Ni zaidi ya miaka 20 sasa somo la Hisabati linakuwa la mwisho katika ufaulu shule za msingi na sekondari. Nani alaumiwe?

Wanafunzi wenyewe
Umemaliza kila kitu. Hawa wanafunzi ni mahiri sana kwenye kuimba haniiiii lakini siyo hesabu... Pili zamani hesabu tulifundishwa lazima uonyeshe njia uliyotumia kupata jibu, hata karatasi za mitihani unakuta kuna sehemu ya swali, katikati ni njia na mwisho ni sehemu ya jibu. Ulishaona wapi hesabu inakuwa ni multiple choices?? Hapa wa kulaumiwa ni serikali na sera zake. Suluhisho: Viongozi wote wa umma na serikali iwe ni lazima watoto wao kusoma shule za Kayumba, iwe ni marufuku watoto wao kusoma hizi English medium... Mimi nakumbuka nilisoma shule moja na Mtoto wa Cleopa Msuya pale Old Mishi, akiwa Waziri wa fedha.. Shule ilikuwa mpaka na walimu wazungu kutoka Marekani, Urusi nk...
 
Serikali imeharibu sana huu mtindo wa kuchagua,sijui nani alianzisha huu utaratibu
 
Hesabu sio somo la mchezo mchezo dunia nzima. Kabla ya kulaumu waalimu tujiulize sisi wazazi tumewahi kuwafundisha watoto hizo hesabu hata mara chache? Wazazi vilaza halafu wanategemea mtoto awe mkali wa hesabu? Wanaoimudu hesabu huwa wanajitoa hasa kufanya bidii ya kusoma na mazoezi ya kutosha. Tukiacha siasa za kufananisha HKL na PCM ndo tutafika mbali. Waalimu wa hesabu walipwe mshahara hata mara 3 ya waalimu wa Arts ili kuvutia wakali wa hesabu kuingia kwenye ajira ya ualimu.
 
Huo muda wa kusolve hesabu watoto wanautoa wapi na kichwani kumejaa haniiii
 
Ukiacha uzembe wa wanafunzi lakini ukijaribu kutembelea tu shule zetu hizi, hao walimu wa maths aisee utachoka kabisa. Watu wanasoma hesabu badala ya kuifanya, no commitment nk
 
hapo we jiulize swali dogo tu je kipofu anaweza kumwongoza kipofu mwenzake?

au je inawezekana mwiba ukazaa maembe au mastaferi?

ukipata hayo majibu pigia mstari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…