Niandae bajeti ya mafuta kiasi gani kwenda Singida?

Kutembea RPM ndogo kwa Speed kubwa inawezekana kabisa, kikubwa kabisa inachangiwa sana na Aina ya gear box. Kama una 4 Speed Automatic kama iliyo kwenye Harrier tako nyani sio rahisi Utembee speed kubwa bila RPM kupanda juu. Ila kama una Six speed Automatic kama iliyo kwenye Mark X GRS 180 au una Seven Speed CVT kama iliyo kwenye Van guard na Rav 4 Miss Tz kufuta kisahani ukiwa kwenye RPM ya kati 3,000 na 4,000 ni kawaida sana. Tena hasa kama Barabara kwa wakati huo haina mpando au kuna ka mteremko.NB hayo ni magari ya Mfano tuu sababu kila mtu anayajua. RPM haihusiki sana Injini bali inahusika sana na gear box. Ndio maana Harrier Tako nyani nyingi zina Injini ya 2AZ na Van guard Nyingi pia zina 2AZ lakini Harrier ina gear box ya gia 4 na Van guard ina Gia box ya Gia 7. Hawa watu wawili wakisafiri kwa speed sawa labda constant 140km/hr mwenye Van gaurd atakuwa na RPM ya Chini kuliko Harrier sababu ya Gear box.
 
bora umeleta evidence kabisa..kuna watu bila hii picha wangeendelea kubisha tu
Kitu kama hukijui au hujawahi kukiona haimanishi kuwa hakipo, kujifunza si jambo la siku moja... tupo pamoja mkuu Genius
 
Kama gari yako inakula vizuri Full tank inatakiwa ufike singida mjini
 
Naomba somo, mnaendeshaje 150/160kph Kwa rpm 2000, gear za chini nazo hamvuki 2000rpm mpaka mnafika hio 160kph?
 
Naomba somo, mnaendeshaje 150/160kph Kwa rpm 2000, gear za chini nazo hamvuki 2000rpm mpaka mnafika hio 160kph?
Kwasababu naendesha sana gari zenye gear nyingi, nikiamua rpm isivukw 2000 tangu mwanzo gari itafika 70kph wakati imemaliza gear zote,hence good fuel economy kwa mjini
 
mkuu k
mkuu kwa uzoefu wako,ni yapi mazuri na mabaya,na vitu vya kuwa makini,na service muhimu kwa gari ya engine ya 3S?,yangu naona kila baada ya km 50 oil inapungua kidogo,yangu ina jumla ya km 227000,ni noah old model,ulaji wa mafuta ni km ngapi kwa lita?msaada mkuu,gear ni automatic.
 
Jee gari ina leakage yoyote ya oil?
Unatumia aina gani ya oil kwa hiyo gari yako?
Kwa hizo kilomita jitahidi ubadilishe timing belt mapema sana usiache.

Na mars nyingi hizi automatic watu hawafati jinsi inavyotakiwa kuendesha na hivyo ubadilishaji wa gia unaenda kwa kuchelewa, endesha kwa kunyaga mafuta taratibu kama hautaki vile na utakuwa unapata mabadiliko ya gia kwenye revo counter 1300 _1400.
Kwa safari za nje ya mji kama gari iko sawa inaenda 1 ltr kwa 12_14 ila kwa mimi manual ndio niliweza kupata ratio ya 1 ltr kwa 14 kwa auto itashuka kwenye 11_12, zaidi zingatia unapoanza kuondoka fata utaratibu huo, pia weka plug za sindano ila upate original.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…