Niambie ni mambo gani ya ajabu ulishawahi kufanya ukiwa na hasira hadi ukikumbuka unaweza kucheka na kujionea aibu kwa wakati mmoja...

Niambie ni mambo gani ya ajabu ulishawahi kufanya ukiwa na hasira hadi ukikumbuka unaweza kucheka na kujionea aibu kwa wakati mmoja...

Wee usiniambie Hadi ya bwana shemeji ulikua unachangamsha gengeπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜ƒπŸ€­
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Hata ya kutafuta mwenza sikua serious na walikua wakija PM nilikua nawashangaa how comes walichukulia serious nyuzi nilizoandika kwa matani mengi ndani yake.

The only non-fiction ni ile miamala tu.πŸ˜‚πŸ˜ na hata sasa bado inatiririka coz my God is good
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Hata ya kutafuta mwenza sikua serious na walikua wakija PM nilikua nawashangaa how comes walichukulia serious nyuzi nilizoandika kwa matani mengi ndani yake.

The only non-fiction ni ile miamala tu.πŸ˜‚πŸ˜ na hata sasa bado inatiririka coz my God is good
Hilo ndo la msingi,,
Humu watu wako serious na maisha Hadi sio poa.
Just imagine Kuna watu wananifanyia counselling wakati Uzi uko chit chats πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Babu kwa hasira hizi unadhani nitaweza kuhimili wivu mtoto wa mtu akinicheat kweli?. Au unataka nikaozee segereaπŸ˜ƒ
Hahaha.......hizo hasira zinaisha Mjukuu ukiwa unapewa morning glory.

Automatic utajikuta uko happy kila Siku kila saa as mwili unakuwa mwepesi Kwa huduma πŸ«£πŸƒπŸƒπŸƒπŸƒ
 
Ungeweka wazi kwamba ulicho andika ni Utani,hakina ukweli mkuu. Kushauri siyo jambo baya. Take it positively,watu wanakupenda
I understand,, na Ni matukio ambayo nimeyafanya lakini watu wamechukulia serious kupitiliza.. I mean wameover think...
I didn't seek for any advice Ndomana nikaweka kwenye jukwaa la chit chats,, najua namna ya kujishughulikia
Anyways thanks πŸ™
 
Happy new year wananzengo
Leo nimetoka kufanya tukio moja hadi nimekaa hapa najitafakari naishia tu kujionea aibu hadi naandika uzi hapa saa hii....

Kwanza kabisa mimi ni mtu mmoja hivi mtulivu sana nyuma ya keyboard, yaani ni mpole mnoo.. Ni aina ya watu ambao hua nakua vibe nikiwa alone, either ofisini au nikiwa chumbani kwangu alone, yaani naweza nikawa na tamasha la kipekeyangu nikaimba na kucheza miziki yote unayoijua kuanzia rhumba, bongo flavor, amapiano, hadi za gospel ilimradi tu zina vibe.. Au sometimes naweza nikawa najifanyia fashion show navaa nguo zote najipakaa makeup natembea kuzunguka chumba kizima with good music..Lakini yote hayo nafanya nikiwa alone,, Yaani nikiwa nje na chumbani au ofisini kwangu nakua mtu wa tofauti kabisa and nobody knows ninayoyafanyaga nikiwa alone[emoji38][emoji38][emoji38]

Back to the topic... Mimi Leejay nina hasira za karibu mno kiasi kwamba sijawahi kujizuia nikikwazika, yaani mtu akiniudhi naweza kufanya kitu kila mtu anabaki anajiuliza hivi ni huyu kweli au amepandwa na mashetani au ni kitu gani... Nitasimulia mojamoja ambayo nimeyafanya tu mwaka jana na mwaka huu hadi leo maana ni Mengi mno..

