Ni wakinga wachache tupo kwenye mambo ya Siasa, Siasa ni kazi ya ziada kwa wakinga

GUSSIE

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
3,880
Reaction score
11,134
Mimi Gussie nimezaliwa kaskazini na watu wananijua ni wa huko, Mimi ni Mkinga kamili wa Ikonda. Nimekaa sana Nchini Rwanda pia

Anayesemwa sana na watu Mzee Mwakipande aliyekuwa anatoa utajiri alikuwa mjomba wangu na alikwishafariki zamani, Hivi sasa anayefanya kazi za uganga ni mtoto wa mjomba anaitwa Leonard Mwakipande ndiye alirithishwa kazi

Wanaokwenda huko si matajiri tu kama watu wanavyosimuliwa, Kuna watu wana matatizo tofauti ya magonjwa ya ushirikina

Na sio kila tajiri unayemuona akienda huko amefuata utajiri Wengine wamezaliwa huko na huko ni kwao kama mimi GUSSIE

Kama una swali lolote kuhusu huko kwa Mwakipande niulize nitakujibu kwa kadri mimi ninavyoishi na hao ndugu zangu

Mambo mengi yanayosemwa kuhusu sisi wakinga sio kweli, Na hata hizi habari za utajiri kuwa Binamu yangu Leonard Mwakipande anatoa utajiri sio kweli

Kaburi la mjomba ni kweli hakuzikwa kama kuzikwa bali amewekwa kwenye kitanda chake na amejengewa nyumba ndogo tu, Yeye haozi na aliomba asizikwe

Maisha ya huko kwetu kwa sasa yamebadilika sana, Zamani tulitembea kwa miguu toka Ikonda mpaka huko, Leo kuna pikipiki za kutosha

Kuhusu Mimi Gussie kupenda siasa na kufanya kama kitu cha ziada ilitokana na sababu zifuatazo:

Mosi, Wakati huo wazazi wangu wanafanya biashara wao hawakusoma sana na hii ni kwa wakinga wengi wenye biashara hapo kariakoo, Wazazi waliamua kukata shauri na kutupeleka shule watoto ili tujue kuwa wahasibu wao na washauri. Mawazo yao hayo sasa yamefanya wakinga wafanye biashara za kisasa kwa kuzingatia sheria za nchi na kutokulalamika

Kwa kuwa wazazi wetu wengi wa kikinga walikuwa na pesa lakini elimu ndogo kila wakati waliona mambo ya kodi na sheria zinawaonea, Lakini sasa wakinga baada ya sisi watoto kwenda shule mambo yamebadilika na tunashauri wazazi vizuri

Kupitia haya mambo ya kwenda TRA na kurudi, Kuhudhuria vikao vya biashara na wanasiasa yakanifanya na Mimi kwanini nisiingie huko ili kupenyeza agenda zetu wakinga

Pili, Niliumia kuona wakinga ambao wapo kwenye siasa na Wakututetea ni wachache sana, Hata Darasani watu kutoka ukinga tulikuwa kidogo sana, Leo hii hapo Udsm sisi wakinga tuna hata mkufunzi Mkinga haikuwa jambo rahisi

Mwisho sisi ni wamoja na wala huwezi sikia tunagombana ingawa tunagombana lakini mambo yetu tunayamaliza kindugu, Hatuna wivu wala chuki sisi na mtu

Nakaribisha maswali kuhusu wakinga, Uliza nitakujibu

Mpaka Leo Mimi nikisikia Mkinga mwezangu amenunua Gari jipya nitajitahidi ninunue kama gari lake, Wakinga tunaigana sana mambo yetu, Ukifika Njombe pale utashangaa unaweza kuta magari yote ya aina moja

Msitucheke wakinga na mambo yetu ya kuigana kwenye kununua vitu

Any Question? , I 'm here to reply about Kinga' s
 
Asante sana mtani wangu....naomba kujua zaidi kuhusu jinsi mnavyoweza kuuza mikeka na nyungonhadi unanunua marcopolo yako mwenyewe.....tufundishe saving yetu ikoje na jinsi raise fund kwa speed hizo....hiyo nidhamu ndio tunaitaka....mengine story tu ila tujikite hapo....
 
