Nia ya mheshimiwa Rais ni njema, turekebishe mapungufu yaliyoonekana ili DPW aanze kazi haraka hapo bandarini.

Sheria za manunuzi ya umma hairuhusu kampuni kutoa ushawishi wowote ikiwemo rushwa ili kupewa tender, kuna taarifa hawa watu wamemwaga asali kwa baadhi ya wanasiasa na watendaji.

Kinachotakiwa ni hiyo kampuni kuwa blacklisted na siyo kuweka viraka kwenye mkataba wa kitapeli.​
 
Ni kweli. Hao jamaa ni wajanja sana, sio wao tu bali wawekezaji wote. Iliyokoukwa ni sheria ya maadili ya viongozi wa umma. Mwekezaji hana kosa, yes, kutoa zawadi nzito nzito kwa viongozi wa nchi fulani ili kurahisisha mchakato it's immoral but not illegal! kosa ni la waliopokea zawadi na kushindwa kuziwasilisha mahala husika.

Hako ka utaratibu ka wawekezaji kuwapeleka watendaji nje kapo sana nchini. Hata TRC bila shaka walikwenda Korea kabla ya kuwapa tenda ya kutengeneza mabehewa. Watu waserikalini huwaambii kitu kwenye hizo safari za nje.
 
Peleka huko uzwazwa wako!
Sisi tunasubiri hukumu ya Mahakama Kuu ya tarehe 7/8.
Kungekuwa na nia njema Watanzania wangejulishwa mapema na si kwenda kisiri Siri ughaibuni kusaini mkataba wa Kimangungo!
 
Hao wabinafsi na wezi wanawekwa na viongozi kwa nepotism. Viongozi wanaweka watu wao kwenye kila shirika linaloingiza pesa nyingi, hapo usitegemee ufanisi bali upigaji.
Katiba mpya iweka vigezo mahususi za kuongoza hayo mashirika, vijana wenye vipaji ndo washikirie mashirika yetu uone kama hayatasonga.
 
Wazanzibari wote hautaki muungano by nature. Kwa hiyo wakipata upenyo wa kuiumiza Tanganyika wanaiumiza kweli kweli. Hapo walikuwa hawafanyi kumkomoa mama bali kuikomoa Tanganyika. Matokeo yake sasa watanganyika wameamka, soon watarudi kwao wasubiri kisiwa chao kumezwa na bahari kama ilivyotabiriwa kwenye Qur'an
 
Kwani wenye mamlaka ya kurekebisha mkataba ni nani? Gharama na usumbufu wa kurekebisha mkataba DPW Hawatakubari kirahisi. Frame ya mkataba wa DPW haukuwa hivi ila mikataba ya namna hii ni kama kubet tu kadri unavyoongeza mechi odd zinaongezeka i.e mpunga unapanda kwa kasi wenye bonas. Sababu ya mikataba kuliumiza taifa ni hyo ya kutaka pakubwa kwa haraka
 
Hata kwakutumia mikataba mibovu? ambayo jiwe allikataa
 
Samia ndo wa kwanza kusign, mkataba una sahihi yake, kwa mara ya kwanza Tanzania Rais ana sign mkataba hewa, lakini cha msingi ni kurekebisha, kuondoa vile vipengele tata na kuendelea na uwekezaji, shida kubwa ni ccm , badala ya kurekebisha wako busy kusomba watu waje kwenye mikutano kusikiliza makosa ambayo hawataki kukubali, unaona walivyo wajinga?

Kama Rais sio mjanja CCM ni raihisi sana kukuingiza King, mimi nashauri Samia asisikilize mapambio ya CCM angesikiliza watalaam wa sheria ambao hawa fungamani na chama , hapo ndo atajua ukweli.
 
Hakuna nia njema, as long as walifanya Siri na Zanzibar hawakuiweka, Samia ana nia ovu na bandari zetu
 
Hakuna rahisi mbovu kama huyu.
Hakuna anachojua zaidi ya kusema na hili nalo mkaliangalie.
Serekale imekuwa ya kipigaji na wizi wa wazi wazi.
 
Peleka huko uzwazwa wako!
Sisi tunasubiri hukumu ya Mahakama Kuu ya tarehe 7/8.
Kungekuwa na nia njema Watanzania wangejulishwa mapema na si kwenda kisiri Siri ughaibuni kusaini mkataba wa Kimangungo!
😁😁😁
Ndugu yangu unaimani kubwa sana juu ya uwezo wa mahakama zetu kuitikisa serikali. Historia inaonesha mara nyingi waheshimiwa majaji hawana huo ujasiri.
 
Bado tuko hatua za awali, hawajawekeza fedha yoyote pale bandarini. Tunaweza kurekebisha au hata kuuvunja kama tutakuwa tayari kusema ukweli mahakamani juu wa viongozi wetu waliopewa 'zawadi' kule Dubai.

Kuomba mazungumzo na kurekebisha ni njia nzuri zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…