#COVID19 Ni Watanzania gani wanaohitaji chanjo?

Naunga mkono hoja....

Nami pia kaka!

Bwana Jumbe Brown waonaje mgawanyo huu?



Labda niongezee, kwa walio wazalendo wana mtazamo kama huu:

 
Mleta mada ni msabato. Hapo inategemea kama kanisa lake litamruhusu, likikataa ataipinga chanjo mpaka mwisho.

Mambo ya Ellen G. White hayo
 
Mkuu wangu.....

Kuhusu janga la CORONA....

Niko wazi....binafsi ninahitaji CHANJO...

Hapa hakuna "SIASA" wala "HISIA ZISIZO ZA KISAYANSI"......

Nichomwe mimi hiyo chanjo...na tuchomwe watanzania ili tupambane na hilo gonjwa "KIWELEDI".......

************************

Kuhusu KATIBA MPYA......

Binafsi siungi mkono katiba mpya....sikumuunga mkono mzee Warioba.....si kwa kuwa moyoni mwangu hakuna "UZALENDO"....laa hashaa......

Matatizo yetu watanzania yako zaidi ya KATIBA.....

Katiba mpya si suluhisho.....huko AFRIKA YA KUSINI wana katiba inayoweza kumfunga RAIS WA NCHI...bado haijawazuia RAIA WAKE kuona USAWA baina ya walio nacho na makabwela.......

Binafsi ninaheshimu msimamo wa serikali 2 za JMT....Baba wa taifa JKN aliona mbali sana kutuepushia "mabalaa" ya wanasiasa.......mfanowe wale "G55".......

Hayo ni kwa ufupi mkuu wangu🙏
 
Umelazimishwa wewe mpuuzi na wakati umeambiwa chanjo ni hiari?
 
Usitusemee..mimi na mke wangu tunahitaji chanjo. Wewe ambae hauna hata ramani ya kwenda huko duniani kaa chini kwa kutulia..wewe ambae haujawahi kupoteza mtu wala kuumwa corona kaa kimya ila ambao tunahitaji chanjo tupo
Mzee wa sweken huyo
 
Mleta mada ni msabato. Hapo inategemea kama kanisa lake litamruhusu, likikataa ataipinga chanjo mpaka mwisho.

Mambo ya Ellen G. White hayo
Duuuh kwa hiyo CHANJO dhidi ya magonjwa inapelekwa "kiimani" 😲

Ha ha ha ha baadhi ya waafrika sisi...🤣

Baadhi yetu tunashindwa kuweka mizania ya imani ya maisha ya hapa duniani na maisha "yajayo".....

#ChanjoIjeTuchomwe
 
Sawa mkuu....

Nitatoka huku kwa Mkunduge kuja kuisaini hiyo fomu mkuu wangu....

Niko radhi na tayari kusaini mkuu wangu....masela wangu Zwande ,Bozu ,Ally Meza na Philimon Chenje nao wamekubali kuchomwa hizo chanjo....nitakuja nao mkuu wangu!!
Hiyo fomu mimi nilisaini na nimechanja dozi zote 2, na nipo poaa kabisa! Hawa wafuasi wa kinjeketile wasikutishe
 
Duuuh kwa hiyo CHANJO dhidi ya magonjwa inapelekwa "kiimani" 😲

Ha ha ha ha baadhi ya waafrika sisi...🤣

Baadhi yetu tunashindwa kuweka mizania ya imani ya maisha ya hapa duniani na maisha "yajayo".....

#ChanjoIjeTuchomwe
Sasa hivi mleta mada yuko kwenye makambi huko ya Kisabasato, wanaambizana Chanjo ya Corona ndio alama ya mnyama a.ka 666 🤣🤣
 
Sasa hivi mleta mada yuko kwenye makambi huko, wanaambizana Chanjo ya Corona ndio alama ya mnyama a.ka 666 🤣🤣
Daah unajua inasikitisha sana....jamii inaweza kutumia misimamo ya kiimani ya makundi na kujipotosha na kupotosha wengine....daaah

Tuna wajibu mzito wa kufundisha watoto "kufikiri vyema" kwa kila wanachoona/kusikia/wanachoambiwa/kufundishwa)/kukaririshwa.
 

Ninaujua msimamo wako ila kwa mchanganuo ule unakutambua wewe kama wa mama.

Si kosa kuwa wa mama au wa baba.

Niliomba uthibitisho wako tu mkuu ikikupendeza lakini.
 
Ninaujua msimamo wako ila kwa mchanganuo ule unakutambua wewe kama wa mama.

Si kosa kuwa wa mama au wa baba.

Niliomba uthibitisho wako tu mkuu ikikupendeza lakini.
🤣🤣

Mimi ni wa BABA....(Hapa kazi tu)

Mimi ni wa MAMA...(Kazi Inaendelea)

Kama Raia kila siku inabidi tuwe bora zaidi ya "Jana"....

Mh.SSH ndiye kiongozi mkuu wa taifa letu pendwa ,kumuunga mkono ni wajibu wetu wa kila mmoja ukiacha baadhi ya wale wenye "mbango"....ni "mbango tu" mkuu....MBANGO TU 🤣

#KaziInaendelea
#ChanjoIjeTu
 
Hata hizo chanjo za watoto wakati zinaanza watu walizikimbia hv hv lakini sikuhizi zikikosekana kwenye vituo vya afya wazazi wanaandamana mpk kwa mkuu wa wilaya. Kwahiyo siyo Jambo geni kwa mnaorukaruka km mahindi ya kukaangwa. Hv km n wazungu kutuangamiza siwangetumia hizo chanjo za watoto ambazo hatuzihofii? Kwann hii moja imekuwa nongwa sana. Kwan taasisi zetu hazina uwezo wa kujua hizo chanjo ni salama au sio salama?
 
Mbona saizi hawaupeleki?
 
Hapo sasa 🤣🤣

Ni Kama zile za "mabusha na matende".....waliongea kuwa ZINAKUJA KUPUNGUZA NGUVU ZA KIUME NA KIZAZI....🤣
 
Wote hawa ni lazima wachanjwe Kumbe ishakuwa lazima.
Tafuta asilimia ya kifo kwa korona na asilimia ya kifo kwa chanjo. Ukipata jibu utaamua mwenyewe cha kufanya hakuna wa kukulazimisha maana kuna fomu ya kujaza.
 
Kama ni hivyo basi inamaana hao wote na familia zao wadungwe sindano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…