Niambie ni mambo gani ya ajabu ulishawahi kufanya ukiwa na hasira hadi ukikumbuka unaweza kucheka na kujionea aibu kwa wakati mmoja...

Niambie ni mambo gani ya ajabu ulishawahi kufanya ukiwa na hasira hadi ukikumbuka unaweza kucheka na kujionea aibu kwa wakati mmoja...

No2..
Kuna siku mwaka jana kama mwezi wa nne hivi kama sio watano.. Nilienda kuna cafeteria moja hivi jirani na ofisini kwetu nikaagiza chai na chapati nikawa nakula taratibu, mara kidogo akaja mkaka mzuri kidogo handsome boy hatari tukakaa tumegeukiana..naye akaagiza maziwa na sambusa l ile ameanza kula akapigiwa Simu akapokea akawa anaongea huku anakula,. Mimi kitu ambacho sipendi ni kuongea wakati wa kula yaani nikiwa naangaliana na mtu hivi mda wakula halafu anaongea ongea najiskia kinyaa sana aisee
Asa bora angekua anaongea vizuri, anaongea kwa sauti halafu anatafuna kama nguruwe mdomo wote pembeni umejaa uchafu, mate yananirukia hatari pamoja na vipande vya sambusa nikawa namkazia tu macho na ishara kukwambia ananikera akawa anielewi, nikaangalia pembeni meza zote na viti vimejaa hamna pa kuhamia nayeye namkazia macho hata hawazi ndio kwanza anaendelea kuongea tena anajiachia na kucheka kabisa[emoji855][emoji855].. Nilikasirika nikasimama nikapiga meza kwa nguvu kila mtu akaaa kimya nikachua chapati nikamrushia usoni, nikachukua chai nikamwagia usoni akamind anauliza wewe dada vipi nikamwambia kwa sauti mtu unatafuna kama nguruwe halafu unaongea ongea huoni kama unawatia kinyaa mwenzako.. Watu wakaanza kusema asa dada si ungesema tungejua tunakusaidiaje au ungemwambia tu, nikawaambia nimemwonesha ishara zote hajanielewa.. Mkaka mmoja akaanza kusema dada hizo dharau kabla hajamaliza nikamrushie kile kidude cha sukari kichwani aliumia, akataka kunifata nikanyanyua kiti nikamrushia nikakimbia nje kuna mwingine alikua ananawa mikono akataka kunishika nikamimina sabuni ya kunawia mikono nikampaka machoni kinakimbia mbio
Sikwenda ofisini nilirudi nyumbani moja kwa moja [emoji38][emoji38]
Utakuja uvunjwe kwa kipigo
 
Yy alikuwa na mnyororo wa wanaume ile kila mwanaume hamkatai, mm nlikuwa na waschana 3 wote hawajuani but yeye alikuwa anawajua wote coz nlimwambia
Masikini, Lengo lako lilikua kumuumiza mdada wa watu makusudi tu😥🤒
 
Hizo hasira zako za kingese huja fokonyolewa vizuri ndio maana njoo uniletee huo usokwe wako uone kama utabaki salama
Watu mna makasiriko😃😃.. Unahisi labda sina wazazi au ndugu wa karibu au mimi mwenyewe labda siwezi kujishughulikia??.. Halafu sijaomba ushauri ni vile tu nimeshare situations zinazonikutaga nikiwa na hasira.. Kuna ambao wanafanya makubwa zaidi ya haya yangu mkuu ni vile tu confidence ndo tatizo
 
Watu huwa wanashindwa kutofautisha ni wakati gani nipo kawaida na wakati gani nina hasira/nimechukia muda wote wananiona na sura ya upole na hicho ndo huwa kinawaponza na ninawaumiza.

Niliwahi kumpiga mtu mzima mwenye umri sawa na baba yangu kwenye daladala nilimkanyaga bahati mbaya akanitukana na kunidhalilisha namuomba samahani ye akawa anaendelea kunitukana mimi joto likaanza kupanda taratibu ye hajui daladala ilivyosimama nikamkaba nikashuka nae nilimpiga jab moja tu akapepesuka akaegemea gari ikafata teke ya tumbo akaanguka chini.

Konda akaja kinizuia nikamsukuma nikavuka upande wa pili nikapanda bodaboda nikaondoka eneo la tukio kabla watu hawajajaa ila kile kitendo huwa nakijutia ningemfahamu mzee yule ningeenda kumuomba radhi.
 
Back
Top Bottom