Ninalia tena msiba unaanza upya pale Mnapo nikumbusha enzi za kupishana angani! Mzee Kikwete alisafiri takribani safari za nje 421 kwa wastani wa siku tatu kila safari alikaa nje ya nchi kwa jumla ya siku 1263 katika miaka kumi, miaka 3 na miezi 4 hakuwepo nchini, ukiongeza siku zake za rikizo 28x10 = siku 280 ukijumlisha na miaka 3.4 unapata mzee hakuwepo ofisini kwa miaka 4 katika kumi, mwisho watu wakamwita Vasco da Gama wa Tanzania, ukiacha yeye mawaziri na watendaji wengine walikuwa wanapishana angani kwa safari za ulaya na nyingi zilikuwa za kwenda kuomba misaada kwa wafadhiri mpaka ya kujenge vyoo vya shule, hakuna tulichokuwa tunakiweza hadi kulipa mishara ya wafanyakazi wa serikali ilikuwa kitendawili '' kasungura kadogo.''
Ni kweli serikali haikuwa na hela za kuwahudumia raia wake kwani walikuwa hawakusanyi kodi misamaha ya kodi ilitamalaki nchi ikawa ya wapiga dili, misheni town misamiati ambayo leo imetoweka! Nakumbuka na bado nakumbuka bodi za wakurugenzi zikikaa nje ya nchi kudadavua ya nchini kwetu! mikataba inayotuhusu ikifungwa nje ya nchi bila ya kuwa na masilahi kwetu hakika zilikuwa enzi za bata bin batani kwa wale wasiofaidi wakati huo Mh.
Kwa sasa acheni tulinganishe kule na huku wapi tumefanikiwa ingawa ni kwa miaka mitano kwa kumi ya wenzi wake ni wapi tumefanikiwa zaidi kama taifa? Hili liko dhahili na hata wao Ma Rais wastaafu wanakili na walishakili mara nyingi kuwa mafanikio ya mwenda zake yameenda mbali kuliko vipindi vyao vya utawala kwani kati ya mengi yaliyowashinda yeye alifanikiwa kwa muda mfupi sana kuyapa ufumbuzi na nchi kuanza kupiga hatua za kimaendeleo. Amin amin nawaambia hakika mtamkumbuka kwa mema na si kwa mabaya.
Bado nakumbuka bajeti zetu za maendeleo na matumizi za kipindi kile, na alizoacha mwenda zake! napata shida moyoni je nitarejea kule au nitasonga mbele machozi yananitoka bado nalia na huenda nikalia zaidi, ila najipa moyo kwa kuwa mama alikuwepo jikoni wakati pishi hili likitengenezwa nina hakika anaijua njia sitarejea kwenye tembele la chukuchuku kwa kuwa eti sisi ni masikini, hatuna hela ya kununua viungo,msiba wangu utadumu milele kama mama atazisikiliza nyimbo za wapiga zumari wa eti ''umasikini wetu haushindiki''