Nimesikia baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali wakisema kuwa Watanzania wanasubiri chanjo ili nao waungane na dunia katika mapambano dhidi ya Corona, Leo ningependa kujua hao Watanzania wanaohitaji chanjo wanapatikana wapi?
Maana ukweli ni kuwa majority wameonesha kutotaka chanjo, au sikuhizi mambo yanakwenda kinyume?
Viongozi wetu mkikosea kwenye hili mtakuja kujuta sana, huu uzi utakuwa shahidi siku hizo.
Hii inaonyesha nchi yetu bado ni masikini. Hata sehemu ambazo chanjo ni bure Mfano USA majimbo masikini kuliko yote ndiyo wamepiga chanjo wachache maana elimu ni ndogo kwa watu. Masikini ndiyo wakwanza kuamini uvumi na uongo na hawaamini sayansi. Hiki ni kipimo kizuri kujua mtu au watu wako kundi lipi. Na kama unasema hamna watu unathibitisha kabisa umezungukwa na hao walala hoi. Kule Uninio najua mimi wazee karibu wote wanasubiri chanjo! kuna watu kibao wengine mpaka waandishi wa habari na wanasiasa wanaenda nje kupata chanjo