Niacheni nilie maana bado sijasahau yaliyonipata jana yasije kunikuta tena

Niacheni nilie maana bado sijasahau yaliyonipata jana yasije kunikuta tena

Jiwe alikuwa mwizi kama wezi wengine tu. Bora hata ya hao wezi wengine walijiweka wazi kuwa wapigaji. Bw. Jiwe alijitwika umalaika mtu, mtiifu kupita kikomo kumbe nyuma ya pazia anatuchapa tu.
Kwa kifupi alikuwa kibaka mbabe. Anakuibia na mikwara juu.
[emoji2][emoji3][emoji2][emoji3][emoji2]
 
Let them provoke under the scene of freedom of expression cause non of your business.Are u okay Mango??!!!
Kenge mkubwa kabisa weye, hujiulizi kwanini Bunge limelalamika watanzania kutema nyongo kwa mwendazake, Kibajaj na Mwigulu wametoa onyo.
Basi muwe bias kwa kila upande sio kusifia misifa ya uongo wakati tulibanwa kila kona mpaka tweeter wakati sio yenu eti mnaifungia
 
Acha uongo wewe.nani kakiri???
Ni kweli wapo watu walio umizwa unadhani kwa nini hata yeye binafsi aliwahi kutamka ''Mtanikumbuka kwa mema na si kwamabaya'' alijua wazi katika kufyeka njia iliyo kuwa poli lazima viumbe wengine wataumia. Kwa jinsi nchi ilipokuwa imefikia ilihitaji shujaa kufanikiwa na ndio maana marais wastaafu wanakiri kushindwa kuirejeshe nchi kwenye mstari wa kuanza kupiga hatua.
 
Tatizo ni moja Tuu, jiwe alihubiri jinsi alivyoipigania nchi hii, Ila ule upande wa shilingi alioumiza watu hausemwi, Ila wahusika walioumizwa wanausema sasa.

Alichokifanya ni nothing dhidi ya maumivu aliyowapa watu, mi mwenyewe ni mhanga, usitegemee nikamsifu jiwe Kwa lolote kabisa.

Kikwete alichukiwa Sana na watu Kwa ubadhirifu wa Fedha na ufisadi, ila Leo hii ukimuuliza mtu Kati ya Jiwe na Msoga atakuchagulia Msoga chap.
Siyo kwel, jisemee mwenyewe! Nipo mtaani, nahoji wananchi! Majibu yanapingana mbali sana na yakovI see! Mimi na wananchi walioitwa wanyonge hatudanganyiki!; Kikwete na mapooza yake hatuwezi kuyakubali!
 
Ninalia tena msiba unaanza upya pale Mnapo nikumbusha enzi za kupishana angani! Mzee Kikwete alisafiri takribani safari za nje 421 kwa wastani wa siku tatu kila safari alikaa nje ya nchi kwa jumla ya siku 1263 katika miaka kumi, miaka 3 na miezi 4 hakuwepo nchini, ukiongeza siku zake za rikizo 28x10 = siku 280 ukijumlisha na miaka 3.4 unapata mzee hakuwepo ofisini kwa miaka 4 katika kumi, mwisho watu wakamwita Vasco da Gama wa Tanzania, ukiacha yeye mawaziri na watendaji wengine walikuwa wanapishana angani kwa safari za ulaya na nyingi zilikuwa za kwenda kuomba misaada kwa wafadhiri mpaka ya kujenge vyoo vya shule, hakuna tulichokuwa tunakiweza hadi kulipa mishara ya wafanyakazi wa serikali ilikuwa kitendawili '' kasungura kadogo.''

Ni kweli serikali haikuwa na hela za kuwahudumia raia wake kwani walikuwa hawakusanyi kodi misamaha ya kodi ilitamalaki nchi ikawa ya wapiga dili, misheni town misamiati ambayo leo imetoweka! Nakumbuka na bado nakumbuka bodi za wakurugenzi zikikaa nje ya nchi kudadavua ya nchini kwetu! mikataba inayotuhusu ikifungwa nje ya nchi bila ya kuwa na masilahi kwetu hakika zilikuwa enzi za bata bin batani kwa wale wasiofaidi wakati huo Mh.

