mkorinto
JF-Expert Member
- Jun 11, 2014
- 32,095
- 39,619
Ata kuzimu kuna malaika wa kuzimu wanaoteswa pamoja naye.
aliyekwambia malaika wa kuzimu ni sehemu ya wateswao ni nani!!!
kama mhudumu wa maiti si miongoni mwa maiti,jifunze zaidi.
Ata kuzimu kuna malaika wa kuzimu wanaoteswa pamoja naye.
Tunalishwa TAKWIMU wakati enzi ya Kikwete tulikula maisha.MWAMBIENI CAG, SISI TUMERIDHIKA!!
1. Mwambieni CAG kwamba sisi wenyewe tumeridhika, tumezoea kuibiwa. Mwambieni tofauti ya wizi wa zamani na huu ni kwamba wizi wa sasa unafaida kwa Wananchi wala asiumize kichwa. Mwambieni sisi Wananchi hatuna tatizo na hasara au wizi uliofanyika wakati wa JPM. Sisi tumeridhika hivyohivyo kwa sababu tuna macho ya kuona!!
2. Mwambieni CAG kwamba tuliibiwa hapa kupitia EPA. Pesa bilioni 135 zikaliwa na watu wachache, wakati huo elimu bure ilikua bado kuja. Mikopo ya elimu ya juu ilikua ni songombingo kwa hiyo hatuoni hatari kuibiwa sasa huku elimu bure ikiwa imeanzishwa na mikopo ikitoka kwa wakati. Sisi tumeridhika kabisa na hasara au wizi wa JPM!!
3. Mwambieni CAG kwamba tuliibiwa hapa bilioni 300 Serikali ikilipa Makampuni hewa katika kashfa ya MEREMETA. Mwambieni hapakua na tatizo lolote na wakati huo bajeti ya Dawa ilikua chini ya bilioni 30 lakini sasa na wizi wa JPM umepandisha bajeti ya DAWA zaidi ya mara tisa; yaani bilioni 270. Mwambieni kwa wizi huu Mungu atupe nini? Tumeridhika sana na wizi wa JPM.
4. Mwambieni CAG kwamba tulishaibiwa sisi kwenye mauzauza ya uwekezaji wa Bulyanhulu na Buzwagi na hata leo hakuna maelezo ya yanayoeleweka. Kodi hazikulipwa na pesa zikapigwa na wajanja wachache. Wakati huo wote madini na migodi yote ilikua ni mali ya wawekezaji wasiolipa kodi, Wananchi ilikua ni marufuku kukaribia migodi katika nchi yao. Kama JPM ameiba halafu wananchi wanachimba madini wenyewe kwa uhuru, ninaumia kwamba atakua ameiba kidogo sana. Wizi wenye manufaa kwa umma una maana zaidi kuliko wizi usio na manufaa. Sisi tumezoea kuibiwa, lakini kwa huu wa JPM tumeridhika.
5. Mwambieni CAG kwamba sisi tumezoea kuibiwa. Tumeshaibiwa haswa, ilikuja hapa tukaibiwa katika Mkataba wa kijinga wa DOWANS. Nchi ikalipa bilioni 111 kwa sababu ya maslahi ya watu wachache. Wakati tunaibiwa kupitia DOWANS, Mv. Victoria ilikua inalaza watu siku mbili ziwani kwa ubovu wake. Maisha yao yalikua hatarini kila safari, leo JPM akiiba au akitutia hasara ya bilioni 60 huku Mv. Victoria ikiwa MPYA kuna tatizo gani? Meli mpya tele kuanzia ziwa Nyasa, Tanganyika na Bahari ya Hindi Kilwa. Tunapenda wizi wa namna hii, angeiba kabisa za kutosha akajenga nyumba nzuri kama wenzake, akamiliki magari za mizigo meupe kukuki na sheli za kumwaga. Au akamilika supermakert za Da'slam kama wenzake. Sisi kuibiwa tumezoea, wizi wa JPM una manufaa, tumeridhika.
