No2..
Kuna siku mwaka jana kama mwezi wa nne hivi kama sio watano.. Nilienda kuna cafeteria moja hivi jirani na ofisini kwetu nikaagiza chai na chapati nikawa nakula taratibu, mara kidogo akaja mkaka mzuri kidogo handsome boy hatari tukakaa tumegeukiana..naye akaagiza maziwa na sambusa l ile ameanza kula akapigiwa Simu akapokea akawa anaongea huku anakula,. Mimi kitu ambacho sipendi ni kuongea wakati wa kula yaani nikiwa naangaliana na mtu hivi mda wakula halafu anaongea ongea najiskia kinyaa sana aisee
Asa bora angekua anaongea vizuri, anaongea kwa sauti halafu anatafuna kama nguruwe mdomo wote pembeni umejaa uchafu, mate yananirukia hatari pamoja na vipande vya sambusa nikawa namkazia tu macho na ishara kukwambia ananikera akawa anielewi, nikaangalia pembeni meza zote na viti vimejaa hamna pa kuhamia nayeye namkazia macho hata hawazi ndio kwanza anaendelea kuongea tena anajiachia na kucheka kabisaπ€π€.. Nilikasirika nikasimama nikapiga meza kwa nguvu kila mtu akaaa kimya nikachua chapati nikamrushia usoni, nikachukua chai nikamwagia usoni akamind anauliza wewe dada vipi nikamwambia kwa sauti mtu unatafuna kama nguruwe halafu unaongea ongea huoni kama unawatia kinyaa mwenzako.. Watu wakaanza kusema asa dada si ungesema tungejua tunakusaidiaje au ungemwambia tu, nikawaambia nimemwonesha ishara zote hajanielewa.. Mkaka mmoja akaanza kusema dada hizo dharau kabla hajamaliza nikamrushie kile kidude cha sukari kichwani aliumia, akataka kunifata nikanyanyua kiti nikamrushia nikakimbia nje kuna mwingine alikua ananawa mikono akataka kunishika nikamimina sabuni ya kunawia mikono nikampaka machoni kinakimbia mbio
Sikwenda ofisini nilirudi nyumbani moja kwa moja ππ