Kwa sasa acheni tulinganishe kule na huku wapi tumefanikiwa ingawa ni kwa miaka mitano kwa kumi ya wenzi wake ni wapi tumefanikiwa zaidi kama taifa? Hili liko dhahili na hata wao Ma Rais wastaafu wanakili na walishakili mara nyingi kuwa mafanikio ya mwenda zake yameenda mbali kuliko vipindi vyao vya utawala kwani kati ya mengi yaliyowashinda yeye alifanikiwa kwa muda mfupi sana kuyapa ufumbuzi na nchi kuanza kupiga hatua za kimaendeleo. Amin amin nawaambia hakika mtamkumbuka kwa mema na si kwa mabaya.

Bado nakumbuka bajeti zetu za maendeleo na matumizi za kipindi kile, na alizoacha mwenda zake! napata shida moyoni je nitarejea kule au nitasonga mbele machozi yananitoka bado nalia na huenda nikalia zaidi, ila najipa moyo kwa kuwa mama alikuwepo jikoni wakati pishi hili likitengenezwa nina hakika anaijua njia sitarejea kwenye tembele la chukuchuku kwa kuwa eti sisi ni masikini, hatuna hela ya kununua viungo,msiba wangu utadumu milele kama mama atazisikiliza nyimbo za wapiga zumari wa eti ''umasikini wetu haushindiki''
Mkuu kwa yanayoendelea, tarajia Tanzania kurudi kule kabla ya JIWE. CCM ndio makini kabisa. La sivyo, itapotea!!!
 
Kinachotakiwa ni ku-balance mambo yote. Sio kuacha hiki na kufanya kile tu.
Mfano: Ni kweli sio vyema kwa kiongozi kupenda anasa na kimiliki vitu vingi vya thamani kupitia uongozi, lakini haikuwa sifa ya maana kwa marehemu Sokoine kusifiwa kumiliki suruali sijui mbili tu.

Watawala wajifunze kwamba Tanzania ni ya watanzania. Wao wamepewa dhamana tu. Kwahiyo yote wanayofanya yae na kiasi na wakumbuke wanawatumikia Tanzania.
JK alikuwa na extremes zake ambazo hazikuisaidia Tanzania. JPM pia. Ila wana mazuri yao mengi tu, maana ubinadamu wetu makosa ni lazima. Laana kubwa ni kusahau Tanzania ina watanzania karibu milioni sitini na kuamua kuwapa rasilimali za Tanzania kwa familia na rafiki zako. lazima watanzania watakuchukia
 
Kenge mkubwa kabisa weye, hujiulizi kwanini Bunge limelalamika watanzania kutema nyongo kwa mwendazake, Kibajaj na Mwigulu wametoa onyo.
Basi muwe bias kwa kila upande sio kusifia misifa ya uongo wakati tulibanwa kila kona mpaka tweeter wakati sio yenu eti mnaifungia
Watanzania gani hawa hawa waliyoacha shughuli zao na kwenda kuaga mwili wa Jiwe huku wakitandika kanga za barabarani Au unazungumzia watanzania wa mitandaoni?
 
Tatizo ni moja Tuu, jiwe alihubiri jinsi alivyoipigania nchi hii, Ila ule upande wa shilingi alioumiza watu hausemwi, Ila wahusika walioumizwa wanausema sasa.

Alichokifanya ni nothing dhidi ya maumivu aliyowapa watu, mi mwenyewe ni mhanga, usitegemee nikamsifu jiwe Kwa lolote kabisa.

Kikwete alichukiwa Sana na watu Kwa ubadhirifu wa Fedha na ufisadi, ila Leo hii ukimuuliza mtu Kati ya Jiwe na Msoga atakuchagulia Msoga chap.
Akirudi kugombea mzee wa Msoga nampa. Akisema anarudi katiba ibadilishwe tumpe atawale MILELE, binafsi sina pingamizi.
Mwendazake alianza vizuri, akalewa madaraka, akawa mbinafsi, mpendelea marafiki na ndugu waziwazi.
Hakuna maraisi waliopita walioonyesha ubinafsi kiwango cha mwendazake.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Mtu ni mmoja, na watu ni kuanzia wawili. Tanzania tupo watu zaidi ya milioni 50. Tufanye hiyo tafiti kwa hilo swali basi kujua watu kiasi gani watajibu vipi.
 