6. Mwambieni CAG kuwa sisi tumezoea kuibiwa asijiumize bure na ma-press ya kutangaza vi-wizi vya kitoto hivyo. Tulipigwa hapa pesa TAKATIFU katika Mkataba maarufu wa RICHMOND ulioondoka na Serikali ya mwaka 2008 hadi sasa hakuna kilichofanyika. Wakati tukipigwa pesa za Richmond daraja la Mfugale lilikua halipo, Daraja la Ubungo (Kijazi Interchange) haikuwahi kufikiriwa, Daraja la Tanzanite (Salender) lilikua katika ndoto, lile la Busisi halikufikiriwa kabisa. Kama tumeibiwa leo na mambo yote haya yamefanyika mwambieni CAG sisi roho kwatu, tumeridhika riport zake tupa kule hatusikii la mwazini wala mnadi swala. Tumefunga masikio!!
7. Mwambieni CAG sio hata siku nyingi zilichotwa BOT bilioni 306 kwa kilichoitwa kashfa ya TEGETA ESCROW. Nchi ikaibiwa tena na wajanja wachache, wakabeba pesa kwenye masandarusi. Wakati tukiibiana bilioni 306 za Escrow umeme vijijini ulikua unaunganishwa kwa Tsh. 454,000 ila kwa wizi wa JPM umeme vijijini unaunganishwa kwa Tsh. 27,000; asilimia zaidi ya 70 umeme umefika vijijini. Wizi mzuri kiasi gani huu!? Sasa tunajenga megawati 2400 kutoka Bwawa la Nyerere ili umeme ushuke zaidi. Ingalikua uwezo ni wangu ningalimrudisha mtu huyu aendelee kuiba na kutia hasara zaidi kwa sababu wizi na hasara zake zina manufaa kwa watu. Mwambieni CAG sisi tumeridhika hivyohivyo, atuwache!!
8. Mwambieni CAG sisi tumewahi kuibiwa Twiga mzima akabebwa na shingo yake akaondoka zake. Hii nchi tunaibiana na Wanyama yeye anahangaika na vipesa vidogo vidogo vya matengenezo ya ATCL. Mwambieni wakati tukiibiana TWIGA upatikanaji wa maji Vijijini ulikua ni asilimia 47 na sasa kwa wizi na hasara za JPM upatikanaji wa Maji vijijini umefikia asilimia 70.1 huku mijini upatikanaji ukitoka asilimia 74 hadi 84. Ni mtu mjinga pekee anaweza kuchukizwa na wizi wa JPM, mwambieni CAG sisi tumeridhika tunatamani angekuwepo aibe tena. Hatutakagi ujinga!!
9. Mwambieni CAG kuwa tumeibiwa sana nchi hii. Wakati wote tuliibiwa huku Nchi ikiwa haina Ndege hai hata moja. Mwambieni leo tuna Ndege 11 za kwetu wenyewe. Hizo hasara za ATCL zisimuumize kichwa, hakuna biashara isiyo na hasara, JPM keshawawekea mtaji na heshima ni wajibu wao kutafuta akili za kupata faida sio kuua mtaji. Mwambieni CAG, sisi tunampenda mwizi anayeiba halafu akanunua Ndege kwa ajili ya Nchi nzima, akajenga reli ya kasi, stend kibao za kisasa, masoko kwa ajili ya biashara nk. Kwakweli sisi tumeridhika sana na wizi huu!! Mungu amlaze mahala pema JPM, ametutoa tongotongo!!
10. Mwambieni CAG asipoteze nguvu zake bure kwa sababu hata hao wezi huwa hawafanywi kitu. Mwambieni tumezoea na zaidi tumeridhika na wizi au hasara za JPM. Mwambieni CAG nchi hii imeongozwa na wezi wengi lakini huyu alikua ni mwizi wa heshima. Tunampenda, tutammiss hivyohivyo na yeyote mwenye kumchafua atachafuka kwanza yeye. Tutakua Taifa la kijimga sana kuacha ALAMA za mtu huyu zifutwe na watu wajinga, wavivu
wasio na lolote walioachiwa Nchi wasiongoze wakihangaika na umbea, udaku na ushambenga.
Kwa taarifa yenu #SISI TUMERIDHIKA HATA ANGEIBA NCHI YOTE AIUZE!! Tuna macho ya kuona, tusichoshane.
#TutakukumbukaDaimaJPM.
MenukaJr,
Da'slam-Tanzania.