No.1
Ilikua mwaka jana kama mwezi wa pili hivi., Nilishikwa na tumbo vidonda vilichachamaa hatari hadi kutembea nilikua siwezi nikabebwa hadi kufika hospitali napita kutapika njia nzima.., tukafika na hali niliyokua nayo ilibidi wagonjwa wote wanipishe kwanza mimi niingie kwa daktari.. nikaanza kuulizwa ulizwa pale mama akawa anatoa maelezo mimi nikiwa siwezi kukaa vizuri nahangaika tu pale kitandani natapika kwelikweli... Asa mle ndani ukiachana na doctor kulikua pia na Manesi wawili mmoja ni mtu mzima kidogo around 42 hivi na mwingine ana kama 26 hivi hadi 28... Yule mdogo nikasikia anamwambia yule mmama, ""Hawa mabinti hawana akili kabisa yaani usikute hapo kuhangaika kote huko ametoa mimba halafu anawasumbua tu baba na mama yake saizi asubuhi yote hii "", Yule mmama akasema unadhani mi siwajui hawa, ukute ni Nyege tu zinamsumbua hana lolote....
Aisee nilikasirika nikashindwa kujizuia nikanyanyuka nikamrukia yule mama teke akaanguka chini ameduwaa nikanyanyuka nimemkunja roba yule mwingine huku natetemeka mishipa ya kichwa imenisimama naongea kwa ukali mnasemaje nyinyi.... Wanajifanya kushangangaa huyu vipi??, nikamwachia mkono mmoja nikamtandika makofi huku ninatetemeka jasho mwili mzima[emoji38][emoji38][emoji38] hapo yule mmama amengukia kwenye ndoo nadhani ilikua na maji machafu sijui alikua anadeki bado hata sikumbuki,,. ile nataka nimfate yule mama dokta na mama wakanishika mikono wanawauliza kwani nyie mmemfanya nini wanaanza kubabaika wanasema uongo nikasimama tena kwa nguvu nikawa na wafata yule mama akakimbilia nje akabaki mdogo nikataka kumpiga teke akakwepa matapishi yalijaa mdomoni nikatemea yote usoni...
Baada ya pale sikuelewa nini kiliendelea nakuja kustuka niko wodini baba angu anacheka hana mbavu sikutaka hata kuuliza kimetokea nini nikajigeuzia upande mwingine nikalala, ila wakati niko mle ndani niliona tu manensi wakionyeshana ndo huyu ndo huyu hata sikuuliza chochote nikikumbuka nacheka tu mwenyewe
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]hii nimeipenda
 
No2..
Kuna siku mwaka jana kama mwezi wa nne hivi kama sio watano.. Nilienda kuna cafeteria moja hivi jirani na ofisini kwetu nikaagiza chai na chapati nikawa nakula taratibu, mara kidogo akaja mkaka mzuri kidogo handsome boy hatari tukakaa tumegeukiana..naye akaagiza maziwa na sambusa l ile ameanza kula akapigiwa Simu akapokea akawa anaongea huku anakula,. Mimi kitu ambacho sipendi ni kuongea wakati wa kula yaani nikiwa naangaliana na mtu hivi mda wakula halafu anaongea ongea najiskia kinyaa sana aisee
Asa bora angekua anaongea vizuri, anaongea kwa sauti halafu anatafuna kama nguruwe mdomo wote pembeni umejaa uchafu, mate yananirukia hatari pamoja na vipande vya sambusa nikawa namkazia tu macho na ishara kukwambia ananikera akawa anielewi, nikaangalia pembeni meza zote na viti vimejaa hamna pa kuhamia nayeye namkazia macho hata hawazi ndio kwanza anaendelea kuongea tena anajiachia na kucheka kabisa[emoji855][emoji855].. Nilikasirika nikasimama nikapiga meza kwa nguvu kila mtu akaaa kimya nikachua chapati nikamrushia usoni, nikachukua chai nikamwagia usoni akamind anauliza wewe dada vipi nikamwambia kwa sauti mtu unatafuna kama nguruwe halafu unaongea ongea huoni kama unawatia kinyaa mwenzako.. Watu wakaanza kusema asa dada si ungesema tungejua tunakusaidiaje au ungemwambia tu, nikawaambia nimemwonesha ishara zote hajanielewa.. Mkaka mmoja akaanza kusema dada hizo dharau kabla hajamaliza nikamrushie kile kidude cha sukari kichwani aliumia, akataka kunifata nikanyanyua kiti nikamrushia nikakimbia nje kuna mwingine alikua ananawa mikono akataka kunishika nikamimina sabuni ya kunawia mikono nikampaka machoni kinakimbia mbio
Sikwenda ofisini nilirudi nyumbani moja kwa moja [emoji38][emoji38]
Mmh kumbe sensia
 
