ANKO JEI
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 1,302
- 2,462
Mkuu nimekuelewa sana,mimi nimekaa sana Makambako so naelewa wakinga walivyo na nidhamu ya pesa ila leo umenifungua namna wanavyofanya.Kuhusu Saving au akiba
Huwezi kuwa na nidhamu ya akiba kama huna lengo
Kwa wakinga linaanza kwanza neno Lengo baadae inafuata akiba
Ukiweka akiba bila lengo lazima utaitumia hiyo akiba yako
Mfano:Mwaka 2023 nataka niwe na Vanguard new Model hii ndio lengo langu kuu
Natafuta bei ya Vanguard sokoni kwa sasa ni kiasi gani?
Nagawa Bei ya Vanguard na idadi ya miezi au week ili nijue yanipasa kuweka kiasi gani?
Kama nikiona hata nikijibana bado bei ya Vanguard sitaifikia naweza badili aina ya gari kabisa?
Nikiona lengo hilo halifai naachana nalo kabisa
Kuweka lengo ni kazi kuliko akiba, Wengi wana pesa wanayoita ndogo lakini hawajui wafanye kitu gani
Tatizo sio akiba, Tatizo kubwa ni malengo
Lengo moja ukiona haiwezekani weka lengo jingine hii ndio principal yetu sisi wakinga
Nakupa mfano wangu binafsi ambao nimemuambia mtoto wangu juzi anayetaka kuoa
Nimemuuliza una lengo gani mwakani akaniambia anataka kuoa, Nikamuuliza Pesa utatoa wapi zako au za kuchangiwa akanijibu za kwake
Alianza kuweka laki Saba tangu January mwaka huu Kwa ajili ya harusi mpaka sasa muda huu ana Milioni sita na laki tatu 6,300,000. kufika mwakani mpaka mwezi anataka kuoa atakuwa na Milioni zaidi ya tisa za kwake binafsi sio za kuchangiwa
Ofcoz wakinga mnaushirikiano sana aisee,dogo anaweza toka bulongwa akaja mjini kwenye duka la kaka,akifanya kazi akapata uzoefu kaka anammegea dogo hata M30 (kulingana na ukubwa wa biashara) dogo nae anaenda kuanzisha himaya yake anamvuta dogo mwingine toka bush,kwa hilo hongereni sana.
Ukienda makambako sahivi wakinga wamenunua subaru forester kwa kasi balaa,wanaigana kwa mambo ya maendeleo.
Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app