Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jirani kila nikijitahidi kuamini ubongo na macho vinabishana 🤣🤣🤣Halafu unaweza hisi ni chai😂😂.. Lakini haina shida nimeiweka chit chat 😃
Hivi wewe Joanah ndiye wewe kwenye avatarNimeangalia uzi upo jukwaa gani nikaelewa logic ya roba,makofi na mateke [emoji23]
Weee Leejay49 huyu ni wewe unayefanya haya yote?😂😂😂No2..
Kuna siku mwaka jana kama mwezi wa nne hivi kama sio watano.. Nilienda kuna cafeteria moja hivi jirani na ofisini kwetu nikaagiza chai na chapati nikawa nakula taratibu, mara kidogo akaja mkaka mzuri kidogo handsome boy hatari tukakaa tumegeukiana..naye akaagiza maziwa na sambusa l ile ameanza kula akapigiwa Simu akapokea akawa anaongea huku anakula,. Mimi kitu ambacho sipendi ni kuongea wakati wa kula yaani nikiwa naangaliana na mtu hivi mda wakula halafu anaongea ongea najiskia kinyaa sana aisee
Asa bora angekua anaongea vizuri, anaongea kwa sauti halafu anatafuna kama nguruwe mdomo wote pembeni umejaa uchafu, mate yananirukia hatari pamoja na vipande vya sambusa nikawa namkazia tu macho na ishara kukwambia ananikera akawa anielewi, nikaangalia pembeni meza zote na viti vimejaa hamna pa kuhamia nayeye namkazia macho hata hawazi ndio kwanza anaendelea kuongea tena anajiachia na kucheka kabisa🤒🤒.. Nilikasirika nikasimama nikapiga meza kwa nguvu kila mtu akaaa kimya nikachua chapati nikamrushia usoni, nikachukua chai nikamwagia usoni akamind anauliza wewe dada vipi nikamwambia kwa sauti mtu unatafuna kama nguruwe halafu unaongea ongea huoni kama unawatia kinyaa mwenzako.. Watu wakaanza kusema asa dada si ungesema tungejua tunakusaidiaje au ungemwambia tu, nikawaambia nimemwonesha ishara zote hajanielewa.. Mkaka mmoja akaanza kusema dada hizo dharau kabla hajamaliza nikamrushie kile kidude cha sukari kichwani aliumia, akataka kunifata nikanyanyua kiti nikamrushia nikakimbia nje kuna mwingine alikua ananawa mikono akataka kunishika nikamimina sabuni ya kunawia mikono nikampaka machoni kinakimbia mbio
Sikwenda ofisini nilirudi nyumbani moja kwa moja 😆😆
😂 jiraaaani naona kama ndotoJirani kila nikijitahidi kuamini ubongo na macho vinabishana 🤣🤣🤣
😂😂😂 Jifinye ushtuke😂 jiraaaani naona kama ndoto
Njoo unifinye 😂😂😂😂 Jifinye ushtuke
Itakua jamaa uliyemmwagia chai.Yaani we acha tu mkuu.. Sijawahi kwenda tena pale na sijui nani alilipiaga bill zile😂😂
ulimkatili mtoto wa watu bure asie na hatia na inavyowashaga.No4..
Kuna rafiki yangu mmoja nilisomaga nae olevel, ana mtoto saizi ..namdai hela yangu ya mda hadi leo bado hajanilipaga hadi nimeamua nimsamehe tu sasa maana sina namna....
Mwanzo wakati deni bado bichi bichi halijawa sugu, kuna siku nilikua sina hata buku nikasema ngoja nikamdai, nyumbani kwetu na kwao sio mbali unapita nyumba kama sita tu hivi unavuka barabara nyumba yao ipo barabarani tu.. Mama yake pale nje anauza supu, chapati, sambusa, kachori na vitu kama hivyo yani pamechangamka kiasi...
Nimefika hadi pale nikaongea nae kuhusu ile hela akaniambia hana, nikamkazia mimi sina hata hela leo naomba unilipe akanibembeleza pale akaniambia hana nimwongezee siku atanilipa.. Basi bwana nikaishiwa pozi nikabaki tu naangalia nae TV maana nilichoka mwili roho hadi nafsi,, mda wote huo si tupo ndani mama yake alikua kule nje na shughuli zake, nyingine., Kulikua na wateja wengi wengi kidogo akamwita akaenda kumsaidia kuwahudumia, Kochi nililokua nimekaa mimi lipo kwa upande wa dirisha linaloangalia pale nje kibarazani, na madirisha yao hayana vioo ni waya tu ule wa mbu basi...
Bwana wee mimi na umbea wangu si nikasikia walivyokua wanaongea, mama yake akamuuliza " kwani Lee hadi leo bado hujamlipa hela yake ile,??".. Yeye akajibu " Unadhani nitampa leo au kesho?, hiyo asahau, hana shida na hela huyo, ilikua gear tu ya kuja kuniona hana lolote "". Mama yake akacheka na yeye akacheka,, Aisee nilipatwa na hasira nikasema huyu ndo wakunifanyia mimi hivi kweli... Nikapiga hesabu za haraka haraka nikaona sina cha kumfanya
Kabla sijakata tamaa kichaa changu kikapanda, nilikua na mtoto wake ndani mle ni kidogo tu kinatambaa bado ndo kinajifunza kusimama,, mezani kwao kulikua na chili halafu haijafungwa vizuri nikasema hii itanifaa sana.. Nikamnyanyua mtoto nikamsogeza karibu na mguu wa meza, meza yenyewe mbovu mbovu halafu fupi, nikafungua chili nikamwagia kwenye paji la uso nikaacha inamshukia taratibu taratibu machoni, nikamshikisha mkononi kopo la chili huku limeinama.. nikarudi kwenye kochi nikajifanya niko busy na simu kama sio mimi vile,, huwezi amini ilipita kama dakika moja tu mama yake huyo rafiki yangu akaingia ndani.. niliogopa lakini hakuniona😥😥
Akaanza kumfokea mwanae yani unajua mtoto alivyo na fujo halafu unamwacha tu njoo ona alichokifanya, na mimi nikajifanya nashangaa shangaa, mtoto alikua analia hatari.. nikazugazuga nikaaga kuondoka nikaacha wapo wanahangaika na mtoto..
Hili tukio nalijutia sana aisee Mungu tu anisamehe🙏🤦♀️🤦♀
Nadhani leo tuishie hapa wapendwa
Kwamba ni chai😃😂Nimeangalia uzi upo jukwaa gani nikaelewa logic ya roba,makofi na mateke 😂
Aisee😃😂, usi kute mna gombea kuweka Kati ya dragon Ball z na ben 10 😃😂Nilikua nagombania remote na dogo nikampiga mpaka akajikojolea🤣
Hadi leo mama anaamini namchukia dogo