#COVID19 Ni Watanzania gani wanaohitaji chanjo?

#COVID19 Ni Watanzania gani wanaohitaji chanjo?

Vibaraka ndo mtachoma, wazalendo tulisha malizana na corona kitambo sana.
Mkuu bado tu unatumia lugha hizo ?!! 🤣

Kibaraka kwenye ugonjwa ?!! 😲

Mkuu muda huu utakuwa huna ndugu/jamaa/rafiki/jirani aliyeko katika mashine ya oksijeni....

Mkuu ama unakumbatia CONSPIRACY THEORIES?!!🤣
 
Hiyo ya majority kutotaka chanjo, huo utafiti ulifanyia wapi? Mimi binafsi sina shida na chanjo. Sijawahi kukosa chanjo yoyote, nina sababu gani ya kuikataa hii ya sasa?

Kazini pangu, kila mmoja anazungumzia kuwa tayari kuchanjwa, sidhani kama yupo hata mmoja ambaye hataki.

Kwanza chanjo haziwezi kutosha kwa watu wote, itakuwa kwa awamu. Kama watakuwepo wasiotaka itakuwa ahueni kwa tunaotaka na kwa Serikali. Hao wasiotaka watakuja kupewa mwishoni kabisa, ikiwezekana hata mwakani, kwa wale ambao watakuwa hai.
Awesome 👊👍👍
 
Mkuu una uhakika gani wa kisayansi kuwa CHANJO itakuwa "failure" mwilini mwangu ?🤣
Wewe mboga saba hata bila chanjo unaweza ku survive, nilikuwa naongelea hao unaoema pasi ndefu wa kwa mtogole..
 
Napata mashaka sana na namna unavyotafsiri neno uzalendo, i respect uour opinion though
Neno "uzalendo" "mzalendo" limekuwa rahisi sana....rahisi sana kutolewa mdomoni na maandishini na yeyote dhidi ya yeyote....kiufupi limekuwa likitumiwa KUFURAHISHA NAFSI ZA WANAOLITOA/TAMKA....
 
Wewe mboga saba hata bila chanjo unaweza ku survive, nilikuwa naongelea hao unaoema pasi ndefu wa kwa mtogole..
Mkuu mimi si wa mboga 7 mapokopoko manjari draft....

Ninawaongelea kwa kuwawakilisha wenzangu ninaosebenza nao kitaa....
 
Usiwasemee watu, subiri chanjo zifike halafu tutashuhudia kwa macho na tutajua uhalisia wa mioyo ya watanzania. Ni mapema sana kuanza kusema chochote kuhusuuhitaji wa hii chanjo ila ninachojua watu wengi watachoma chanjo, ni suala la muda tu
👍
 
Askari wetu walio mstari wa mbele kutupatia HUDUMA ZA AFYA;

1) Manesi(nurses)

2) Madaktari (Doctors)

3) Wataalam wa maabara

4) Wataalam wa mionzi ,mashine za hospitali

5) Makatibu wa hospitali

6) Wahasibu wa hospitali

7) Watoa ushauri nasaha

8) Wataalamu wa viungo cheza

9) Wafamasia

10) Wahifadhi maiti

11) Wahudumu (nurses attendants)

12) Wahudumu wa usafi hospitalini

13) Wafanyakazi wa BANK za malipo zilizopo ndani ya Hospitali

14) Walinzi wakiwemo maaskari wa SUMA JKT/magrupu ya Ulinzi

WOTE HAWA NI LAZIMA WACHANJWE..

Upande wetu RAIA ,mathalani binafsi nitakuwa wa mwanzomwanzo kuitikia wito wa KUCHANJWA CHANJO HIYO DHIDI YA CORONA.

Hapa nimeshaanza kuliandaa bega langu kwa ajili ya hizo SINDANO....💪

#TuchanjweNduguZangu
#TuwalindeWengine
#NchiKwanza
#ChanjoNiMuhimu
#KaziIendelee

Mimi, familia yangu na ndugu na jamaa zetu wa karibu tuko kama mtu 20 kama wave 3 itatunusuru hadi chanjo kufika tutakuwa batch ya mwanzo kabisa.
 
Hii inaonyesha nchi yetu bado ni masikini. Hata sehemu ambazo chanjo ni bure Mfano USA majimbo masikini kuliko yote ndiyo wamepiga chanjo wachache maana elimu ni ndogo kwa watu. Masikini ndiyo wakwanza kuamini uvumi na uongo na hawaamini sayansi. Hiki ni kipimo kizuri kujua mtu au watu wako kundi lipi. Na kama unasema hamna watu unathibitisha kabisa umezungukwa na hao walala hoi. Kule Uninio najua mimi wazee karibu wote wanasubiri chanjo! kuna watu kibao wengine mpaka waandishi wa habari na wanasiasa wanaenda nje kupata chanjo
Hivi kuamini sayansi ni kupi ni kukubali kila unachoambiwa ilimradi kimehuaiahwa na sayansi au ni vp? maana sielewi hii kauli, hao unaosema hawaamini sayansi ndio hao hao wanatibiwa hospitali endapo wakiumwa na hospitali wanatumia sayansi. Wengine wanadharau matunda na kuita uganga wa kienyeji ila jawajui kuwa sayansi hiyo hiyo ndio inatuambia faida zilizopo kwenye hayo matunda(kama malimao vitunguu tangawizi) na madhara yake, ila mtu anaona kula hayo matunda ni kinyume na sayansi na ni sawa na matunguri.