Akirudi kugombea mzee wa Msoga nampa. Akisema anarudi katiba ibadilishwe tumpe atawale MILELE, binafsi sina pingamizi.
Mwendazake alianza vizuri, akalewa madaraka, akawa mbinafsi, mpendelea marafiki na ndugu waziwazi.
Hakuna maraisi waliopita walioonyesha ubinafsi kiwango cha mwendazake.

Everyday is Saturday............................... 😎
Mhh, una uhakika? Isije kuwa zile dili za mujini ndio zilikuziba macho na masikio ukaona uko peponi.
 
Yapo mengi mema aliyo lifanyia taifa hili kutoka taifa lisilojitambua uwezo wake, hadi kuwa taifa linalojitambua,makosa yapo lakini yatupasa kushukuru kwa mema.
kujitambua ni kutesa raia wako kisa tofauti za mitizamo, kuwawekea vita vya kiuchumi wafilisike,kununua mandege yenye kuleta hasara, halmashauri kupata hati chafu kila mwaka,, kujengaa maukuta ya gharama huku unaibiwa kweli huko ni kujitambua?
 
Jiwe alikuwa mwizi kama wezi wengine tu. Bora hata ya hao wezi wengine walijiweka wazi kuwa wapigaji. Bw. Jiwe alijitwika umalaika mtu, mtiifu kupita kikomo kumbe nyuma ya pazia anatuchapa tu.
Kwa kifupi alikuwa kibaka mbabe. Anakuibia na mikwara juu.
Uzuri Magufuli alikuwa asafiri kwa hiyo mmeishia kusema alikuwa mwizi lakini mnashindwa kusema hizo fedha alizoiba aliziweka wapi?!
Kama alikuwa mwizi na wengine wanasema aliiba trilioni 1.5! Tuelezeni kama alizificha kule Dodoma shambani tukazifukue!!
 
Mtu anapiga 1.5 trilioni kimya kimya haijulikani ziko wapi

Kampuni yake unapata tenda za ujenzi kila Kona ya nchi.

Bado Kuna midege iliyonunuliwa mkataba wa manunuzi haijulikani ulipo hatujui alitupiga kiasi gani Cha juu.

Bado mishe mishe nyingi kazipiga na hakuna alieyeweza kumuhoji ukihoji unaishia jela au mochwari.

Hapo hapo !!

Watoto wa maskini waliomaliza vyuo kwa maelfu wanalalamika ajira hawaoni Wala hasikii.

Anakwapua hela za wastaafu kwa kigezo Cha vyeti feki Kama si uonevu Ni Nini?

Hakuna ongezeko la mishahara miaka 5 Wala madaraja

Pesa anatafuna yeye na cycle yake .

Kumuona Huyo mtu shujaa Ni uchizi,uwendawazimu na uduanzi labda Kama ulikuwa mnufaika na ufisadi wake

Hapo sijaongelea kubana Uhuru wa kujieleza na habari,mauaji ya wakosoaji wake ,kesi za kubumba,na mengine kedekede.

Binafsi nitaaahadithia wanangu tuliwahi kuwa na rais wa ovyo aitwa Magufuli
Embu tueleze hizo trilioni 1.5 aliziweka wapi?! Hauwezi kutudanganya alizificha abroad wakati hata nchi za jirani hakufanya ziara!!
 
Uzuri Magufuli alikuwa asafiri kwa hiyo mmeishia kusema alikuwa mwizi lakini mnashindwa kusema hizo fedha alizoiba aliziweka wapi?!
Kama alikuwa mwizi na wengine wanasema aliiba trilioni 1.5! Tuelezeni kama alizificha kule Dodoma shambani tukazifukue!!

hicho wanaandika hata wao hawakubaliani nacho,ndio vile watatanyaje maana kinachotakiwa ni kuzika alama aliyoweka.
 
Back
Top Bottom