econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Kutokana na sintofahamu kwenye chama Cha CHADEMA inayoendelea sasa hivi ndani ya chama hasa Viongozi kuhongwa na suala la akina Halima Mdee kurudishwa kwenye chama huko mbeleni, nina ushauri maalumu.
Ushauri wangu ni kwamba CHADEMA ijikite kwenye damu changa na siyo kuendelea kuhangaika na majina ya Viongozi waliohudumu CHADEMA Kwa muda mrefu. Hii Hali ya kuwa na Viongozi wa muda mrefu kwenye chama ndio inasababisha mgawanyiko. Maana Kuna Viongozi wengine wanajiona wao ndio Bora kwenye chama bila wao chama hakiendi, hivyo kuleta vitisho vya kuhama.
Mimi nadhani tukiwekeza kwa vijana na kuachana na haya majina makubwa hicho kiburi kitapungua. Kwa mfano kiongozi ndani ya CHADEMA anagombea cheo Fulani , asipokipata anahama chama. Hili tumeliona kwa Katibu Mkuu wa zamani Dr Mashinji aliyeondoka CHADEMA na kuhamia CCM baada ya kutoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA. kwa Msigwa pia baada ya kuanguka uenyekiti wa Kanda ya Nyasa na hata kwa Selasini baada ya kushindwa uchaguzi wa Kanda ya Kaskazini akahamia NCCR. Hii ni hatari Sana. Hivi karibuni Wenje katangaza kugombea umakamu wenyekiti, je akianguka atabaki kwenye chama? au atahama Kama Msigwa. Je John Mnyika asipoteuliwa Tena kwenye Ukatibu Mkuu atabaki kwenye chama? Ila tungekubali kuwapa nafasi vijana ndani ya chama haya mambo ya Kiongozi kugombea nafasi kisa anataka kuhama yasingekuwepo maana anajua akiondoka wapo wengi wa kujaza nafasi yake.
Pia Kuna ujinga Fulani ndani ya CHADEMA ya kwamba kiongozi Fulani akipata ubunge anaanza kuota mapembe na kukidharau chama. Tumeona hili kwa Nassari ambaye alidiriki hata kukacha vikao vya bunge ili afukuzwe ahamie CCM, tumeona kwenye bunge la 2015 kwa akina Silinde, Lwakatare, Kubenea, nk wengi waliohama chama na kukidharau baada ya kupata ubunge, maana walijiona wao Wana majina makubwa hivyo chama kinawahitaji kuliko wao kukihitaji chama. Ila tungewekeza kwa vijana haya maujinga yasingekuwepo.
Mwisho CHADEMA imeshakuwa brand, Sasa tuiuze hiyo brand watu wailewe ili tupate vijana wengi wanachama. Tuje na strategies ya kupata vijana wengi.