Wengine humu unakuta hata matumizi sahihi ya barakoa hayajui ila nae anavaa tu na kupoga kelele humu ili tu asionekane mjinga asiyeelimika kama sie wengine, hata hawa wanaotaka chanjo si kwamba wanauelewa wengine hawana uelewa wotewote ni kufuata mkumbo tu nae aonekane anaamini sayansi.
 
Nimesikia baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali wakisema kuwa Watanzania wanasubiri chanjo ili nao waungane na dunia katika mapambano dhidi ya Corona, Leo ningependa kujua hao Watanzania wanaohitaji chanjo wanapatikana wapi?

Maana ukweli ni kuwa majority wameonesha kutotaka chanjo, au sikuhizi mambo yanakwenda kinyume?

Viongozi wetu mkikosea kwenye hili mtakuja kujuta sana, huu uzi utakuwa shahidi siku hizo.
IMG_20210714_221408_881.jpg
 
Elimu ya huu ugonjwa bongo imerubuniwa sana, wengi wanaamini kuwa wana taarifa kamili lakini wakifungua kimywa utashangaa na ukimuuliza umepata wapi hizo taarifa mara nyingi jibu ni "nimeambiwa na furani"au "nimeskia",hapo bado hawajaongezea mambo ya 'new world order',yaani wengi hawana taarifa kutoka kwa wataalamu wa afya,yaani wenye fani za utabibu.
Ni vizuri chanjo zitatolewa kwa hiyari sio lazima,lakini kumbukeni watanzania asilimia kubwa washapata hizi chanjo,hasa wanaoishi nje na baadhi bongo.asilimia kubwa nchi nyingi ulimwenguni zimechanya,ivo watz mna mamillioni ya data ambazo mnaweza kutumia kama ushahidi kufuatilia mwenendo wa chanjo.Chanjo yoyote itakayoletwa bongo,tayari ishatumika kwa mamilioni ya binadamu wengine,tena wa kila rangi.
We are not that special,tuseme chanjo zisaidie wengine sisi zitudhuru! Inabidi tufikirie vizuri.
 
Kuna watu wengi wanapata infection bila kuonyesha dalili, lakini hawajachoma hizo takataka...
Kwani kung'atwa na mbu ndio kupata ugonjwa wa malaria?!!

Mkuu wangu unadhani sote tuna KINGA madhubuti dhidi ya magonjwa ya milipuko ?!!

Kwa hizi chumi zetu za kupitisha mchana kwa pasi ndefu...kahawa vikombe 3 na kashata ili vitoto vyetu viende SKONGA.....

Kwa hizi tamaduni zetu huku uswazi ambako mboga za majani na matunda ni mwiko na anasa ?!!

Mkuu ni bora tu tuchanjwe halafu ukija kutuchapa basi hatua stahiki zitakuwa zimeshachukuliwa.....
Usiwasemee watu, subiri chanjo zifike halafu tutashuhudia kwa macho na tutajua uhalisia wa mioyo ya watanzania. Ni mapema sana kuanza kusema chochote kuhusuuhitaji wa hii chanjo ila ninachojua watu wengi watachoma chanjo, ni suala la muda tu
mbn naww umewasemea watu
 
Hiyo ya majority kutotaka chanjo, huo utafiti ulifanyia wapi? Mimi binafsi sina shida na chanjo. Sijawahi kukosa chanjo yoyote, nina sababu gani ya kuikataa hii ya sasa?

Kazini pangu, kila mmoja anazungumzia kuwa tayari kuchanjwa, sidhani kama yupo hata mmoja ambaye hataki.

Kwanza chanjo haziwezi kutosha kwa watu wote, itakuwa kwa awamu. Kama watakuwepo wasiotaka itakuwa ahueni kwa tunaotaka na kwa Serikali. Hao wasiotaka watakuja kupewa mwishoni kabisa, ikiwezekana hata mwakani, kwa wale ambao watakuwa hai.
hata ww unaweza ukafa vile vile
 
Vibaraka ndo mtachoma, wazalendo tulisha malizana na corona kitambo sana.
Taifa linahitaji raia wenye afya njema, kukubali kuchanjwa ni tendo la kizalendo ingawa hulazimishwi.
Mi binafsi sikubali mtu anipangie cha kufanya.
Chanjo na ije nichanjwe.
 
Back
Top Bottom