Ni zipi mbinu za kudhibiti wizi kwenye duka la jumla?

Ahsante kwa ushauri wako kuu

Ngoja niwatafute jamaa wa IT naamini hii itakua issue simple kwao...
 
Hapo software itafanya kila kitu
Stock inayoingia na jinsi wafanyakazi wanavyo uza. Kila kitu kirekodiwe kwenye software
sawa mkuu ngoja nianze kuifatilia hi issue

Nitaweka mrejesho hapa...
 
Mkuu samahani nje ya mada. Hivi duka kama lako hilo la jumla linacost kiasi gani cha pesa?
nimeanza na mtaji mdogo then kila biashara inavyo zidi kuwa na wateja wengi naongeza mtaji


Minimum niliyoanza nayo milion 10.700.000
 
Mkuu una ID ya kibabe sana.
Tupe siri ya mafanikio katika biashara yako
 

Kuna system sijui ndo app unaingiza stock yako yote
Akiuza anaingiza inadeduct pale,bidhaa ikikaribia kuisha inaonyesha pale

App inabeba idadi ya bidhaa pamoja na mauzo

Utaona turnover ya mwezi na pia unaweza kuregister wanunuzi wa mara Kwa mara ukaona turnover yao.
 
Ahsante kwa ushauri wako kuu

Ngoja niwatafute jamaa wa IT naamini hii itakua issue simple kwao...

Kuna jamaa anafanya hii ndo wauzaji wa kariakoo wanatumia
Ukihitaji kesho naweza kukutafutia mawasiliano
 
Kwa picha ya Duka lake inaonekana Ni biashara changa bado na kumuambia sijui CCTV sijui Software unamuongezea gharama bila sababu. Wabongo anakuja na vitu vyake anauza kwanza baadae ndio anauza vyako. Hizo Software hazigusi utakuta hesabu zipo sawa always
 
hi ndio inaniumiza sana siku nitakayo tembelea mfano Mwanza nikaa Dukanii mweyewe siku nzima basi mauzo yanaongezeka mara mbili ya mauzo ya wafanyakazi....
 
All in all huwezi kuzuia mianya ya kupigwa hata ufunge nn
Chamsingi walipe vizur wafanyakazi ishi nao kwà amani na upendo Jenga Imani kwako

Cha mwisho kama unapata faida hicho ndo chamsingi hayo mengine ni kujipa gharama bure

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mastermind wanajua kusoma ramani jinsi ya kupiga na mda gani jambo litokee huenda wakachagua siku upo ñdo wanapiga vizur tuu hata ufunge nn wabongo hawashindwi jambo


Ilikujaga mashine ya kukamata wezi bongo mbona iliibiwa hiyo mashine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Weka mfumo wa computer, kuna kiapplication kinaitwa aleco kiko poa, au app nying tu za ivyo zipo ukitafta
 
Hahaha kumbe ndivyo ilivyo
Mkuu usiombee!

Nilikuwa nafanya kazi na dogo mmoja nauza spare na oils,sasa siku moja akaja jamaa nilikumbuka kumuona sana akija kufanya manunuzi pale dukani so nikawa nimekariri bidhaa anazopenda kuchukua mara kwa mara ila siku hiyo akaja akataka bidhaa tofauti na alizozoea,(kwangu halikuwa tatizo)tatizo ni bidhaa aliyoagiza mbona carton yake ikaonekana nzito sana isivyo kawaida?

Normally,carton ya oil zile litre moja moja uzito wake hauzidi Kg10/12 but nikashangaa mbona hili boksi alilotoa huyu dogo linaonekana zito ameinua hadi mishipa ya shingo imemtoka na amelifunga kamba katikati?siyo kawaida kabisa box jepesi kufungwa kamba(ukweli sikuelewa na ilikuwa ni bahati yangu tu kama ningekuwa bize ningeshaisha)nikamwambia weka hilo box chini,akashtuka ohh bro unajua jamaa ana haraka sana nikamuuliza ana haraka mbona unamsemea wewe yeye hajasema mwenyewe?kuinua macho namuona jamaa yule mteja anavuka mtaa anakimbia na hela yake kaacha,nikajiuliza inakuwaje hapa?sijakaa sawa yule dogo akatoka mle ndani speed alikoswa koswa kugongwa na pikipiki.

Kwa ufupi,alikuwa amejaza spare battery terminals zile za gari kubwa zenye thamani ya Tsh 680,000/= kwenye boksi ya oil yenye thamani ya Tsh 56,000/= ambayo ndo nilikuwa nimelipwa mkononi!!utauwa mtu!!!mimi sasa hivi kama sipo office haifunguliwi acha nipate hasara ya siku kuliko kuamini tena mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…