu wengi ambao hawamo humu JF.
 
Nyerere aliongoza Tanzania ikiwa na watu chini ya milioni tano ikiwa na chuo kikuu kimoja tu pale Mlimani, ikiwa na rundo la wajinga kila sehemu.


Falsafa zake zilikuwa na mashiko enzi zile kwa mazingira ya wakati ule. Haipo mantiki yoyote ya kuhoji falsafa za wakati ule katika miaka ya sasa.
 
Naunga mkono hoja
 
Hizi fikra wamerithi watu wetu kiasi kwamba wakiwa hata na vyeo vidogo tu basi hujiona ni Kila kitu na wao ndio wenye kuliko Kila mtu, na hii hupelekea hata Rais wa nchi akikosolewa sera na mienendo yake huona ni dhambi kubwa.

JKN kama binadamu anamakosa yake ambayo yanapaswa kusahihishwa ili twende mbele na sio kumchukulia yeye ndio kama msahafu au biblia ya maisha yetu kama Taifa huku tukiona kabisa maeneo mengi alifail na sera zake ndio zimetufikisha hapa.
 
Unataka kutuambia hakuwaza kama Tanzania watu watazaliana, watu watasoma nk, inamaana allifikiria Tanzania itaishia hapohapo.

Hili bila shaka ndio limeleta madhara Kwa waliopo sasa kuwaza Leo na si Kwa niaba hata ya vizazi kumi mbele.

Falsafa zinapaswa kuishi.
 

Kuhoji na kuchunguza ni haki ya msingi ya katiba, as long as hatuvunji sheria.

Muungano haina maana hatutakiwi kuuboresha pale inapobidi.

Mambo ya Mwijage sio msaafu wa kila mtu kuufuata. Na sio yeye tu anayeandika mambo ya Nyerere vile alivyoona. Ndio ubinadamu wetu ulivyo
 
Zanzibar ni sawa na kinondoni kwa idadi ya watu, ni sehemu ndogo sana ya JMT, hizi nongwa zinamlenga Samia na urais wake na waanzilishi ni hao hao wanasiasa tutakaoyaona majina yao wakati wa kampeni mwakani wakiutaka urais.
 
Nadhani uwezo wako wa kufikiri hauna tofauti na kuku

Umejaa ujinga,

But wengi wanaomchukia Nyerere ni walee wafuasi wa....
Alichokiandika ni ukweli mtupu chukulia mfano setup ya mfumo WA elimu nchini....unaridhika nao?
Ada irudishwe mashuleni,wazazi wachangie ili kuiondolea serikali hili zigo la mikojo yetu.

HUDUMA YA AFYA NDIYO IPATIKANE KWA GHARAMA NAFUU ILA ELIMU TULIPIE.
 
Jenerali ulimwengu ,alishawahi mpa makavu huyu babu kuhusu mambo yake

Anasema ,hata ukiifatilia katiba iliandikwa kilakitu kwa maamuzi yake ,zingatia kuanzia umri wa kugombea urais
 
Unaona falsafa za Mwalimu JK haziishi kwa sababu unazitazama kwa mtazamo wa 2024, ikifika 2060 watakaokuwepo wataziona hizi falsafa za sasa zimepitwa na wakati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…