No4..
Kuna rafiki yangu mmoja nilisomaga nae olevel, ana mtoto saizi ..namdai hela yangu ya mda hadi leo bado hajanilipaga hadi nimeamua nimsamehe tu sasa maana sina namna....
Mwanzo wakati deni bado bichi bichi halijawa sugu, kuna siku nilikua sina hata buku nikasema ngoja nikamdai, nyumbani kwetu na kwao sio mbali unapita nyumba kama sita tu hivi unavuka barabara nyumba yao ipo barabarani tu.. Mama yake pale nje anauza supu, chapati, sambusa, kachori na vitu kama hivyo yani pamechangamka kiasi...
Nimefika hadi pale nikaongea nae kuhusu ile hela akaniambia hana, nikamkazia mimi sina hata hela leo naomba unilipe akanibembeleza pale akaniambia hana nimwongezee siku atanilipa.. Basi bwana nikaishiwa pozi nikabaki tu naangalia nae TV maana nilichoka mwili roho hadi nafsi,, mda wote huo si tupo ndani mama yake alikua kule nje na shughuli zake, nyingine., Kulikua na wateja wengi wengi kidogo akamwita akaenda kumsaidia kuwahudumia, Kochi nililokua nimekaa mimi lipo kwa upande wa dirisha linaloangalia pale nje kibarazani, na madirisha yao hayana vioo ni waya tu ule wa mbu basi...
Bwana wee mimi na umbea wangu si nikasikia walivyokua wanaongea, mama yake akamuuliza " kwani Lee hadi leo bado hujamlipa hela yake ile,??".. Yeye akajibu " Unadhani nitampa leo au kesho?, hiyo asahau, hana shida na hela huyo, ilikua gear tu ya kuja kuniona hana lolote "". Mama yake akacheka na yeye akacheka,, Aisee nilipatwa na hasira nikasema huyu ndo wakunifanyia mimi hivi kweli... Nikapiga hesabu za haraka haraka nikaona sina cha kumfanya
Kabla sijakata tamaa kichaa changu kikapanda, nilikua na mtoto wake ndani mle ni kidogo tu kinatambaa bado ndo kinajifunza kusimama,, mezani kwao kulikua na chili halafu haijafungwa vizuri nikasema hii itanifaa sana.. Nikamnyanyua mtoto nikamsogeza karibu na mguu wa meza, meza yenyewe mbovu mbovu halafu fupi, nikafungua chili nikamwagia kwenye paji la uso nikaacha inamshukia taratibu taratibu machoni, nikamshikisha mkononi kopo la chili huku limeinama.. nikarudi kwenye kochi nikajifanya niko busy na simu kama sio mimi vile,, huwezi amini ilipita kama dakika moja tu mama yake huyo rafiki yangu akaingia ndani.. niliogopa lakini hakuniona[emoji26][emoji26]

Akaanza kumfokea mwanae yani unajua mtoto alivyo na fujo halafu unamwacha tu njoo ona alichokifanya, na mimi nikajifanya nashangaa shangaa, mtoto alikua analia hatari.. nikazugazuga nikaaga kuondoka nikaacha wapo wanahangaika na mtoto..
Hili tukio nalijutia sana aisee Mungu tu anisamehe[emoji120][emoji2356][emoji2953]

Nadhani leo tuishie hapa wapendwa
Daah
 
Itakuwa hivyo ila jitahidi kuzuia hasira zako usijefanya kitu cha hatari zaidi kikakugharimu na kukufanya ujutie maisha yako yote.
Kumbuka hasira hasara ndio maana hatupaswi kufanya maamuzi tukiwa hatupo katika hali yetu ya kawaida.
Nimeumia
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]bora umewaza kwa sauti,hasa hii ya pili nimeshindwa kuamini kama ni kwel
Sema ndio hivyo ni utani ndio maana ipo chit chat.
Ukishindwa kujicontrol hasira zako ni hatari mno, unaweza fanya jambo kwa shinikizo la hasira likakudhuru hata wewe mwenyewe.
 
Back
Top Bottom