Ni wazi Serikali haina mikakati ya tatizo la Ajira kwa vijana

Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Posts
2,319
Reaction score
3,128
Wanasiasa wote ndani ya CCM na upinzani wamekuwa wakilitaja tatizo la ajira lakini kwa hotuba ya leo ya Rais Samia, ni wazi serikali haina ufumbuzi wa tatizo hili. Kujiajili hiyo siyo mbinu ya serikali, ni jambo la mtu binafsi kuamua.

Serikali lazima itengeneze ajira. Kupunguza kodi siyo mbinu ya ajira kwa vijana. Kufuta tozo za OSHA siyo ufumbuzi. Viwanja vya michezo siyo ufumbuzi. Ni kama utatanishi tu na kutaja facts ambazo kila mtu anazijua.

Vijana hawana ajira, serikali itueleze wanategenezaje ajira. Hatutaki kuuza Bar kama tulivyoambiwa enzi za awamu ya 4.
 
Vijana wa nchi hii wenyewe hawajielewi ndio maana wanaishia kutumiwa na wajanja wachache.

Sasa hivi ukishakuwa na kundi la misukule nyuma yako, nenda kaliuze huko CCM wananunua.

Steve Nyerere ana Mama sema na mwanao.

Wasanii washauza mashabiki wao.

Machinga waneshatekwa kwa ujira wa mlo wa siku.

Nahisi joto la vijana wanasiasa wataanza kulionja baada ya miaja 10 mbele.

Wakati huo kila mtu atakuwa hoi bin taaban, haambiliki tena maana serikali haina mkakati wowote.
 
Walishazoea kazi za kutwa buku 10 au 5 na udalali hela ya chapuchapu.

Ni afadhali serikali ingewawezeeha wenye mitaji mikubwa ili wawape masharti ya kuajiri b Jana na kulipa Kodi, kwa sababu wameshindwa kuwaajiri hao vijana.
 
Wanasiasa wote ndani ya CCM na upinzani wamekuwa wakilitaja tatizo la ajira lakini kwa hotuba ya leo ya rais Samia, ni wazi serikali haina ufumbuzi wa tatizo hili. Kujiajili hiyo siyo mbinu ya serikali, ni jambo la mtu binafsi kuamua.

Serikali lazima itengeneze ajira. Kupunguza kodi siyo mbinu ya ajira kwa vijana. Kufuta tozo za OSHA siyo ufumbuzi. Viwanja vya michezo siyo ufumbuzi. Ni kama utatanishi tu na kutaja facts ambazo kila mtu anazijua. Vijana hawana ajira, serikali itueleze wanategenezaje ajira. Hatutakikuuza bar kama tulivyoambiwa enzi za awamu ya 4.
Vijana Suala la AJIRA sahauni Mara Ajira mil.12,10,8,mara Mkeka unakuja ni SIASA
 
Wanasiasa wote ndani ya CCM na upinzani wamekuwa wakilitaja tatizo la ajira lakini kwa hotuba ya leo ya rais Samia, ni wazi serikali haina ufumbuzi wa tatizo hili. Kujiajili hiyo siyo mbinu ya serikali, ni jambo la mtu binafsi kuamua.

Serikali lazima itengeneze ajira. Kupunguza kodi siyo mbinu ya ajira kwa vijana. Kufuta tozo za OSHA siyo ufumbuzi. Viwanja vya michezo siyo ufumbuzi. Ni kama utatanishi tu na kutaja facts ambazo kila mtu anazijua. Vijana hawana ajira, serikali itueleze wanategenezaje ajira. Hatutakikuuza bar kama tulivyoambiwa enzi za awamu ya 4.
Lazima mazingira ya sekta binafsi yaboreshwe tuweze kupata ajira za kutosha
 
Yaani rais anakwenda kuhutubia vijana bila ufumbuzi wa tatizo lao kubwa!
Utata ni mkubwa sana. Wanasema uchumi unakuwa kwa 5% population growth yetu ni 3%, kwa nini uchumi unashindwa kuikamata population hii? Bado viongozi hawa hawaelewi matatizo ya wananchi. Ni rahisi kuweka mabomba ya maji na umeme wa REA, lakini inahitaji akili na mipango mizuri kukuza ajira. Sijui nani ana akili hiyo kwa hawa wanasiasa.
 
Lazima mazingira ya sekta binafsi yaboreshwe tuweze kupata ajira za kutosha
Nionavyo, tatizo la sekta binafsi pia ni gumu kiasi. Niliwaona wakizungumza na JPM ikulu kipindi kile. Badala ya kueleza changamoto za biashara zao, mtu anaomba rais amsaidie kupata shamba analohitaji wilayani Magu, akifahamu ni shamba la wananchi ambao atawaondoa kwenye ajira yao! Mtu anakwenda na matatizo binafsi kabisa!

