Umemaliza kila kitu. Hawa wanafunzi ni mahiri sana kwenye kuimba haniiiii lakini siyo hesabu... Pili zamani hesabu tulifundishwa lazima uonyeshe njia uliyotumia kupata jibu, hata karatasi za mitihani unakuta kuna sehemu ya swali, katikati ni njia na mwisho ni sehemu ya jibu. Ulishaona wapi hesabu inakuwa ni multiple choices?? Hapa wa kulaumiwa ni serikali na sera zake. Suluhisho: Viongozi wote wa umma na serikali iwe ni lazima watoto wao kusoma shule za Kayumba, iwe ni marufuku watoto wao kusoma hizi English medium... Mimi nakumbuka nilisoma shule moja na Mtoto wa Cleopa Msuya pale Old Mishi, akiwa Waziri wa fedha.. Shule ilikuwa mpaka na walimu wazungu kutoka Marekani, Urusi nk...