AmeeenHao marais wastaafu walikuwa wanakiri sio kwakuwa walikuwa wanakubali kama walivyosema , bali walikuwa wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Hivi ulitegemea waseme ukweli tofauti na alichokua anataka kusikia? Halafu usitake kuonyesha eti alikuwa anasafisha pori ndio watu wakaumia. Aliumiza watu kwa kutumia kundi lake la watu wasiojulikana kwa kuwateka, kuwaua, kupora fedha za watu kwa kuwabambikia kodi, kufanya mauaji, kaucha wananchi na vilema hasa wa upinzani ili anajisi uchaguzi. Kwa maneno marahisi jamaa alikuwa shetani, ndio maana Mungu akaamua kufanya mabadiliko bila damu kumwagika.
Hata kuagwa namna ile hakustahili.Alikuwa mtu katili sana hakuwa na sifa yakuwa kiongozi
Mbona ubaya wake ndo umetamalaki? ndo ujue watu walichoshwaNi kweli wapo watu walio umizwa unadhani kwa nini hata yeye binafsi aliwahi kutamka ''Mtanikumbuka kwa mema na si kwamabaya'' alijua wazi katika kufyeka njia iliyo kuwa poli lazima viumbe wengine wataumia. Kwa jinsi nchi ilipokuwa imefikia ilihitaji shujaa kufanikiwa na ndio maana marais wastaafu wanakiri kushindwa kuirejeshe nchi kwenye mstari wa kuanza kupiga hatua.
Ninalia tena msiba unaanza upya pale Mnapo nikumbusha enzi za kupishana angani! Mzee Kikwete alisafiri takribani safari za nje 421 kwa wastani wa siku tatu kila safari alikaa nje ya nchi kwa jumla ya siku 1263 katika miaka kumi, miaka 3 na miezi 4 hakuwepo nchini, ukiongeza siku zake za rikizo 28x10 = siku 280 ukijumlisha na miaka 3.4 unapata mzee hakuwepo ofisini kwa miaka 4 katika kumi, mwisho watu wakamwita Vasco da Gama wa Tanzania, ukiacha yeye mawaziri na watendaji wengine walikuwa wanapishana angani kwa safari za ulaya na nyingi zilikuwa za kwenda kuomba misaada kwa wafadhiri mpaka ya kujenge vyoo vya shule, hakuna tulichokuwa tunakiweza hadi kulipa mishara ya wafanyakazi wa serikali ilikuwa kitendawili '' kasungura kadogo.''
Ni kweli serikali haikuwa na hela za kuwahudumia raia wake kwani walikuwa hawakusanyi kodi misamaha ya kodi ilitamalaki nchi ikawa ya wapiga dili, misheni town misamiati ambayo leo imetoweka! Nakumbuka na bado nakumbuka bodi za wakurugenzi zikikaa nje ya nchi kudadavua ya nchini kwetu! mikataba inayotuhusu ikifungwa nje ya nchi bila ya kuwa na masilahi kwetu hakika zilikuwa enzi za bata bin batani kwa wale wasiofaidi wakati huo Mh.
Kwa sasa acheni tulinganishe kule na huku wapi tumefanikiwa ingawa ni kwa miaka mitano kwa kumi ya wenzi wake ni wapi tumefanikiwa zaidi kama taifa? Hili liko dhahili na hata wao Ma Rais wastaafu wanakili na walishakili mara nyingi kuwa mafanikio ya mwenda zake yameenda mbali kuliko vipindi vyao vya utawala kwani kati ya mengi yaliyowashinda yeye alifanikiwa kwa muda mfupi sana kuyapa ufumbuzi na nchi kuanza kupiga hatua za kimaendeleo. Amin amin nawaambia hakika mtamkumbuka kwa mema na si kwa mabaya.
Bado nakumbuka bajeti zetu za maendeleo na matumizi za kipindi kile, na alizoacha mwenda zake! napata shida moyoni je nitarejea kule au nitasonga mbele machozi yananitoka bado nalia na huenda nikalia zaidi, ila najipa moyo kwa kuwa mama alikuwepo jikoni wakati pishi hili likitengenezwa nina hakika anaijua njia sitarejea kwenye tembele la chukuchuku kwa kuwa eti sisi ni masikini, hatuna hela ya kununua viungo,msiba wangu utadumu milele kama mama atazisikiliza nyimbo za wapiga zumari wa eti ''umasikini wetu haushindiki''
Alafu hao wapiga deal ndio wana coordinate kumchafua JPM! Tumewashtukia! Watachafuka wao kwanza! Uzuri sabuni ya kuwachafua ipo ...MWAMBIENI CAG, SISI TUMERIDHIKA!!
