Mkuu hujatoa fununu kuhusu kiasi na umri wa watu ambao wanaweza kutumia katika jamii. Nasema hivyo kwa kuwa matumizi ya vilevi kuna tahadhari inatolewa kuhusu wale wenye umri zaidi ya miaka 18, kutokunywa kwa kupitiliza na pia unywaji uwe wenye kumtaka mnywaji kuwajibika mwenyewe endapo matokeo ya unywaji wake yatakapo leta taflani fulani.
Aidha katika matumizi ya mazao ya tumbaku, tunaona tahadhari ikitolewa kwa kuzingatia umri pia kuhusu adhari za kiafya kwa mtumiaji. Sasa hii kitu hii šBANGE š tahadhari gani itatolewa kuhusu matumizi yake kwa kuzingatia umri unaokulabilika, sehemu rasmi za uvutaji wake (kwa wale wavutaji), athari zake za kiafya (natambua zipo kwa kuwa bange inaorodheshwa kama mojawapo ya madawa ya kulevya hapa nchini),, harufu (kwa maana kitu huwa kinatema! š©), ikiwa katika hali yake uasilia, yaani, "crude form" ama "processed" n.k.
Mtoa mada jaribu kudadavua zaidi ili tupime kwa nini nchi chache sana zimehalalisha matumizi yake, wakati nchi nyingi zikiwa zimepiga marufuku matumizi yake. Ukizichunguza kwa umakini baadhi ya haki za binadamu zinakwenda kinyume kabisa na maadili ya Mwafrika, na imani zake za kiroho. Agenda nyingi zenye nia mbaya zinapenyezwa "overtly or covertly" zikiwa na nia mbaya ya kumfanya Mwafrika awe "derailed and brainwashed par excellence"!
Tumbaku sio asili ya mwafrika lakini imehalalishwa na ililetwa na Wakaloni wakawafundisha wazee wetu kuvuta kiko na wengine kutumia Ugoro. Tumbaku inatengeneza Siagari ambayo pia sio asili yetu.
Pombe zote za viwandani zililetwa na Wazungu sio asili yetu.
Pombe za kienyeji zinapigwa vita sana na serikali kwa sababu serikali ni matokeo ya Ukoloni.
.Bangi ni zao la asili linaloota kwenye misiti na Mbuga zetu kama ilivyo pia Mirungi. Haya mazao yanaota yenyewe na kiasili ni dawa na sehemu nyingine ni mboga
nyungu inavyofanyika.
Mimea au mazao yaliyoletwa na Wakaloni kama vile tumbaku hayawezi kuota kwenye mapori yetu bila kulimwa na kuhudumiwa kitaalam . Bangi ni mbaya kwa sababu imepewa jina baya kutokana na ushindani wa kibiashara.
Madhara yanayotakana na ulevi wa pombe na uvutaji wa sigara wenye jamii ni makubwa kuliko yale yanayotokana na bangi.
Zao la Bangi linatumika kutengeneza bidhaa nyingi kuliko tumbaku inayotengeneza sigara na ugoro pekee.
Iko hivi ;biashara zote duniani zenye soko kubwa la kuvuka mipaka ya nchi ambazo zinapatikana kirahisi zinadhibitiwa na watawala wa Dunia na familia zao na marafiki zao ndio wanaoweza kuzifanya.
Biashara za Pembe za ndovu.
Biashara za dhahabu.
Biashara za wanyama hai.
Biashara ya bangi kwenye makontena kwenda nje ya nchi.
Biashara ya Mafuta .
Biashara za mirungi
Biashara za madawa kama unga wa kokeini.
Biashara ya kutakatisha fedha.
Mikataba hewa n.k.
Hizi ni biashara za watawala wa dunia . Hakuna mtu anayeweza kuzifanya akatoboa kama hana koneksheni na watawala wa dunia hii.
Ndio maana zikawekewa sheria kali ili watu maskini wasije wakapata fedha kirahisi rahisi .
Tujiulize kwa nini mara nyingi watoto wa wakubwa au marafiki zao kote duniani ndio wanaozifanya!?
Kuna wakati Dr.Slaa alimtuhumu Mtoto wa Zakaya ,Lithione kuwa alikamatwa China.
Alipojitambulisha kuwa ni mtoto wa mkubwa ,kilichofanyika ni wakubwa kutaka kuhakiki tu kuwa ni kweli ni mtoto wa mkubwa mwenzao ili aendelee na biashara yake .
Kwa Mujibu wa Dr. Slaa Inasemekana walipopata uhakika kuwa ni mtoto wa mkubwa walimuachia huru bila kunyongwa kwa mujibu wa sheria ya China.
Kwa nini walimwachia mpaka sasa hatujawekwa wazi lakini,ukweli ni kwamba hizo ndizo biashara zinazofanywa na watawala wengi wa Dunia na familia zao hasa wa nchi za Magharibi na Asia na sasa Afrika ndio maana familia zao zinaibuka kwa utajiri mkubwa sana na kwa Muda mfupi.
Hii inasaidia wao kupata pesa nyingi sana mbali na pesa za umma za madafu .
Akitokea mtawala kama JPM atapingwa sana kila kona ya dunia lakini sababu kubwa ni kuzuia biashara hizo nilizozotaja ambazo ni dili kubwa kwa watawala wa dunia lakini kwa wananchi wa kawaida ni marufuku kuzifanya au hata kufikiria kuzifanya.
Mfano tu kukutwa na Gunua la bangi ni kosa kuwa kuliko kuhamishia malipo ya serikali kwenye Akaunti ya mtu na kujaza pesa nyumbani kwenye gunia mana anaweza akazirudisha na mambo yakaisha, na baadae akateuliwa tena kwenda kwenye ofisi nyingine ya kusimamia mapato.