Wakuu nipo mbali Sana na mziki wa wa Africa kipindi Cha nyuma nlikuwa naskiza radio station moja ya Naigeria huko online naona cku hizi haipo

Sasa naombeni msaada wa hizi nyimbo

Patoranking mpya
Bebe Cool cjui Ila neno moja naskia Ni Party au la cjui msaada pia

Kuna huu mpya wakinaija Somebody nisaidie
 
Kuna wimbo wa kiafrica umeimbw na mwanadada fulani, miondoko ya taratibu kwenye korasi (chorus) wanataja maneno Kama TABURAREE halafu inafata gitaa ya besi ya taratibu.

Kama Kuna anaeufaham hata jina naomba anitajie..jimeshahangaika sana
Somebody help
 
ANAITWA MBILIA BEL WIMBO UNAITWA BOYA YE
 
Nadhani unaitwa NIMEMFUKUZA wa msanii Naurichiko
 
Kuna wimbo siujui jina kabisa ila ulipigwa na Producer D Money ,unasound kama Raha aaaa ...Ai sijui Dar ...aaaaa .....ai afu kuna kakinanda kanapiga kwa ndani hivi na biti kali sana huo wimbo ulikuwa unapigwa sana Kiss fm hasa za D Money
 
Kuna wimbo kaimba mzee gurumo,anaimba hivi,unatesa familia yako kwa kujali anasa kutwa kwenye mitaa nyumbani huonekani,nautafuta sana huu wimbo
 
Kuna wimbo kaimba mzee gurumo,anaimba hivi,unatesa familia yako kwa kujali anasa kutwa kwenye mitaa nyumbani huonekani,nautafuta sana huu wimbo
Unaitwa Isihaka, ni wa bendi ya Orchestra Safari Sound (OSS). Ninao kwenye simu ila siwezi kuutuma humu kwenye JF maana kila nikijaribu kutuma chochote humu kinakataa.
 
Mambo vipi? Kuna wimbo nilisikia kitambo wa bongo fleva unaimmbwa
"nitawakabili wasichana wawili nashindwa tegua kitendawili nimwamini yupi kati ya pili au lilly" kama unaufahamu na unaweza kuupata utupue
 
Kuna wimbo wa kitambo kidogo bongo fleva unaitwa pili au lilly kama unao naomba
 
Naomba kupatiwa wimbo wa rama d - bila yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…