Ni wapi naweza kupata Kiwanja cha chini ya milioni 4 kwa Dar es Salaam?

Ni wapi naweza kupata Kiwanja cha chini ya milioni 4 kwa Dar es Salaam?

Au aende mbele ya Kigamboni kunaitwa Buyuni na vimepimwa. Kwa bei hiyo atapata kizuri tu..

By the way, kuna watu huwa wanadanganyana sehemu kama Mbagala etiunaweza pata eneo zuri kwa bei rahisi...
Sasa Buyuni sindio yale yale tu! Unakuta eneo lilipo na city centre kama kariakoo,mnazi ama posta distance yake ni 25KM+ yani ni lazima pawe mbali tu!

Kuhusu mbagala eneo kupata hawezi! Bei ni kubwa yani na maeneo hakuna tena!
 
Kuwa na subra hata kimara huko ndani unapata. Hii mentality ya kwamba Dar ni expensive kote sio sawa.
Kimara ipi utakayouziwa eneo 4m? We una masihara kweli mtu labda akuuzie eneo lenye vichuguu 😅 na milima na mabonde ambalo limemshinda!

Kibamba yenyewe tu labda umuotee kapuku amefeli ada za watoto au anauguza. Yani kimsingi asipompata mtu mwenye shida na hio hela direct atapata eneo ila lazma liwe interior kichizi na mbali ambako watu hawapataki!
 
Kigamboni mji mwema patakufaa zaidi, 20 kwa 20 unapata na ni karibu na mjini bora adha ya kuvuka pantoni kuliko kwenda kujenga Chanika utajuta.

Ukishamalizana na matapeli wote ukiwa upo tayari kununuwa kiwanja nicheck nitakukabidhi kwa mwenyekiti wa mtaa unamaliza shida yako.

Hakuna mjanja yoyote anayekaa mbali na city center, viwanja vipo tatizo wabongo ujuwaji mwingi.
Asee kulipa 4,000 ili nikalale kwangu kila siku hio biashara itanishinda 😅! Ni sawa na Minimum ya 120,000 kila mwezi ambayo inanikera tu kwa roho!
 
Kiluvya ipi hiyo unayotumia dk 30 kwenda Posta?

Hivi unapajua Kiluvya au unatype type tu?
Kibaha posta ni dk 30/40 na Barabara Bado ilikuwa haijafunguliwa yote.. ujenzi ulikuwa unaendelea. Kiluvya posta 30 minutes muda ambao sio rush hour ni sawa kabisa
 
Back
Top Bottom