1. Mwambieni CAG kwamba sisi wenyewe tumeridhika, tumezoea kuibiwa. Mwambieni tofauti ya wizi wa zamani na huu ni kwamba wizi wa sasa unafaida kwa Wananchi wala asiumize kichwa. Mwambieni sisi Wananchi hatuna tatizo na hasara au wizi uliofanyika wakati wa JPM. Sisi tumeridhika hivyohivyo kwa sababu tuna macho ya kuona!!
2. Mwambieni CAG kwamba tuliibiwa hapa kupitia EPA. Pesa bilioni 135 zikaliwa na watu wachache, wakati huo elimu bure ilikua bado kuja. Mikopo ya elimu ya juu ilikua ni songombingo kwa hiyo hatuoni hatari kuibiwa sasa huku elimu bure ikiwa imeanzishwa na mikopo ikitoka kwa wakati. Sisi tumeridhika kabisa na hasara au wizi wa JPM!!
3. Mwambieni CAG kwamba tuliibiwa hapa bilioni 300 Serikali ikilipa Makampuni hewa katika kashfa ya MEREMETA. Mwambieni hapakua na tatizo lolote na wakati huo bajeti ya Dawa ilikua chini ya bilioni 30 lakini sasa na wizi wa JPM umepandisha bajeti ya DAWA zaidi ya mara tisa; yaani bilioni 270. Mwambieni kwa wizi huu Mungu atupe nini? Tumeridhika sana na wizi wa JPM.
4. Mwambieni CAG kwamba tulishaibiwa sisi kwenye mauzauza ya uwekezaji wa Bulyanhulu na Buzwagi na hata leo hakuna maelezo ya yanayoeleweka. Kodi hazikulipwa na pesa zikapigwa na wajanja wachache. Wakati huo wote madini na migodi yote ilikua ni mali ya wawekezaji wasiolipa kodi, Wananchi ilikua ni marufuku kukaribia migodi katika nchi yao. Kama JPM ameiba halafu wananchi wanachimba madini wenyewe kwa uhuru, ninaumia kwamba atakua ameiba kidogo sana. Wizi wenye manufaa kwa umma una maana zaidi kuliko wizi usio na manufaa. Sisi tumezoea kuibiwa, lakini kwa huu wa JPM tumeridhika.
5. Mwambieni CAG kwamba sisi tumezoea kuibiwa. Tumeshaibiwa haswa, ilikuja hapa tukaibiwa katika Mkataba wa kijinga wa DOWANS. Nchi ikalipa bilioni 111 kwa sababu ya maslahi ya watu wachache. Wakati tunaibiwa kupitia DOWANS, Mv. Victoria ilikua inalaza watu siku mbili ziwani kwa ubovu wake. Maisha yao yalikua hatarini kila safari, leo JPM akiiba au akitutia hasara ya bilioni 60 huku Mv. Victoria ikiwa MPYA kuna tatizo gani? Meli mpya tele kuanzia ziwa Nyasa, Tanganyika na Bahari ya Hindi Kilwa. Tunapenda wizi wa namna hii, angeiba kabisa za kutosha akajenga nyumba nzuri kama wenzake, akamiliki magari za mizigo meupe kukuki na sheli za kumwaga. Au akamilika supermakert za Da'slam kama wenzake. Sisi kuibiwa tumezoea, wizi wa JPM una manufaa, tumeridhika.
6. Mwambieni CAG kuwa sisi tumezoea kuibiwa asijiumize bure na ma-press ya kutangaza vi-wizi vya kitoto hivyo. Tulipigwa hapa pesa TAKATIFU katika Mkataba maarufu wa RICHMOND ulioondoka na Serikali ya mwaka 2008 hadi sasa hakuna kilichofanyika. Wakati tukipigwa pesa za Richmond daraja la Mfugale lilikua halipo, Daraja la Ubungo (Kijazi Interchange) haikuwahi kufikiriwa, Daraja la Tanzanite (Salender) lilikua katika ndoto, lile la Busisi halikufikiriwa kabisa. Kama tumeibiwa leo na mambo yote haya yamefanyika mwambieni CAG sisi roho kwatu, tumeridhika riport zake tupa kule hatusikii la mwazini wala mnadi swala. Tumefunga masikio!!
