Nia ya mheshimiwa Rais ni njema, turekebishe mapungufu yaliyoonekana ili DPW aanze kazi haraka hapo bandarini.

Nia ya mheshimiwa Rais ni njema, turekebishe mapungufu yaliyoonekana ili DPW aanze kazi haraka hapo bandarini.

Mzalendo Uchwara

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2020
Posts
4,437
Reaction score
13,836
Nchi hii ina mambo jamani, yaani kuna vita zinaendelea chini chini huko ndani ya chama Mungu amsaidie mama yetu SSH.

Nia ya uwekezaji pale bandarini ni njema kabisa, dhamira safi kabisa. Ni uwekezaji unaokwenda kukata mirija wa watoto wa mjini ambao wamekuwa wakinyonya pale kwa raha zao.

Sasa nashindwa kuelewa, kwamba wahusika walipaswa kumsaidia Mh. Rais kwenye ule mkataba/ makubaliano ni vilaza au wamefanya makusudi kusaini yale madudu ili kumchafua Mheshimiwa?? Kwamba miongoni mwao wapo watu wa ile kambi nyingine ya chama ambao wameamua kumhujumu Rais kwa makusudi kabisa??

Mama SSH usiwe mnyonge, rekebisha mapungufu machche yaliyopo kisha wawajibishe wote waliosababisha taharuki hii kwa kutokutimiza wajibu wao na kupitisha mkataba ukiwa hovyo kiasi kile. Baada ya hapo kazi iendelee, tunahitaji uwekezaji wenye tija pale bandarini. Kama DPW anaiweza hiyo kazi na watafanya kwa uaminifu na kuhakikisha wale wahuni hawaigeuzi bandari kuwa shamba la bibi, why NOT? Tuwape wapige kazi.

Usisahau kuiweka mikataba wazi, itakusaidia usichomekewe madudu na wapinzani wako wa ndani ya chama. Inaonekana mtandao wao ni mpana.
 
HUYU MAMA HUWA NA UTARATIBU WA KUMUOMBEA KILA ALFAJIRI
Safi, mafanikio yake ni mafanikio ya nchi. Plus, huyu ni best chance ya nchi kupata katiba mpya, ikitupita hiyo ndio basi tena. Labda miaka 20 mbele.
 
Hivi akituchezea akili akisema tunaurekebisha na akatoa vipengele vilivyorekebishwa lakini chini ya kapeti ukatekelezwa huu wa tarehe 25.10.2022 tutafanyaje?
 
Asifanye kiburi arekebishe hayo mapungufu. Asikaze shingo kama alivyo peleka mkataba bungeni wakati huku nyuma kuna malalamiko mengi
Mama samia rekebisha mambo
 
Utaratibu wa manunuzi ya umma utumike, tender itangazwe kampuni ziombe. Kuingiza nchi kwenye vifungo vya mkataba wa hovyo kwa jambo dogo la kuendesha operation za makontena bandarini ni ujuha.​
 
suala la katiba kwa sasa watanzania wanahitaji uchumi bora ,afya , elimu miundombinu bora nk
Ni kweli, hayo mahita yapo na yatakuwepo kwa miaka mingi ijayo.

Katiba bora itawezesha inahitajika ili kuweka misingi ya uwajibikaji na haki. Ni vigumu kupata maendeleo kwenye mfumo ambao mtu anaweza kufisadi fedha nyingi tu lakini vyombo vyote vilivyoundwa ili kuzuia hayo havina meno dhidi yake.
 
Kabisa, anayeshindwa anapisha wenye akili ya kuendesha. Watanganyika million 60 hatuwezi kukosa vijana 1000 wa kuendesha bandari zetu
Mkuu uko sahihi lkn tatizo kubwa la nchi hii ni kuto kuwa na maadili na uzalendo kwa nchi yetu na kwa wa Tz wenzetu, hii imepekea kuwa kuwa wabinafsi tulio kubuhu.
Watu hatujali kabisa shida za wezetu hata kidogo, hatudhamini kabisa naisha ya watu wengine.
Na chukizwa sana na hii tabia ya ubinafsi
 
Nchi hii ina mambo jamani, yaani kuna vita zinaendelea chini chini huko ndani ya chama Mungu amsaidie mama yetu SSH.

