No4..
Kuna rafiki yangu mmoja nilisomaga nae olevel, ana mtoto saizi ..namdai hela yangu ya mda hadi leo bado hajanilipaga hadi nimeamua nimsamehe tu sasa maana sina namna....
Mwanzo wakati deni bado bichi bichi halijawa sugu, kuna siku nilikua sina hata buku nikasema ngoja nikamdai, nyumbani kwetu na kwao sio mbali unapita nyumba kama sita tu hivi unavuka barabara nyumba yao ipo barabarani tu.. Mama yake pale nje anauza supu, chapati, sambusa, kachori na vitu kama hivyo yani pamechangamka kiasi...
Nimefika hadi pale nikaongea nae kuhusu ile hela akaniambia hana, nikamkazia mimi sina hata hela leo naomba unilipe akanibembeleza pale akaniambia hana nimwongezee siku atanilipa.. Basi bwana nikaishiwa pozi nikabaki tu naangalia nae TV maana nilichoka mwili roho hadi nafsi,, mda wote huo si tupo ndani mama yake alikua kule nje na shughuli zake, nyingine., Kulikua na wateja wengi wengi kidogo akamwita akaenda kumsaidia kuwahudumia, Kochi nililokua nimekaa mimi lipo kwa upande wa dirisha linaloangalia pale nje kibarazani, na madirisha yao hayana vioo ni waya tu ule wa mbu basi...
Bwana wee mimi na umbea wangu si nikasikia walivyokua wanaongea, mama yake akamuuliza " kwani Lee hadi leo bado hujamlipa hela yake ile,??".. Yeye akajibu " Unadhani nitampa leo au kesho?, hiyo asahau, hana shida na hela huyo, ilikua gear tu ya kuja kuniona hana lolote "". Mama yake akacheka na yeye akacheka,, Aisee nilipatwa na hasira nikasema huyu ndo wakunifanyia mimi hivi kweli... Nikapiga hesabu za haraka haraka nikaona sina cha kumfanya
Kabla sijakata tamaa kichaa changu kikapanda, nilikua na mtoto wake ndani mle ni kidogo tu kinatambaa bado ndo kinajifunza kusimama,, mezani kwao kulikua na chili halafu haijafungwa vizuri nikasema hii itanifaa sana.. Nikamnyanyua mtoto nikamsogeza karibu na mguu wa meza, meza yenyewe mbovu mbovu halafu fupi, nikafungua chili nikamwagia kwenye paji la uso nikaacha inamshukia taratibu taratibu machoni, nikamshikisha mkononi kopo la chili huku limeinama.. nikarudi kwenye kochi nikajifanya niko busy na simu kama sio mimi vile,, huwezi amini ilipita kama dakika moja tu mama yake huyo rafiki yangu akaingia ndani.. niliogopa lakini hakuniona😥😥
Akaanza kumfokea mwanae yani unajua mtoto alivyo na fujo halafu unamwacha tu njoo ona alichokifanya, na mimi nikajifanya nashangaa shangaa, mtoto alikua analia hatari.. nikazugazuga nikaaga kuondoka nikaacha wapo wanahangaika na mtoto..
Hili tukio nalijutia sana aisee Mungu tu anisamehe🙏🤦♀️🤦♀
Nadhani leo tuishie hapa wapendwa