Serikali nayo ikizunguimza nao inawapa maneno ya kufurahisha tu! Sioni mikakati yao ya kwenda kwenye teknolojia, tuwe na uzalishaji ndani na kuuza nje. Ni watu wa kununua na kuuza ndo maana kila siku ni TRA, TRA, TRA!
 
Ndiyo hii mifumo ya kipumbafu imetufikisha hapa mahali tulipo, tuibadili
 
Wanasiasa wote ndani ya CCM na upinzani wamekuwa wakilitaja tatizo la ajira lakini kwa hotuba ya leo ya rais Samia, ni wazi serikali haina ufumbuzi wa tatizo hili. Kujiajili hiyo siyo mbinu ya serikali, ni jambo la mtu binafsi kuamua.

Serikali lazima itengeneze ajira. Kupunguza kodi siyo mbinu ya ajira kwa vijana. Kufuta tozo za OSHA siyo ufumbuzi. Viwanja vya michezo siyo ufumbuzi. Ni kama utatanishi tu na kutaja facts ambazo kila mtu anazijua. Vijana hawana ajira, serikali itueleze wanategenezaje ajira. Hatutaki kuuza bar kama tulivyoambiwa enzi za awamu ya 4.
Kitendo cha serikali ya CCM kuruhusu machinga kumiliki barabara na maeneo ya wazi ili wapate kura zao hakiwezi kufutwa kwa propaganda.
Machinga ni kaa la moto hawagusiki.
Mama hakupaswa kuwafukuza kazi DC na mwenzake tena hadharani. Amewaongezea kiburi machinga.
Angesema tu nguvu isitumike, lakini kwakuwa vyombo vya Dola ni silaha ya CCM dhidi ya upinzani hawezi kusema hivyo.
This is a systemic corruption, part and parcel of an autocracy.

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Nionavyo, tatizo la sekta binafsi pia ni gumu kiasi. Niliwaona wakizungumza na JPM ikulu kipindi kile. Badala ya kueleza changamoto za biashara zao, mtu anaomba rais amsaidie kupata shamba analohitaji wilayani Magu, akifahamu ni shamba la wananchi ambao atawaondoa kwenye ajira yao! Mtu anakwenda na matatizo binafsi kabisa!

Serikali nayo ikizunguimza nao inawapa maneno ya kufurahisha tu! Sioni mikakati yao ya kwenda kwenye teknolojia, tuwe na uzalishaji ndani na kuuza nje. Ni watu wa kununua na kuuza ndo maana kila siku ni TRA, TRA, TRA!
Uko sahihi sana! Wanaojiita wafanyabiashara, wengi ni kuuza na kununua bidhaa tu! Unapoagiza bidhaa unakwepaje sheria za TRA?

Kuna watu wamesoma nchi hii wanastahili kupewa mitaji ya kimkakati ili watoe ajira. Badala yake tunawapa wanasiasa, akina Mzindakaya (RIP) wasio na uelewa zaidi ya siasa, matokeo wanaishia kuanzisha miradi ya kufikirika tu, eti kiwanda cha nyama! Viwanda vingi walipewa walio karibu na wanasiasa hapa Dar, moro vyote vimekufa tu! Akina Lwakatare wakaharibu viwanda na kuvigeuza shule za boarding. A complete nonsense!
 
Vijana hawana ajira, serikali itueleze wanategenezaje ajira. Hatutaki kuuza Bar kama tulivyoambiwa enzi za awamu ya 4.
Bora hata kama hizo Bar kama zipo zitasaidia..., tunakoelekea Bar hazipo, vijana wakiamua kulima masoko ya kubahatisha..., yaani unataka mtu alime akishavuna aanze kuingia sokoni kutafuta madalali by the time ametapeliwa na kulipwa robo ya pesa zake msimu wa kulima umeshamuacha... (kinachobaki ni madeni na stress)

By the way wazee wa fursa wekezeni kwenye ushauri wa magonjwa ya akili na kuchanganyikiwa..., potentially naona wengi watakumbwa na hili tatizo.... (ila angalizo..., watakuwa hawana pesa za kuwalipa)
 
Wanasiasa wote ndani ya CCM na upinzani wamekuwa wakilitaja tatizo la ajira lakini kwa hotuba ya leo ya Rais Samia, ni wazi serikali haina ufumbuzi wa tatizo hili. Kujiajili hiyo siyo mbinu ya serikali, ni jambo la mtu binafsi kuamua.

Serikali lazima itengeneze ajira. Kupunguza kodi siyo mbinu ya ajira kwa vijana. Kufuta tozo za OSHA siyo ufumbuzi. Viwanja vya michezo siyo ufumbuzi. Ni kama utatanishi tu na kutaja facts ambazo kila mtu anazijua.

