#COVID19 Ni Watanzania gani wanaohitaji chanjo?

itakuwa ndo chanjo ya maisha au wanazi update kila baada ya muda flani kama software
Chanjo ya maisha dhidi ya hiyo CORONA....zitakuwa ni zaidi ya moja kama chanjo nyinginezo tu.....

Mbona tunachomwa chanjo 5 kwa ajili ya kuzuia PEPOPUNDA?!!!
 

Kuna tofauti kubwa baina ya kumwunga mkono mtu na kuwa chawa wake. Ninamwuunga mkono mama, lakini siyo chawa wake.

Unaona chawa wa baba na Corona? Unadhani hawaelewi hatari yake? Unaona chawa wa mama na katiba? Unadhani hawauoni umuhimu wake?

Sioni andiko bora kabisa kuhusu vyawa kuliko hili:



Au nasema uongo ndugu zangu?
 

Mtu ambaye hataki chanjo kiukweli sio mwelewa. Mimi naishi US hapa watu 200 Milioni wamepata chanjo mimi nikiwa mojawapo na ndugu zangu wengine zaidi ya kumi wote tuko salama na tuna kinga. Kwasasa wasiwasi wa Watanzania wengi ni wazee wetu ambao wako 70's ni hatari sana kwao kupata Corona. Tunavyosema sayansi kuna wasomi wameshakaa na kuja na report ya kila kitu kuhusu chanjo.

Lakini ukweli ni kwamba kuna uhusiano mkubwa wa umasikini na kuamini chanjo mfano hapa US chanjo ni bure lakini majimbo masikini kuliko yote ndiyo kuna watu wengi ambao ni waoga wamechanja 36% hivi lakini nchi nzima ni karibu 67%. Inaelekea ukiwa na fikra za kimasikini vilevile unakuwa mtu wa kuamini uvumi. Hapa nasema fikra za kimasikini maana leo ukiwa masikini ukaenda kuiba bank na kuwa tajiri kwa wizi bado fikra zako ni za kimasikini.
 
Tafuta asilimia ya kifo kwa korona na asilimia ya kifo kwa chanjo. Ukipata jibu utaamua mwenyewe cha kufanya hakuna wa kukulazimisha maana kuna fomu ya kujaza.
Hiyo ni fomu ya ridhaa kushiriki kwenye majaribio ya chanjo, mnafanywa panya wa majaribio maana hakuna fidia yoyote mnayolipwa na mtafiti hausiki na madhara yatakayojitokeza.......huu ni uzumbukuku...
 
"...WOTE HAWA NI LAZIMA WACHANJWE..."

Huoni kama hujatoa jibu sahihi bado?

By the way, chanjo ni hiari wala siyo hiyo sentence yako
 
Majority ya Health care workers hawako tayari kuchanjwa. Anyway, tutegemee wengi kufoji vyeti vya Chanjo ili tuu waweze kupata vibali vya kufanya kazi na Taasisi za Kimataifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…