Umenichekesha sana mkuu, Hapo ndipo unapoanza kufeli sasa, Na hapo ndio tunatafutiana kati ya wakinga na wengine kwenye kuthaminisha vitu au Pesa

Usiite mikeka au nyungo ni kitu kidogo, Unakosea sana huwezi fanikiwa ukishasema ni kitu kidogo

Kwanza hakuna kitu kidogo, Wala hakuna pesa ndogo

Kwa biashara ya nyungo na mikeka, Mikeka wakati huo ilikuwa na thamani kubwa sana kwa watu wa Mbeya hasa wanyakyusa. Mnyakyusa alizikwa kaburini na mkeka wa Kamba za migomba na ilikuwa heshima kubwa sana

Wanyakyusa wa Mbeya walipamba mikeka sebuleni na waliitumia sana kwenye sherehe kuwatandikia watu

Wakinga walianza kutafuta ukiri wa kusukia mikeka wakichanganya na Rangi ili kuweza kupata soko na kuwavutia wanyakyusa wengi

Mikeka ya Rangi Rangi iliyosukwa vizuri ilisababisha baadhi ya wakinga wengi wajipatie pesa za kutosha maeneo ya Mbeya na kidogo sehemu za Songea

Kumbuka wakati huo wa mikeka ipo juu sana kwa watu wa Mbeya,

Wakinga walikuwa hawaweki pesa Bank wala hawakujua maana ya Bank, Pesa waliweka ndani na kuzichimbia chini, Ilikuwa ngumu kupata taarifa ya Mkinga Bank

Pesa ndogo unayoita ilikuwa inachimbiwa ndani ya nyumba hata kwa miaka minne, Kwa kuwa hakuna taarifa Bank hivyo ni siri

Anapohitaji kuagiza kitu Mkinga inampsa aende Bank ndio hapo maneno yanaanza na wakati huo Bank ni NBC Bank, Mkinga aliweza kwenda Bulk cash NBC na maguni matano ya pesa ili aagize gari lake nje ya nchi. Maneno yanaanza kuzagaa kuwa muuza ungo na mikeka mchawi na anavuta pesa za wenzake wakati pesa alichimbia ndani kwa miaka hiyo
 
Asante sana mtani wangu....naomba kujua zaidi kuhusu jinsi mnavyoweza kuuza mikeka na nyungonhadi unanunua marcopolo yako mwenyewe.....tufundishe saving yetu ikoje na jinsi raise fund kwa speed hizo....hiyo nidhamu ndio tunaitaka....mengine story tu ila tujikite hapo....
Issue Unawezaje kufanya saving, Nitakujibu najiandaa kidogo nianze elekea kwenye ofisi
 
Umenichekesha sana mkuu, Hapo ndipo unapoanza kufeli sasa, Na hapo ndio tunatafutiana kati ya wakinga na wengine kwenye kuthaminisha vitu au Pesa

Usiite mikeka au nyungo ni kitu kidogo, Unakosea sana huwezi fanikiwa ukishasema ni kitu kidogo
Hizi mada za ukabila nazichukia kwelikweli naziona ni takataka kama kinyesi.Zinatusaidia nini sisi? Baadala ya kuongelea Taifa letu tunalikwamuaje sisi tunakazana na ukabila.Muafrika Mungu kamnyima akili na fikra ndoo maana yote haya yanatokea.
 
Taifa lipi unaliongelea wewe?

Anza wewe kwanza onyesha umefanya kitu gani Halafu tafuta msaada toka kwa wanasiasa, Huwezi kukwepa wanasiasa wao ndio wanaamua kesho yako na wajukuu

Hii mada nimeileta kwa lengo la kuonyesha utajiri wa wakinga ni tofauti na watu wanavyofikiria

Mimi kuwa Mkinga wewe unaumia kitu gani?

Hata siku moja mimi siwezi umia nikiona wachaga wanaenda Moshi mwezi December, Nani amekukataza wewe kwenda kwenu kwenye kabila lako

Wewe Itakuwa ni wale watu wanaodharau walikotoka, Kwenu ni kwenu tu. Siku ukifa watu wanauliza huyu anatoka mkoa gani ni kabila gani?

Hata Ukitaka kuoa watu watauliza huyu anatoka mkoa gani na kabila gani?
 
