Ni wapi naweza kupata Kiwanja cha chini ya milioni 4 kwa Dar es Salaam?

Ni wapi naweza kupata Kiwanja cha chini ya milioni 4 kwa Dar es Salaam?

Ahaa kumbe Kibugumo. Hapo Sawa.
Kibugumo ipo mji mwema au iko wapi? Maana hata Dege hufiki.

Kuliko mtu kwenda kununuwa chanika au mbande, ni matumizi mazuri ya akili kununuwa Kibugumo si mbali na mjini na si mbali na beach za kigamboni.

Binadamu wote Mungu katupa akili lakini issue inakuja kwenye matumizi mazuri ya akili tu.
 
Habari Wana JF,

Natafuta Kiwanja Dar es salaam Cha bei poa Chini ya Mil 4

Vigezo;
  • Eneo liwe lina upatikanaji wa maji na umeme
  • Pasiwe mbali sana na Mji(Ndani ya dar es salaam)
  • Eneo la kutosha vyuma ya vyumba 3 na choo 2.

Kigamboni mwongozo unapata
Kigambon mwela unapata
Kigamboni kibugumo
0689733183 nipigie
 
Kuna maeneo ya Kisemvule nayafahamu unapata kiwanja tena kikubwa tu kizuri hakipo bondeni na kimepimwa. Pi pameendelea maji umeme na daladala zipo.

Ila ndani ya Dar es Salaam mmmmmh ni ngumu sana.

Naishi Dar ila kwa maeneo nayoishi mm bila Mil 15 na kuendelea wala usifikirie kuhusu kiwanja

Karibu
Kisemvule siyo Dar
 
Kama bajeti yako ni Mil.4 hakikisha unatenga at least laki 2-3 kwajili ya uhakiki. Pwani ni yakitapeli mno.. hasa hivi viwanja vya miguu kwa miguu.

Watu hawana huruma ma imekuwa biashara kubwa nhawajifichi tena. Unajikuta umemlipa tapeli, mtu alitapeliwa kwenye maeneo yenye upimaji na Umiliki. Kuwa makini sana.
 
Kigamboni mji mwema patakufaa zaidi, 20 kwa 20 unapata na ni karibu na mjini bora adha ya kuvuka pantoni kuliko kwenda kujenga Chanika utajuta.

Ukishamalizana na matapeli wote ukiwa upo tayari kununuwa kiwanja nicheck nitakukabidhi kwa mwenyekiti wa mtaa unamaliza shida yako.

Hakuna mjanja yoyote anayekaa mbali na city center, viwanja vipo tatizo wabongo ujuwaji mwingi.

Kuliko kujenga chanika bora ukajenge mkoani kabisa…
 
Madale ipi boss
Misumi vyote hivo viko sokoni
IMG-20210930-WA0050.jpg
 
Huwezi kupata eneo ndani ya Dar es salaam kwa hela hio mzee! Maeneo yapo Mkuranga kwa hio pesa unapata eneo kubwa tu la kutosha. Hio ni Kilwa road!

Upande wa Bagamoyo road pia yapo maeneo Vikawe ni mbele kidogo ya bunju unapata eneo freshi kubwa tu 20*20 au zaidi!

Morogoro road ni kuanzia mbele ya kibaha hapo. Kama upo tayari tunaweka wese tunaenda kamata eneo chap!
Au aende mbele ya Kigamboni kunaitwa Buyuni na vimepimwa. Kwa bei hiyo atapata kizuri tu..

By the way, kuna watu huwa wanadanganyana sehemu kama Mbagala etiunaweza pata eneo zuri kwa bei rahisi...
 
Habari Wana JF,

Natafuta Kiwanja Dar es salaam Cha bei poa Chini ya Mil 4

Vigezo;
  • Eneo liwe lina upatikanaji wa maji na umeme
  • Pasiwe mbali sana na Mji(Ndani ya dar es salaam)
  • Eneo la kutosha vyuma ya vyumba 3 na choo 2.
Kwa hiyo bei, unachokitafuta utakipata. Usirudi humu kutililia.......
 
Back
Top Bottom