7. Mwambieni CAG sio hata siku nyingi zilichotwa BOT bilioni 306 kwa kilichoitwa kashfa ya TEGETA ESCROW. Nchi ikaibiwa tena na wajanja wachache, wakabeba pesa kwenye masandarusi. Wakati tukiibiana bilioni 306 za Escrow umeme vijijini ulikua unaunganishwa kwa Tsh. 454,000 ila kwa wizi wa JPM umeme vijijini unaunganishwa kwa Tsh. 27,000; asilimia zaidi ya 70 umeme umefika vijijini. Wizi mzuri kiasi gani huu!? Sasa tunajenga megawati 2400 kutoka Bwawa la Nyerere ili umeme ushuke zaidi. Ingalikua uwezo ni wangu ningalimrudisha mtu huyu aendelee kuiba na kutia hasara zaidi kwa sababu wizi na hasara zake zina manufaa kwa watu. Mwambieni CAG sisi tumeridhika hivyohivyo, atuwache!!
8. Mwambieni CAG sisi tumewahi kuibiwa Twiga mzima akabebwa na shingo yake akaondoka zake. Hii nchi tunaibiana na Wanyama yeye anahangaika na vipesa vidogo vidogo vya matengenezo ya ATCL. Mwambieni wakati tukiibiana TWIGA upatikanaji wa maji Vijijini ulikua ni asilimia 47 na sasa kwa wizi na hasara za JPM upatikanaji wa Maji vijijini umefikia asilimia 70.1 huku mijini upatikanaji ukitoka asilimia 74 hadi 84. Ni mtu mjinga pekee anaweza kuchukizwa na wizi wa JPM, mwambieni CAG sisi tumeridhika tunatamani angekuwepo aibe tena. Hatutakagi ujinga!!
9. Mwambieni CAG kuwa tumeibiwa sana nchi hii. Wakati wote tuliibiwa huku Nchi ikiwa haina Ndege hai hata moja. Mwambieni leo tuna Ndege 11 za kwetu wenyewe. Hizo hasara za ATCL zisimuumize kichwa, hakuna biashara isiyo na hasara, JPM keshawawekea mtaji na heshima ni wajibu wao kutafuta akili za kupata faida sio kuua mtaji. Mwambieni CAG, sisi tunampenda mwizi anayeiba halafu akanunua Ndege kwa ajili ya Nchi nzima, akajenga reli ya kasi, stend kibao za kisasa, masoko kwa ajili ya biashara nk. Kwakweli sisi tumeridhika sana na wizi huu!! Mungu amlaze mahala pema JPM, ametutoa tongotongo!!
10. Mwambieni CAG asipoteze nguvu zake bure kwa sababu hata hao wezi huwa hawafanywi kitu. Mwambieni tumezoea na zaidi tumeridhika na wizi au hasara za JPM. Mwambieni CAG nchi hii imeongozwa na wezi wengi lakini huyu alikua ni mwizi wa heshima. Tunampenda, tutammiss hivyohivyo na yeyote mwenye kumchafua atachafuka kwanza yeye. Tutakua Taifa la kijimga sana kuacha ALAMA za mtu huyu zifutwe na watu wajinga, wavivu
wasio na lolote walioachiwa Nchi wasiongoze wakihangaika na umbea, udaku na ushambenga.
Kwa taarifa yenu #SISI TUMERIDHIKA HATA ANGEIBA NCHI YOTE AIUZE!! Tuna macho ya kuona, tusichoshane.
#TutakukumbukaDaimaJPM.
MenukaJr,
Da'slam-Tanzania.
Hata kuagwa namna ile hakustahili.
Wanalia na kusaga menoNia yao waendelee kuvuna wasichopanda lkn sasa wamegonga mwamba maana mfadhili wao hayupo tena.