Usizichukie mkuu kwa sababu hata ukizichukia haita kuja kuwezekana tanzania ikawa kabila moja achana na mambo ya siasa kwenye makabila ya watu, makabila yapo na kuna mambo mengi ya kujifunza kupitia tofauti zetu za makabila hakuna namna

Hizo siasa za kusema kujadili makabila nantaratibu zao ni kuleta ukabila ni mambo ya siasa tu lakini uhalisia makabila yapo na kila kabisa lina namna yake na ni vena kujifunza namba makabila yanavuo jitofautisha kwa sababu haita kuja kuwezekana tanzania ikawa kabila moja. Ila tunashukuru makabila mengi tanzania kuunganishwa na lugha moja lakini haita wezekana kuua makabila yaliyopo.
 
Mimi Gussie nimezaliwa kaskazini na watu wananijua ni wa huko, Mimi ni Mkinga kamili wa Ikonda. Nimekaa sana Nchini Rwanda pia

Anayesemwa sana na watu Mzee Mwakipande aliyekuwa anatoa utajiri alikuwa mjomba wangu na alikwishafariki zamani, Hivi sasa anayefanya kazi za uganga ni mtoto wa mjomba anaitwa Leonard Mwakipande ndiye alirithishwa kazi

Wanaokwenda huko si matajiri tu kama watu wanavyosimuliwa, Kuna watu wana matatizo tofauti ya magonjwa ya ushirikina
Wakinga wastaarabu sana.

Ona Mangula alovyopewa sumu, mzee wa watu akasamehe tu.
 
Taifa lipi unaliongelea wewe?
Anza wewe kwanza onyesha umefanya kitu gani Halafu tafuta msaada toka kwa wanasiasa, Huwezi kukwepa wanasiasa wao ndio wanaamua kesho yako na wajukuu

Hii mada nimeileta kwa lengo la kuonyesha utajiri wa wakinga ni tofauti na watu wanavyofikiria

Mimi kuwa Mkinga wewe unaumia kitu gani?

Hata siku moja mimi siwezi umia nikiona wachaga wanaenda Moshi mwezi December, Nani amekukataza wewe kwenda kwenu kwenye kabila lako

Wewe Itakuwa ni wale watu wanaodharau walikotoka, Kwenu ni kwenu tu. Siku ukifa watu wanauliza huyu anatoka mkoa gani ni kabila gani?

Hata Ukitaka kuoa watu watauliza huyu anatoka mkoa gani na kabila gani?
Umejibu majibu yenye ujazo wa kima cha juu chenye kufurika kombe la upumbavu.
 
Mimi Gussie nimezaliwa kaskazini na watu wananijua ni wa huko, Mimi ni Mkinga kamili wa Ikonda. Nimekaa sana Nchini Rwanda pia

Anayesemwa sana na watu Mzee Mwakipande aliyekuwa anatoa utajiri alikuwa mjomba wangu na alikwishafariki zamani, Hivi sasa anayefanya kazi
Ila wakinga noma sana.
Kumtoa hela mkinga hata kwa faida yake mwenyewe ni kama kukamua jiwe upate juisi.
Ni wagumu kinoma.
Wako tayari hata kunyongwa lakini pesa isitoke, watu wanawasema wapare ni mabahili, hawajawaona wakinga.
 
Asante sana mtani wangu....naomba kujua zaidi kuhusu jinsi mnavyoweza kuuza mikeka na nyungonhadi unanunua marcopolo yako mwenyewe.....tufundishe saving yetu ikoje na jinsi raise fund kwa speed hizo....hiyo nidhamu ndio tunaitaka....mengine story tu ila tujikite hapo....
Kuhusu Saving au akiba

Huwezi kuwa na nidhamu ya akiba kama huna lengo

Kwa wakinga linaanza kwanza neno Lengo baadae inafuata akiba

Ukiweka akiba bila lengo lazima utaitumia hiyo akiba yako

Mfano:Mwaka 2023 nataka niwe na Vanguard new Model hii ndio lengo langu kuu

Natafuta bei ya Vanguard sokoni kwa sasa ni kiasi gani?

Nagawa Bei ya Vanguard na idadi ya miezi au week ili nijue yanipasa kuweka kiasi gani?

