Kilimbatzz
JF-Expert Member
- Feb 11, 2023
- 9,134
- 14,593
Ameenda lini!?Diplomasia mkuu, inasemekana ameenda huko mwemyewe, hopefully atafanikiwa. Namwombea afanikiwe.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ameenda lini!?Diplomasia mkuu, inasemekana ameenda huko mwemyewe, hopefully atafanikiwa. Namwombea afanikiwe.
heshima ni jambo la bure si kila reply unapaswa kuquoteChawa mwenye njaa kali hatari
'inasemekana' mkuu 😁, zinaweza kuwa tetesi za uwongo. Lakini bila shaka ameyasikia malalamiko ya watu.Ameenda lini!?
Nikupe like!?heshima ni jambo la bure si kila reply unapaswa kuquote
nafikiri sikipaumbeleNikupe like!?
Manunuzi ya umma yanaruhusu single source ukiwa na justification. Haina tatizo kabisa, kwenye tenda huko hakufai sometimes.
Hao wanajaribu kung'olewa pale bandarini watakuja na makampuni yenye majina tofauti tofauti na watapenyeza rupia mpaka washinde tenda. Kisha business as usual.
Turekebishe tu ule mkataba usikae ki 'Mangungo', uwe na muda naalumu na kuwe na mechanism ya kuhakikisha pande zote zinawajibika.
😏😏😏😏😏nafikiri sikipaumbele
Ni kweli. Hao jamaa ni wajanja sana, sio wao tu bali wawekezaji wote. Iliyokoukwa ni sheria ya maadili ya viongozi wa umma. Mwekezaji hana kosa, yes, kutoa zawadi nzito nzito kwa viongozi wa nchi fulani ili kurahisisha mchakato it's immoral but not illegal! kosa ni la waliopokea zawadi na kushindwa kuziwasilisha mahala husika.Sheria za manunuzi ya umma hairuhusu kampuni kutoa ushawishi wowote ikiwemo rushwa ili kupewa tender, kuna taarifa hawa watu wamemwaga asali kwa baadhi ya wanasiasa na watendaji.
Kinachotakiwa ni hiyo kampuni kuwa blacklisted na siyo kuweka viraka kwenye mkataba wa kitapeli.
tuendele na mjadala😏😏😏😏😏
Hao wabinafsi na wezi wanawekwa na viongozi kwa nepotism. Viongozi wanaweka watu wao kwenye kila shirika linaloingiza pesa nyingi, hapo usitegemee ufanisi bali upigaji.Mkuu uko sahihi lkn tatizo kubwa la nchi hii ni kuto kuwa na maadili na uzalendo kwa nchi yetu na kwa wa Tz wenzetu, hii imepekea kuwa kuwa wabinafsi tulio kubuhu.
Watu hatujali kabisa shida za wezetu hata kidogo, hatudhamini kabisa naisha ya watu wengine.
Na chukizwa sana na hii tabia ya ubinafsi
Wazanzibari wote hautaki muungano by nature. Kwa hiyo wakipata upenyo wa kuiumiza Tanganyika wanaiumiza kweli kweli. Hapo walikuwa hawafanyi kumkomoa mama bali kuikomoa Tanganyika. Matokeo yake sasa watanganyika wameamka, soon watarudi kwao wasubiri kisiwa chao kumezwa na bahari kama ilivyotabiriwa kwenye Qur'anAtaweza kuwafukuza watoto wapendwa Mbarawa, Aisha na Johari! Sidhani na sitarajii.
Hivi kweli wewe unategemea Mbarawa, Ausha na Johari wanaweza kuwa maadui wa ndani ya chama wa mama?
Ufahamu kuwa inner circle yote ya kushughulikia jambo hili ilikuwa ya Wazanzibari. Unataka kuwaaminisha watu kuwa maadui wa mama ni Wazanzibari?
Hata kwakutumia mikataba mibovu? ambayo jiwe allikataaNchi hii ina mambo jamani, yaani kuna vita zinaendelea chini chini huko ndani ya chama Mungu amsaidie mama yetu SSH.
Nia ya uwekezaji pale bandarini ni njema kabisa, dhamira safi kabisa. Ni uwekezaji unaokwenda kukata mirija wa watoto wa mjini ambao wamekuwa wakinyonya pale kwa raha zao.
Sasa nashindwa kuelewa, kwamba wahusika walipaswa kumsaidia Mh. Rais kwenye ule mkataba/ makubaliano ni vilaza au wamefanya makusudi kusaini yale madudu ili kumchafua Mheshimiwa?? Kwamba miongoni mwao wapo watu wa ile kambi nyingine ya chama ambao wameamua kumhujumu Rais kwa makusudi kabisa??
Mama SSH usiwe mnyonge, rekebisha mapungufu machche yaliyopo kisha wawajibishe wote waliosababisha taharuki hii kwa kutokutimiza wajibu wao na kupitisha mkataba ukiwa hovyo kiasi kile. Baada ya hapo kazi iendelee, tunahitaji uwekezaji wenye tija pale bandarini. Kama DPW anaiweza hiyo kazi na watafanya kwa uaminifu na kuhakikisha wale wahuni hawaigeuzi bandari kuwa shamba la bibi, why NOT? Tuwape wapige kazi.
Usisahau kuiweka mikataba wazi, itakusaidia usichomekewe madudu na wapinzani wako wa ndani ya chama. Inaonekana mtandao wao ni mpana.
😁😁😁Peleka huko uzwazwa wako!
Sisi tunasubiri hukumu ya Mahakama Kuu ya tarehe 7/8.
Kungekuwa na nia njema Watanzania wangejulishwa mapema na si kwenda kisiri Siri ughaibuni kusaini mkataba wa Kimangungo!
Bado tuko hatua za awali, hawajawekeza fedha yoyote pale bandarini. Tunaweza kurekebisha au hata kuuvunja kama tutakuwa tayari kusema ukweli mahakamani juu wa viongozi wetu waliopewa 'zawadi' kule Dubai.Kwani wenye mamlaka ya kurekebisha mkataba ni nani? Gharama na usumbufu wa kurekebisha mkataba DPW Hawatakubari kirahisi. Frame ya mkataba wa DPW haukuwa hivi ila mikataba ya namna hii ni kama kubet tu kadri unavyoongeza mechi odd zinaongezeka i.e mpunga unapanda kwa kasi wenye bonas. Sababu ya mikataba kuliumiza taifa ni hyo ya kutaka pakubwa kwa haraka