Nia ya uwekezaji pale bandarini ni njema kabisa, dhamira safi kabisa. Ni uwekezaji unaokwenda kukata mirija wa watoto wa mjini ambao wamekuwa wakinyonya pale kwa raha zao.

Sasa nashindwa kuelewa, kwamba wahusika walipaswa kumsaidia Mh. Rais kwenye ule mkataba/ makubaliano ni vilaza au wamefanya makusudi kusaini yale madudu ili kumchafua Mheshimiwa?? Kwamba miongoni mwao wapo watu wa ile kambi nyingine ya chama ambao wameamua kumhujumu Raisbkwa makusudi kabisa??

Mama SSH usiwe mnyonge, rekebisha mapungufu machche yaliyopo kisha wawajibishe wote waliosababisha taharuki hii kwa kutokutimiza wajibu wao na kupitisha mkataba ukiwa hovyo kiasi kile. Baada ya hapo kazi iendelee, tunahitaji uwekezaji wenye tija pale bandarini. Kama DPW anaiweza hiyo kazi na watafanya kwa uaminifu na kuhakikisha wale wahuni hawaigeuzi bandari kuwa shamba la bibi, why NOT? Tuwape wapige kazi.

Usisahau kuiweka mikataba wazi, itakusaidia usichomekewe madudu na wapinzani wako wa ndani ya chama. Inaonekana mtandao wao ni mpana.
Ataweza kuwafukuza watoto wapendwa Mbarawa, Aisha na Johari! Sidhani na sitarajii.

Hivi kweli wewe unategemea Mbarawa, Aisha na Johari wanaweza kuwa maadui wa ndani ya chama wa mama?

Ufahamu kuwa inner circle yote ya kushughulikia jambo hili ilikuwa ya Wazanzibari. Unataka kuwaaminisha watu kuwa maadui wa mama ni Wazanzibari?
 
Ni kweli, hayo mahita yapo na yatakuwepo kwa miaka mingi ijayo.

Katiba bora itawezesha inahitajika ili kuweka misingi ya uwajibikaji na haki. Ni vigumu kupata maendeleo kwenye mfumo ambao mtu anaweza kufisadi fedha nyingi tu lakini vyombo vyote vilivyoundwa ili kuzuia hayo havina meno dhidi yake.
Katiba bora bila utashi sahihi wa watawala na watawaliwa hakuna kitu
 
Utaratibu wa manunuzi ya umma utumike, tender itangazwe kampuni ziombe. Kuingiza nchi kwenye vifungo vya mkataba wa hovyo kwa jambo dogo la kuendesha operation za makontena bandarini ni ujuha.​
Manunuzi ya umma yanaruhusu single source ukiwa na justification. Haina tatizo kabisa, kwenye tenda huko hakufai sometimes.

Hao wanajaribu kung'olewa pale bandarini watakuja na makampuni yenye majina tofauti tofauti na watapenyeza rupia mpaka washinde tenda. Kisha business as usual.

Turekebishe tu ule mkataba usikae ki 'Mangungo', uwe na muda naalumu na kuwe na mechanism ya kuhakikisha pande zote zinawajibika.
 
Ataweza kuwafukuza watoto wapendwa Mbarawa, Aisha na Johari! Sidhani na sitarajii.

Hivi kweli wewe unategemea Mbarawa, Ausha na Johari wanaweza kuwa maadui wa ndani ya chama wa mama?

Ufahamu kuwa inner circle yote ya kushughulikia jambo hili ilikuwa ya Wazanzibari. Unataka kuwaaminisha watu kuwa maadui wa mama ni Wazanzibari?
Sina imani na Johari. Mbarawa sidhani kama ni memba wa mtandao wowote. Inawezekana ameponzwa na hofu tu kuwa Mheshimiwa anataka hili lifanyike, nikianza kuibua mapungufu nitaonekana nakwamisha. Ni kitu common sana serikalini.
 
Back
Top Bottom