Vijana hawana ajira, serikali itueleze wanategenezaje ajira. Hatutaki kuuza Bar kama tulivyoambiwa enzi za awamu ya 4.
Mtoa mada elewa sio wajibu wa serikali kutoa ajira ,wajibu wake ni kutengeneza mazingira ya watu kujiajili au private sector's kurahisishiwa mazingira ya kuendesha shughuli zao na hii inaleta ajira,na elewa PresidentSamia ametoa ombi kuwa laumu na pia toa mawazo ya to remedy the situations sasa wewe unafanya kinyume,lawama lawama tu bila ya kushauri the better way forward,amka wewe middle class wa kitanzania acha kuwa kama mtoto anayehitaji kulishwa.
 
Kijana makini na anaye jitambua hawezi sikiliza maneno ya Wanasiasa katika kuamua hatima ya maisha yake
Nchi Taifa inabidi kutengeneza Sera za Majority na sio Individuals..., wangapi wanajitambua (hata kama ni wengi) wangapi wana discipline ?

Kuna watu wapo exceptional hata ukiwapeleka Syria au Somalia kwenye vita wao wataperform tu...., Ila realistically kwenye miti wajenzi sio wote waliopo pale..., bali wachache (kwahio watengeneza Sera wetu wahakikishe hii Keki ambayo kwa Tanzania ni kubwa sana inawafikia majority) sisemi watu wote wawe matajri (that's a pipe dream) bali tuwe na middle income wengi na sio tunakuoelekea kwenye walionacho wachache na wasionacho wengi (its going to be hell)...
 
Mtoa mada elewa sio wajibu wa serikali kutoa ajira ,wajibu wake ni kutengeneza mazingira ya watu kujiajili au private sector's kurahisishiwa mazingira ya kuendesha shughuli zao na hii inaleta ajira,na elewa PresidentSamia ametoa ombi kuwa laumu na pia toa mawazo ya to remedy the situations sasa wewe unafanya kinyume,lawama lawama tu bila ya kushauri the better way forward,amka wewe middle class wa kitanzania acha kuwa kama mtoto anayehitaji kulishwa.
Kila Serikali inaendeshwa tofauti na Capitalists Government ndio sio wajibu wao kutoa Ajira (na kama ndivyo..., hizo Government basi ziwe slim na ziendeshwe kwa tija na pesa ndogo) Je are we really a Capitalistic Free Market Country (au bado tunapangiana bei na kuruhusiwa kama tuuze Mazao yetu nje au tusiuze, au bei tukiuza tofauti tunaitwa walanguzi)
 
Mtoa mada elewa sio wajibu wa serikali kutoa ajira ,wajibu wake ni kutengeneza mazingira ya watu kujiajili au private sector's kurahisishiwa mazingira ya kuendesha shughuli zao na hii inaleta ajira,na elewa PresidentSamia ametoa ombi kuwa laumu na pia toa mawazo ya to remedy the situations sasa wewe unafanya kinyume,lawama lawama tu bila ya kushauri the better way forward,amka wewe middle class wa kitanzania acha kuwa kama mtoto anayehitaji kulishwa.
Nonsense! Ulipata lolote toka hotuba ya rais? Mwenye mada kalianzisha. soma michango ya watu ndo uelewe umuhimu wa uzi huu.
Ajira huwa ni ajenda muhimu kwa kila taifa. Serikali inatakiwa kubuni mipango ya kuongeza ajira. Siyo kutueleza vijana mujiajiri, wajiajiri wapi?
 
Kwa akili yako unaona kazi ya rais ni kutoa ombi? UNazungumzia kurahisisha mazingira, kwa vipi au nayo ni theory mpya. Biashara ni kulipa kodi, FINITO! Hawa wanachukuwa Forex wanapeka China kununua plastiki na nguo. Wanauza kwa shilingi na kununua tena forex kupeleka china. Wasipotozwa kodi hizo forex wanazo export zitatoka wapi?

Serikali itoe mikakati ya kusupport manufacturing industries siyo wafanyabiashara wa kununua kuuza nao wadai huruma ya tax!
 
No need kupishana kwa lugha isiyo staa,jibu hoja na its our right kutofautiana sio kutumia lugha za matusi,kuniita mimi au mchango wangu nonsense ni kuonyesha wewe ni mtu wa namna gani,wewe engage mimi kihoja sio matusi,na wewe sio spokesperson wa serikali za dunia,sio wajibu wa serikali kutoa ajira but ni wajibu wao kuandaa mazingira ya kuzalisha ajira nyingi.
 
Kwa akili yako unaona kazi ya rais ni kutoa ombi? UNazungumzia kurahisisha mazingira, kwa vipi au nayo ni theory mpya. Biashara ni kulipa kodi, FINITO! Hawa wanachukuwa Forex wanapeka China kununua plastiki na nguo. Wanauza kwa shilingi na kununua tena forex kupeleka china. Wasipotozwa kodi hizo forex wanazo export zitatoka wapi?

Serikali itoe mikakati ya kusupport manufacturing industries siyo wafanyabiashara wa kununua kuuza nao wadai huruma ya tax!
Hili ninaafikiana nalo ,na sijalipinga kabisa kodi ndio msingi na wajibu wetu
 
Back
Top Bottom