Kama nikiona hata nikijibana bado bei ya Vanguard sitaifikia naweza badili aina ya gari kabisa?

Nikiona lengo hilo halifai naachana nalo kabisa

Kuweka lengo ni kazi kuliko akiba, Wengi wana pesa wanayoita ndogo lakini hawajui wafanye kitu gani

Tatizo sio akiba, Tatizo kubwa ni malengo

Lengo moja ukiona haiwezekani weka lengo jingine hii ndio principal yetu sisi wakinga

Nakupa mfano wangu binafsi ambao nimemuambia mtoto wangu juzi anayetaka kuoa

Nimemuuliza una lengo gani mwakani akaniambia anataka kuoa, Nikamuuliza Pesa utatoa wapi zako au za kuchangiwa akanijibu za kwake

Alianza kuweka laki Saba tangu January mwaka huu Kwa ajili ya harusi mpaka sasa muda huu ana Milioni sita na laki tatu 6,300,000. kufika mwakani mpaka mwezi anataka kuoa atakuwa na Milioni zaidi ya tisa za kwake binafsi sio za kuchangiwa
 
Mimi Gussie nimezaliwa kaskazini na watu wananijua ni wa huko, Mimi ni Mkinga kamili wa Ikonda. Nimekaa sana Nchini Rwanda pia

Anayesemwa sana na watu Mzee Mwakipande aliyekuwa anatoa utajiri alikuwa mjomba wangu na alikwishafariki zamani, Hivi sasa anayefanya kazi

Msitucheke wakinga na mambo yetu ya kuigana kwenye kununua vitu

Any Question? , I 'm here to reply about Kinga' s
GUSSIE kuwa tajiri anayemiliki gorofa kubwa au msululu wa basi halafu huwezi kula chakula kizuri na kuvaa mavazi mazuri ni utumwa.

Labda Fred Vunjabei tu ndiye mkinga ninaye muona anaishi kama binadamu. Wengine wote wanaishi kama Fuko au panya buku. Wengi wamewaweka wazaz wao misukule kwenye vyumba vya Siri ndani ya biashara zao.

Na wakivunja masharti hufilisika immediately. Ukinga ni utumwa
 
Kwa vile huwafahamu.
Siye tunaotoka karibu bso tumemwelewa.
Wakinga ni watu poa sana na wakarimu sana nakumbuka mwaka 2002 nikuwa na kazi maalum makete- lupila tukaja hapa ikonda tukamalizia matamba hawana shida ni wakarimu sana halafu wanaushirikiano sana na hasa wakikutana ugenini, ila nilicho gundua kwao ukiwachokoza ni wakorofi sana tena ukorofi wa aina zote.
 
GUSSIE kuwa tajiri anayemiliki gorofa kubwa au msululu wa basi halafu huwezi kula chakula kizuri na kuvaa mavazi mazuri ni utumwa.

Labda Fred Vunjabei tu ndiye mkinga ninaye muona anaishi kama binadamu. Wengine wote wanaishi kama Fuko au panya buku. Wengi wamewaweka wazaz wao misukule kwenye vyumba vya Siri ndani ya biashara zao.

Na wakivunja masharti hufilisika immediately. Ukinga ni utumwa
Wewe ni muongo na story zako za vijiweni hebu tuambie ni nani unae mfahamu na umemuona kamuweka mzazi kwenye chumba cha siri.

Hilo la ubahili ndilo linafanya wakinga hata wakitajirika wasiishi maisha ya anasa ndicho nimejifunza kwao kwa kweli ni mabahili kwelikweli tena hasaa, hata kununua nguo tu huwa anaona anapunguza pesa kwenye mzunguko wa biashara yake.
 
GUSSIE kuwa tajiri anayemiliki gorofa kubwa au msululu wa basi halafu huwezi kula chakula kizuri na kuvaa mavazi mazuri ni utumwa.

Labda Fred Vunjabei tu ndiye mkinga ninaye muona anaishi kama binadamu. Wengine wote wanaishi kama Fuko au panya buku. Wengi wamewaweka wazaz wao misukule kwenye vyumba vya Siri ndani ya biashara zao.

