Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Msaada natafuta huu wimbo muimbaji;
Manyota-pesa

Nautafuta sana sijafanikiwa kupata,

Na wimbo mungine wa asili nilikua nausikia sana kwenye kipindi cha Ngoma zetu tbc Kanda ya kusini enzi hizo,
Na mtangazaji asheri chilewa wimbo umeimbwa na;

Ilulu theatre - pesa

Mwenye nao tafadhali au naombeni muongoza namna gani naupata, Nawasilisha.
 
Squeezer - Kubamba
Jaji hakim - Miss bongo
G Solo - kwenye tv
G Solo - Umaarufu

Mwenye hizo nyimbo anisaidie wakuu.
 
Kuna Ile nyimbo ya Zamani Sijui kaimba nani sio mtanzania ila Wanaimba hv

Mano Mano Mambo
Mano Mambo eeeh
Mano Mambo Mano Mambo Eeeh
 
Oy nataka nyimbo zofiatazo kama unazo ni bless
1.H mbizo zuzu
2.Young Dee cowbama
3. hii nakumbuka choruss tu inaimbs hv "Mwisho wa mwezi ukifika watu tunajirusha x2
"Twende juu mpaka chini sote tunajirusha"
4Hii nayo nakumbuka choruss tu
"Anataka kwenda """ nami ni usiku wa raha mambo hadharani. Baby
 
Kuna nyimbo inapigwa sana efm inasema “sinung’ung’uniki
Si lalamiki”
Sehemu nyingine anasema
“Ridhiki anatoa mola”
Yani wanaipiga sana efm tatizo jina silifahamu
 
Kuna wimbo mwenyewe nautafuta wakuu,
01: Kiu Yangu-Mamajusi Choir
02:Yesu alimwambia Simon-Kilimanjaro Revival Choir.

Msaada mwenye nazo🙏
 
Kuna wimbo wa gospel nautafuta ila siujuwi jina ila wa zamani kidogo, nakumbuka tu nukuu yake;

Nifanye nini, bwana amesemaa,
Mtu yule atakae ukoka,
Akimbie Ili aiponyee,nafasi yaake.
(Hiyo ni kweli)
Fikilia unayoyafanyaa,
Ni mazurii, au yanatishaa,
Ubadilikee Ili uiponyee,nafasi yakoo,
(Tubadilike).

Mwenye kukumbuka huo wimbo anisaidie wakuu.
 
Habari humu
Tafadhari wale wa zilipendwa wenzangu
Mwenye wimbo wa Remmy Ongala na bendi yake super Matimila
Wimbo unaitwa UZEE
mashairi yake yako hivii
"Nikikumbuka uzee silaaali ninabaki na mawazo huruuuma,
Ujana maaaama ujaaaana, ujana maji ya moto ujaaana"
Tafadhari mwenye huo wimbo nauomba
 
We mkaka mambo, natafuta wimbo wa "Shangingi/Buzi" wameimba Muungano Cultural Taarab.

Wanaimba hivi:

Buzi limewekwa chini shangingi analichuuuna
Linachunwa kwa ulanini huku linapakwa ina.
Mashangingi acheni mambo waume mtawamaliiiza
Punguzeni urembo wenzenu mwawatatiza


Yaani nikiupata nitafurahi sana, hata ukinitongoza sitokataa.
Nimeupay tyr 🤣
 
Back
Top Bottom