Ukweli ni mwamba hata serikali ya jiwe ulichukua mikopo kutoka nje , sema ilifanya siriNi ya maendeleo na yeye anapaswa kupongezwa kwa hilo,na yapo mengi tu mazuri ya kikwete aliyoyafanya kadiri Mungu alivyomtunuku,ninachokiongea hapa si kuwa hawakufanya mema la hasha ila ninaogopa kurudi kwenye enzi ya kuhubiri umasikini na kuwa hatu wezi kila kitu mpaka waje wafadhiri, kuufanya umasikini kuwa kisingizio cha watu kutowajibika hapo ndipo namuona MAGU akijitokeza waziwazi mbele yangu.
Mwenda zake aliwahonga vyeo hao kina kijazi,mfugale,kicheere,na wengineo toka hiyo wizara ya ujenzi na miundo mbinu ili kuwafunga midomo.Hahaha
Mkuu mbona mikopo walichukua mingi tu?kwani deni la taifa lilipandaje?Wanalia na kusaga meno
Ukweli ni mwamba hata serikali ya jiwe ulichukua mikopo kutoka nje , sema ilifanya siri
Kuna siri moja watu hawaelewi kuhusu safari za nje ya nchi kwa mkuu wa nchi. Lazima emergency funds (si hela ya kitoto) ziwekwe kwenye account ya nje ya nchi. Kujiandaa chochote kikitokea ukiwa nje ya nchi… Na pia hii hela huwa hairudishwi hazina ikishatolewa. Tafakari….Ninalia tena msiba unaanza upya pale Mnapo nikumbusha enzi za kupishana angani! Mzee Kikwete alisafiri takribani safari za nje 421 kwa wastani wa siku tatu kila safari alikaa nje ya nchi kwa jumla ya siku 1263 katika miaka kumi, miaka 3 na miezi 4 hakuwepo nchini, ukiongeza siku zake za rikizo 28x10 = siku 280 ukijumlisha na miaka 3.4 unapata mzee hakuwepo ofisini kwa miaka 4 katika kumi, mwisho watu wakamwita Vasco da Gama wa Tanzania, ukiacha yeye mawaziri na watendaji wengine walikuwa wanapishana angani kwa safari za ulaya na nyingi zilikuwa za kwenda kuomba misaada kwa wafadhiri mpaka ya kujenge vyoo vya shule, hakuna tulichokuwa tunakiweza hadi kulipa mishara ya wafanyakazi wa serikali ilikuwa kitendawili '' kasungura kadogo.''
Ni kweli serikali haikuwa na hela za kuwahudumia raia wake kwani walikuwa hawakusanyi kodi misamaha ya kodi ilitamalaki nchi ikawa ya wapiga dili, misheni town misamiati ambayo leo imetoweka! Nakumbuka na bado nakumbuka bodi za wakurugenzi zikikaa nje ya nchi kudadavua ya nchini kwetu! mikataba inayotuhusu ikifungwa nje ya nchi bila ya kuwa na masilahi kwetu hakika zilikuwa enzi za bata bin batani kwa wale wasiofaidi wakati huo Mh.
Kwa sasa acheni tulinganishe kule na huku wapi tumefanikiwa ingawa ni kwa miaka mitano kwa kumi ya wenzi wake ni wapi tumefanikiwa zaidi kama taifa? Hili liko dhahili na hata wao Ma Rais wastaafu wanakili na walishakili mara nyingi kuwa mafanikio ya mwenda zake yameenda mbali kuliko vipindi vyao vya utawala kwani kati ya mengi yaliyowashinda yeye alifanikiwa kwa muda mfupi sana kuyapa ufumbuzi na nchi kuanza kupiga hatua za kimaendeleo. Amin amin nawaambia hakika mtamkumbuka kwa mema na si kwa mabaya.
Bado nakumbuka bajeti zetu za maendeleo na matumizi za kipindi kile, na alizoacha mwenda zake! napata shida moyoni je nitarejea kule au nitasonga mbele machozi yananitoka bado nalia na huenda nikalia zaidi, ila najipa moyo kwa kuwa mama alikuwepo jikoni wakati pishi hili likitengenezwa nina hakika anaijua njia sitarejea kwenye tembele la chukuchuku kwa kuwa eti sisi ni masikini, hatuna hela ya kununua viungo,msiba wangu utadumu milele kama mama atazisikiliza nyimbo za wapiga zumari wa eti ''umasikini wetu haushindiki''
Ilikuwa ni dili, subiri muda utasemaHata kuagwa namna ile hakustahili.
