#COVID19 Ni Watanzania gani wanaohitaji chanjo?

#COVID19 Ni Watanzania gani wanaohitaji chanjo?

Jasusi Mbobezi

Senior Member
Joined
May 17, 2020
Posts
195
Reaction score
851
Nimesikia baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali wakisema kuwa Watanzania wanasubiri chanjo ili nao waungane na dunia katika mapambano dhidi ya Corona, Leo ningependa kujua hao Watanzania wanaohitaji chanjo wanapatikana wapi?

Maana ukweli ni kuwa majority wameonesha kutotaka chanjo, au sikuhizi mambo yanakwenda kinyume?

Viongozi wetu mkikosea kwenye hili mtakuja kujuta sana, huu uzi utakuwa shahidi siku hizo.
 
Askari wetu walio mstari wa mbele kutupatia HUDUMA ZA AFYA;

1) Manesi(nurses)

2) Madaktari (Doctors)

3) Wataalam wa maabara

4) Wataalam wa mionzi ,mashine za hospitali

5) Makatibu wa hospitali

6) Wahasibu wa hospitali

7) Watoa ushauri nasaha

8) Wataalamu wa viungo cheza

9) Wafamasia

10) Wahifadhi maiti

11) Wahudumu (nurses attendants)

12) Wahudumu wa usafi hospitalini

13) Wafanyakazi wa BANK za malipo zilizopo ndani ya Hospitali

14) Walinzi wakiwemo maaskari wa SUMA JKT/magrupu ya Ulinzi

WOTE HAWA NI LAZIMA WACHANJWE..

Upande wetu RAIA ,mathalani binafsi nitakuwa wa mwanzomwanzo kuitikia wito wa KUCHANJWA CHANJO HIYO DHIDI YA CORONA.

Hapa nimeshaanza kuliandaa bega langu kwa ajili ya hizo SINDANO....💪

#TuchanjweNduguZangu
#TuwalindeWengine
#NchiKwanza
#ChanjoNiMuhimu
#KaziIendelee
 
Nimesikia baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali wakisema kuwa Watanzania wanasubiri chanjo ili nao waungane na dunia katika mapambano dhidi ya Corona, Leo ningependa kujua hao Watanzania wanaohitaji chanjo wanapatikana wapi?...
Usitusemee..mimi na mke wangu tunahitaji chanjo. Wewe ambae hauna hata ramani ya kwenda huko duniani kaa chini kwa kutulia..wewe ambae haujawahi kupoteza mtu wala kuumwa corona kaa kimya ila ambao tunahitaji chanjo tupo
 
Nimesikia baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali wakisema kuwa Watanzania wanasubiri chanjo ili nao waungane na dunia katika mapambano dhidi ya Corona, Leo ningependa kujua hao Watanzania wanaohitaji chanjo wanapatikana wapi?..
Mkuu umesahau unafiki wa wanasihasa wa danganyika....hapo wameshanusa dili la pesa ya mabeberu.
 
Usitusemee..mimi na mke wangu tunahitaji chanjo. Wewe ambae hauna hata ramani ya kwenda huko duniani kaa chini kwa kutulia..wewe ambae haujawahi kupoteza mtu wala kuumwa corona kaa kimya ila ambao tunahitaji chanjo tupo
Pole sana mkuu kwa kufiwa na baba yako na mama yako kwa CORONA, kweli nimeamini inabidi wakudunge na nyingine unywe.
 
Si lazima lakini
IMG-20210714-WA0017.jpg
 
WOTE HAWA NI LAZIMA WACHANJWE, kumbe ishakuwa lazima.
Ninapendekeza hilo.

Nchi za wenzetu hakuna hiyari kwa hao watoa huduma mahospitalini.

HEBU TUFIKIRIE:
Mtaalamu wetu wa HOSPITALI anarudi nyumbani kwa mumewe/mkewe na wanawe...hajachanjwa, anaupeleka ugonjwa nyumbani kwa wapendwa wake....tusisahau wao ndio rahisi mno kuambukizwa "DOZI KUBWA" kuliko wengine.

#ChanjoIweLazimaKwaWataalamWaAfya
#MieMlalahoiNinaisubiriKwaHamuHiyoChanjo
 
Ninapendekeza hilo.....

Nchi za wenzetu hakuna hiyari kwa hao watoa huduma mahospitalini.....

HEBU TUFIKIRIE:

Mtaalamu wetu wa HOSPITALI anarudi nyumbani kwa mumewe/mkewe na wanawe...hajachanjwa....anaupeleka ugonjwa nyumbani kwa wapendwa wake....tusisahau wao ndio rahisi mno kuambukizwa "DOZI KUBWA" kuliko wengine....

#ChanjoIweLazimaKwaWataalamWaAfya
#MieMlalahoiNinaisubiriKwaHamuHiyoChanjo
Ndo maana nikauliza chanjo ishakuwa lazima? au hayo makundi hayatakiwi kujaza consent form kushiriki kwenye majaribio ya chanjo.....wao ni piga, ua, garagaza, ozesha, fukia lazima kuchanja......sasa hapo inakuwa ni kulazimisha, huwezi kuita 'consent'
 
Hapana mkuu....

Haijawa lazima kaka....

Nimependekeza tu kama mlalahoi huku mitaani mkuu wangu !
 
Mkuu wangu ugonjwa upo....

Tunao ndugu zetu tena ni vijana tu wako katika mashine za "OKSIJENI" kwa ajili ya huo UGONJWA....

Mkuu kama halijakufika shukuru M/ Mungu tu......
Hiyo chanjo haiondoi ugonjwa, maana siyo tiba....
 
Usitusemee..mimi na mke wangu tunahitaji chanjo. Wewe ambae hauna hata ramani ya kwenda huko duniani kaa chini kwa kutulia..wewe ambae haujawahi kupoteza mtu wala kuumwa corona kaa kimya ila ambao tunahitaji chanjo tupo
Hakika mkuu....

Pole sana Kaka....

Pole ndugu yangu....

Tuchanjwe tu....naisubiri kwa hamu hiyo CHANJO!!!
 
Back
Top Bottom