Na wakivunja masharti hufilisika immediately. Ukinga ni utumwa
Mkuu, Ni kweli ule ni ushamba tu wa wazee wetu wa zamani

Kizazi cha wakinga kama Fred Vunja Bei ni kizazi kipya kilichoenda shule na kuwa na exposure

Nenda Leo pale Kariakoo vijana wa Kikinga wapo smart sana na wanakula pamba vizuri

Kama nilivyosema hapo awali wazazi wetu hawakwenda shule, Shule inasaidia pia mtu kuwa mstaarabu sana

Leo hii kuna mabadiliko makubwa sana kwa sisi wakinga
 
Mimi Gussie nimezaliwa kaskazini na watu wananijua ni wa huko, Mimi ni Mkinga kamili wa Ikonda. Nimekaa sana Nchini Rwanda pia

Anayesemwa sana na watu Mzee Mwakipande aliyekuwa anatoa utajiri alikuwa mjomba wangu na alikwishafariki zamani, Hivi sasa anayefanya kazi za uganga ni mtoto wa mjomba anaitwa Leonard Mwakipande ndiye alirithishwa kazi

Wanaokwenda huko si matajiri tu kama watu wanavyosimuliwa, Kuna watu wana matatizo tofauti ya magonjwa ya ushirikina

Na sio kila tajiri unayemuona akienda huko amefuata utajiri Wengine wamezaliwa huko na huko ni kwao kama mimi GUSSIE

Kama una swali lolote kuhusu huko kwa Mwakipande niulize nitakujibu kwa kadri mimi ninavyoishi na hao ndugu zangu

Mambo mengi yanayosemwa kuhusu sisi wakinga sio kweli, Na hata hizi habari za utajiri kuwa Binamu yangu Leonard Mwakipande anatoa utajiri sio kweli

Kaburi la mjomba ni kweli hakuzikwa kama kuzikwa bali amewekwa kwenye kitanda chake na amejengewa nyumba ndogo tu, Yeye haozi na aliomba asizikwe

Maisha ya huko kwetu kwa sasa yamebadilika sana, Zamani tulitembea kwa miguu toka Ikonda mpaka huko, Leo kuna pikipiki za kutosha

Kuhusu Mimi Gussie kupenda siasa na kufanya kama kitu cha ziada ilitokana na sababu zifuatazo:

Mosi, Wakati huo wazazi wangu wanafanya biashara wao hawakusoma sana na hii ni kwa wakinga wengi wenye biashara hapo kariakoo, Wazazi waliamua kukata shauri na kutupeleka shule watoto ili tujue kuwa wahasibu wao na washauri. Mawazo yao hayo sasa yamefanya wakinga wafanye biashara za kisasa kwa kuzingatia sheria za nchi na kutokulalamika

Kwa kuwa wazazi wetu wengi wa kikinga walikuwa na pesa lakini elimu ndogo kila wakati waliona mambo ya kodi na sheria zinawaonea, Lakini sasa wakinga baada ya sisi watoto kwenda shule mambo yamebadilika na tunashauri wazazi vizuri

Kupitia haya mambo ya kwenda TRA na kurudi, Kuhudhuria vikao vya biashara na wanasiasa yakanifanya na Mimi kwanini nisiingie huko ili kupenyeza agenda zetu wakinga

Pili, Niliumia kuona wakinga ambao wapo kwenye siasa na Wakututetea ni wachache sana, Hata Darasani watu kutoka ukinga tulikuwa kidogo sana, Leo hii hapo Udsm sisi wakinga tuna hata mkufunzi Mkinga haikuwa jambo rahisi

Mwisho sisi ni wamoja na wala huwezi sikia tunagombana ingawa tunagombana lakini mambo yetu tunayamaliza kindugu, Hatuna wivu wala chuki sisi na mtu

Nakaribisha maswali kuhusu wakinga, Uliza nitakujibu

Mpaka Leo Mimi nikisikia Mkinga mwezangu amenunua Gari jipya nitajitahidi ninunue kama gari lake, Wakinga tunaigana sana mambo yetu, Ukifika Njombe pale utashangaa unaweza kuta magari yote ya aina moja

Msitucheke wakinga na mambo yetu ya kuigana kwenye kununua vitu

Any Question? , I 'm here to reply about Kinga' s
Mkinga mpe pesaa
 
Back
Top Bottom