Wewe ni mtu mzimaaa au mtoto?Historia inawahukumu
New Member...........Ninalia tena msiba unaanza upya pale Mnapo nikumbusha enzi za kupishana angani! Mzee Kikwete alisafiri takribani safari za nje 421 kwa wastani wa siku tatu kila safari alikaa nje ya nchi kwa jumla ya siku 1263 katika miaka kumi, miaka 3 na miezi 4 hakuwepo nchini, ukiongeza siku zake za rikizo 28x10 = siku 280 ukijumlisha na miaka 3.4 unapata mzee hakuwepo ofisini kwa miaka 4 katika kumi, mwisho watu wakamwita Vasco da Gama wa Tanzania, ukiacha yeye mawaziri na watendaji wengine walikuwa wanapishana angani kwa safari za ulaya na nyingi zilikuwa za kwenda kuomba misaada kwa wafadhiri mpaka ya kujenge vyoo vya shule, hakuna tulichokuwa tunakiweza hadi kulipa mishara ya wafanyakazi wa serikali ilikuwa kitendawili '' kasungura kadogo.''
Ni kweli serikali haikuwa na hela za kuwahudumia raia wake kwani walikuwa hawakusanyi kodi misamaha ya kodi ilitamalaki nchi ikawa ya wapiga dili, misheni town misamiati ambayo leo imetoweka! Nakumbuka na bado nakumbuka bodi za wakurugenzi zikikaa nje ya nchi kudadavua ya nchini kwetu! mikataba inayotuhusu ikifungwa nje ya nchi bila ya kuwa na masilahi kwetu hakika zilikuwa enzi za bata bin batani kwa wale wasiofaidi wakati huo Mh.
Kwa sasa acheni tulinganishe kule na huku wapi tumefanikiwa ingawa ni kwa miaka mitano kwa kumi ya wenzi wake ni wapi tumefanikiwa zaidi kama taifa? Hili liko dhahili na hata wao Ma Rais wastaafu wanakili na walishakili mara nyingi kuwa mafanikio ya mwenda zake yameenda mbali kuliko vipindi vyao vya utawala kwani kati ya mengi yaliyowashinda yeye alifanikiwa kwa muda mfupi sana kuyapa ufumbuzi na nchi kuanza kupiga hatua za kimaendeleo. Amin amin nawaambia hakika mtamkumbuka kwa mema na si kwa mabaya.
Bado nakumbuka bajeti zetu za maendeleo na matumizi za kipindi kile, na alizoacha mwenda zake! napata shida moyoni je nitarejea kule au nitasonga mbele machozi yananitoka bado nalia na huenda nikalia zaidi, ila najipa moyo kwa kuwa mama alikuwepo jikoni wakati pishi hili likitengenezwa nina hakika anaijua njia sitarejea kwenye tembele la chukuchuku kwa kuwa eti sisi ni masikini, hatuna hela ya kununua viungo,msiba wangu utadumu milele kama mama atazisikiliza nyimbo za wapiga zumari wa eti ''umasikini wetu haushindiki''
Hili swali lako ilibidi liulizwe na robbotWewe ni mtu mzimaaa au mtoto?
Wewe ni mtu mwenye akili sawasawa au moja imetangulia Mbele
Au tu wewe ni mbishani?
Hii nchi sasa hivi inaye rais aliye madarakani hivyo nipende kuwashauri nyinyi mnaotaka kutuletea uhasama na mgawanyiko kwa manufaa yenu muache mara moja hiz tabia za kibinafsi.Wewe ni mtu mzimaaa au mtoto?
Wewe ni mtu mwenye akili sawasawa au moja imetangulia Mbele
Au tu wewe ni mbishani?
haya orodhesha mazuri yote ya kikwete .Kila binaadam ana mapungufu yake,lakini pia ni binaadam wa hatari sana asiyeweza kuthamini mema ya wengine kwa kisingizio cha ubaya ''yatupasa kushukuru kwa yote ndipo tunapoweza kupata kibari machoni pa bwana''
Let them provoke under the scene of freedom of expression cause non of your business.Are u okay Mango??!!!Natamani sana kumfahamu huyo mfqdhili wenu anaye isimamia hii show mwanzo mwisho!
Maana nyuzi za kumfagilia marehemu na kumponda JK, zimetamalaki sana humu jukwaani kutoka kwa members wapya kabisa!