Ni wakati turuhusu New Breed CHADEMA


Toka ujio wa Lowassa nilisema Mbowe hastahili tena kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm. Kinachoendelea sasa ndani ya cdm ni madhara ya uongozi wa muda mrefu wa Mbowe kama mwenyekiti wa cdm.
 
Viongozi wa chama wasiwe wabunge Wala madiwani. Na uongozi wa chama, ubunge,udiwani uwe na ukomo at least miaka 10 mpaka 15. Ukishatumikia chama kwenye ubunge,udiwani au nafasi ya juu ya chama ukimaliza muda wako unapisha wengine. Hii itatoa furusa kupata mawazo mapya. Lakini pia kiongozi mmoja asishike nafasi mbili kwa wakati mmoja, hii itasaidia mgawanyo wa madaraka nakutoa nafasi kwa vipaji vipya.

Ingawa sidhani kama itawezekana.
 
Nakubaliana na wewe. Ila Lissu bado anahitajika pale kwenye uenyekiti.
huoni kwamba hiyo itaendeleza cold war baina ya huyo atakae ng'atuka na atakae baki uongozini na kuchochea migawanyiko zaidi, lakini na mipasuko isiyoisha ndani ya Chadema?

hali ya kisiasa inayoendelea hivi sasa ndani ya Chadema, inasemekana ni kuhujumiana katika azma za mafahali hawa wa wawili yaani chairman na vice chairman kufikia ndoto, malengo na matarajio yao ya siku za usoni....

kwa mfano,
chairman ana uhakika 100% wa kukiongoza chama uchaguzi mkuu ujao na kikapata wabunge at least wa5 wa kuchaguliwa na kujihakikishia ruzuku na wingi wa wabunge wa viti maalumu kulingana na wingi wa kura za mgombea urasi ambae, kwa kumtazama body language, tone na facial expressions za mwenyekiti ni dhahiri anapendelea awe Dr.wilbroad Peter slaa na sio huyu naibu wake chamani kama siyo yeye mwenyewe kugombea 🐒

nadhani fresh blood ni muhimu zaidi kwa uhai wa sasa, na kwa mustakabali mwema wa Chadema ya baadae 🐒
 
Asante sana Kwa maoni yako mkuu.
 
Mkileta ujinga tutawafukuza Chadema, na tutaanza na mzee wa buti la Jeje
Wewe na nani?. Unashangaza Sana upo CCM ila unajinasibu Kama mwanachama wa CHADEMA
 
Hakutatokea cold war, maana mwenyekiti alishatangaza anastaafu Sasa sijui ni pesa za Abdul ndio zimemfanya aghairi kustaafu.

Kwa succession plan Lissu alistahili kuwa Mwenyekiti kwa wakati huu kutokana kuaminika na kusimamia ukweli na kuwa mwanaharakati ambayo ndio tradition ya CHADEMA. Mbowe ameshamaliza muda wake makalio yake yameisha.
 
Toka ujio wa Lowassa nilisema Mbowe hastahili tena kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm. Kinachoendelea sasa ndani ya cdm ni madhara ya uongozi wa muda mrefu wa Mbowe kama mwenyekiti wa cdm.
Kweli mkuu, Mbowe hastahili kuendelea kuwa Mwenyekiti. Na akilazimisha kuendelea CHADEMA itaingia kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 ukiwa dhaifu kupindukia na hata CCM haitakuwa na haja ya kuiba kura.
 
Ni Too late nadhani soln ni kupata katiba mpya ili raisi asiwe na nguvu ya kuhonga Kila mtu au kumshawishi Kila mtu

Wapambe wa raisi Wana hela nyingi za rushwa wanaweza kuhonga Kila mtu
 
Mlikubali ushindi wa sugu bila kujua pesa zilipotoka
Msigwa aliyehama anaweza asiwe threat kwa chama kuliko sugu aliyebaki. Amepokea rushwa, imemsaidia kuwa kiongozi mkubwa ndani ya chama. Mmekwisha
 
disrespect na loyalty yenye shaka ya vice chairman inatambakiza chairman chadema mpaka ahakikishe chadema iko mikononi mwa mtu ambae ni loyal na amemuandaa but for sure, not the shouting gentleman 🐒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…