Niambie ni mambo gani ya ajabu ulishawahi kufanya ukiwa na hasira hadi ukikumbuka unaweza kucheka na kujionea aibu kwa wakati mmoja...

Watu huwa wanashindwa kutofautisha ni wakati gani nipo kawaida na wakati gani nina hasira/nimechukia muda wote wananiona na sura ya upole na hicho ndo huwa kinawaponza na ninawaumiza.

Niliwahi kumpiga mtu mzima mwenye umri sawa na baba yangu kwenye daladala nilimkanyaga bahati mbaya akanitukana na kunidhalilisha namuomba samahani ye akawa anaendelea kunitukana mimi joto likaanza kupanda taratibu ye hajui daladala ilivyosimama nikamkaba nikashuka nae nilimpiga jab moja tu akapepesuka akaegemea gari ikafata teke ya tumbo akaanguka chini.

Konda akaja kinizuia nikamsukuma nikavuka upande wa pili nikapanda bodaboda nikaondoka eneo la tukio kabla watu hawajajaa kile kitendo huwa nakijutia ningemfahamu mzee yule ningeenda kumuomba radhi.
Yaani hii statement inaumiza sana... I can feel you 😥😥
 
Kwa kweli muombe sana Mungu
Hiyo ni hatari..kemea roho za hasira kupita kiasi.

Hata maandiko yanasema mwe na hasira lakini msitende dhambi.

Unapiga hadi manesi😂🙌
Si wanaweza kukuua na misindano .
Serious itakuja kunicost.. Naomba Mungu anisaidie sana, hasira ni mbaya sana na ninazichukia mnoo
 
Kwa kweli muombe sana Mungu
Hiyo ni hatari..kemea roho za hasira kupita kiasi.

Hata maandiko yanasema mwe na hasira lakini msitende dhambi.

Unapiga hadi manesi😂🙌
Si wanaweza kukuua na misindano .
Mungu mwema, naimani atafanya🙏
My friend ile hospitali sitakuja nikanyage tena naogopa nisijechomwa sindano za sumu nife😥😂😂
 
Pole sana.

Sijasoma kote, kama kuna ambao tayari wameshakupa ushauri basi ni vizuri. Kwanza tambua ya kuwa, hasira si kitu kizuri na wala hupaswi kujivunia.

Neno la Mungu linasema hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu.

Mpumbavu kwa tafsiri hapo juu, ni mtu asiyeweza kujidhibiti hisia zake, asiyejali uhai wake na mwenzake. Mtu asiye na uono wa majuto ya vitendo vitokanavyo na hasira zake.

Kwanza, hebu ikatae. Usiseme hasira zangu, wala joto langu wala mapepo yako. Usijiambatanishe na hasira. Hasira isiwe yako. Kuanzia leo kemea ikae mbali nawe. Huna hasira yako, bali shetani anatumia udhaifu wako wa kushindwa kujidhibiti kukushurutisha kufanya mambo ya ajabu.

Pili, tambua ya kuwa hii dunia imejaa maudhi. Na maudhi hayo ndiyo maisha halisi. Ukiudhika hebu vuta hewa, jitafakari hatua unayotaka kuichukua ina madhara gani kwako na mhusika? Imagine bibi wa watu kule hospital, umrukie na kumnyonga ukute ana magonjwa yake ya moyo na presha. Afe, mpaka ije ifahamike ni kifo cha kutokusudia umeshapoteza muelekeo.

Hasira ni pepo. Hukuwa na nguvu, ila ghafla umepata nguvu nyingi na kuanza kutandika watu.

Tatu, hasira ikikupanda tafuta alternative kuliko kutaka kulipiza watu kwa maumivu. Amua kupuuzia. Potezea, haikupunguzii chochote.

Nne, ukikaa baadae na kujitafakari ulichokifanya wala usicheke. Jutia na umia. Kaombe msamaha uliowadhuru. Kawaambie ni hasira na hukulenga kufanya hivyo.

Tano, omba sana Mungu. Muombe kwa bidii yote. Akuondolee na huo udhaifu unaoumiza. Yeye atakuwezesha.

Kila la kheri.
 
Thank you Dr Restart , I do like your positivity😥... Stay blessed always 🙏🙏
 
Hatari sana😂
Huwezi jua wanakuwazia Nini hao manesi.

Try to control your temper
Siyo lazima ureact kwa kila kitu,vitu vingine vipuuze tu..
Kisasi ni juu ya Bwana.

Akikukera mtu wewe msukumize tu kwa Mungu,endelea na mambo Yako.
Mungu atalipa mwenyewe kwa kipimo chake ,na kwa wakati wake.

Shetani anaweza tumia lango la hasira kuleta uharibifu..

Mungu akusaidie.
Mungu mwema, naimani atafanya🙏
My friend ile hospitali sitakuja nikanyage tena naogopa nisijechomwa sindano za sumu nife😥😂😂
 
Hatari sana😂
Huwezi jua wanakuwazia Nini hao manesi.

Try to control your temper
Siyo lazima ureact kwa kila kitu,vitu vingine vipuuze tu..
Kisasi ni juu ya Bwana.

Akikukera mtu wewe msukumize tu kwa Mungu,endelea na mambo Yako.
Mungu atalipa mwenyewe kwa kipimo chake ,na kwa wakati wake.

Shetani anaweza tumia lango la hasira kuleta uharibifu..

Mungu akusaidie.
Na ikawe hivyo kwakweli
 
Back
Top Bottom