Hivi kuamini sayansi ni kupi ni kukubali kila unachoambiwa ilimradi kimehuaiahwa na sayansi au ni vp? maana sielewi hii kauli, hao unaosema hawaamini sayansi ndio hao hao wanatibiwa hospitali endapo wakiumwa na hospitali wanatumia sayansi. Wengine wanadharau matunda na kuita uganga wa kienyeji ila jawajui kuwa sayansi hiyo hiyo ndio inatuambia faida zilizopo kwenye hayo matunda(kama malimao vitunguu tangawizi) na madhara yake, ila mtu anaona kula hayo matunda ni kinyume na sayansi na ni sawa na matunguri.
Wengine humu unakuta hata matumizi sahihi ya barakoa hayajui ila nae anavaa tu na kupoga kelele humu ili tu asionekane mjinga asiyeelimika kama sie wengine, hata hawa wanaotaka chanjo si kwamba wanauelewa wengine hawana uelewa wotewote ni kufuata mkumbo tu nae aonekane anaamini sayansi.