Niambie ni mambo gani ya ajabu ulishawahi kufanya ukiwa na hasira hadi ukikumbuka unaweza kucheka na kujionea aibu kwa wakati mmoja...

Kadada unajua hadi kupiga mateke,🀣🀣
 
Hata bomu huwa ni tulivu sana hadi lirushwe ndio mtiti wake huonekana...

Kama ulichoandika ni kweli basi una shida ya mizimu, mapepo au majini...

Ipo siku utayapa kitu wanachotaka, damu ya mtu...
Hapana mkuu. Hii ni religious indoctrination

Ajifunze tu kudhibiti hasira
 
Hata bomu huwa ni tulivu sana hadi lirushwe ndio mtiti wake huonekana...

Kama ulichoandika ni kweli basi una shida ya mizimu, mapepo au majini...

Ipo siku utayapa kitu wanachotaka, damu ya mtu...
Mkuu sidhani kama ni mapepo, maana wakati Niko shule nilikua naenda kusali makanisa ya walokole na sikuwahi kuangukaπŸ€”πŸ€”
 
Mwaka 2022 mwishoni nilimkopesha broda wangu shilingi mil 1.7 kwa ahadi ya kwamba atarudisha baada ya mwez mmoja. Mwezi umekamilika na offcoz nilikuwa nashida nayo sana ile pesa kwa wakati ule, nilipoona yupo kimya ikabidi nimkumbushe ila alinijibu kwamba hanilipi kwasababu alitumia pesa nyingi kunisomesha mpka kufika hapa nilipo. Yale majibu yalinipandisha hasira na ukizngatia nilikuwa namikwamo yangu kwa muda ule basi nilipita kijiweni nikamchukuwa mshikaji wangu ni boda boda jamaa kapiga kibuyu mpka kwa broda uzuri hakuwepo alikuwa kasafr kidogo kwahiyo nilimkuta shemej na chalii yake wa kike. Wazee nilisalimia kisha nikaanza kuzungusha macho pale seblen nikaangaza nikaona chakuchukua fasta fasta ni mtv ulikuwa ni Samsung 53' sound bar ya Sony na laptop mac book then nikasepa japo mzigo ulitusumbua njiani lakini ulifika salama. Ile nipo njiani simu zikaanza kuita lakini sikuokota mpka nilipofika kwangu nikamwambia bro nakupa masaa 24 pesa iwe ishawekwa bank lasivo nauza, sitapokea simu zako mpka nipate mesej ya crdb. Oya kesho yake mida ya saa 4 asubuhi napata mesej kiasi cha tsh 1.7 mil kimewekwa kwenye acc yako inayoishia na Γ—Γ—Γ— nikasema mambo si ndo haya. Nikaitoa fasta nikasov mambo yangu then nkamchek boda boda tukarudsha mazaga maisha yakaendelea na mpka sasa tupo powa tu lakini baadae nilikaa nikajutia nlichokifanya japo kilinisaidia kupata pesa na kusov mambo yangu
 
Sidhani kama ulifanya kosa mkuu.. sometimes watu wanatakiwa kujua upande wetu wa pili ukoje ili waache kutuchukulia poa.. Nadhani huyo bro wako hata ikitokea safari nyingine akakuazima pesa atakua na discipline kwenye kukurudishia
 
Nimesoma Visa vyako, hakika vinafurahisha.

Kwa Ushauri, naomba uridhie ile Posa iliyoletwa kwaajili yako Wazee tuipokee japo haijafikia lengo 😜.

Maana tukikuacha uendeleze hivyo Mjukuu bila Mchumba utakuja kutupiga Mtaa Mzima πŸƒπŸƒπŸƒπŸƒ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…