Niandae bajeti ya mafuta kiasi gani kwenda Singida?

Niandae bajeti ya mafuta kiasi gani kwenda Singida?

Kutembea RPM ndogo kwa Speed kubwa inawezekana kabisa, kikubwa kabisa inachangiwa sana na Aina ya gear box. Kama una 4 Speed Automatic kama iliyo kwenye Harrier tako nyani sio rahisi Utembee speed kubwa bila RPM kupanda juu. Ila kama una Six speed Automatic kama iliyo kwenye Mark X GRS 180 au una Seven Speed CVT kama iliyo kwenye Van guard na Rav 4 Miss Tz kufuta kisahani ukiwa kwenye RPM ya kati 3,000 na 4,000 ni kawaida sana. Tena hasa kama Barabara kwa wakati huo haina mpando au kuna ka mteremko.NB hayo ni magari ya Mfano tuu sababu kila mtu anayajua. RPM haihusiki sana Injini bali inahusika sana na gear box. Ndio maana Harrier Tako nyani nyingi zina Injini ya 2AZ na Van guard Nyingi pia zina 2AZ lakini Harrier ina gear box ya gia 4 na Van guard ina Gia box ya Gia 7. Hawa watu wawili wakisafiri kwa speed sawa labda constant 140km/hr mwenye Van gaurd atakuwa na RPM ya Chini kuliko Harrier sababu ya Gear box.
Screenshot_20220906_053517_com.android.gallery3d.jpg
 
bora umeleta evidence kabisa..kuna watu bila hii picha wangeendelea kubisha tu
Kitu kama hukijui au hujawahi kukiona haimanishi kuwa hakipo, kujifunza si jambo la siku moja... tupo pamoja mkuu Genius
 
Wakuu mambo vipi?
Mapema mwezi October nina ndugu yangu wa karibu anaoa huko Singida maeneo ya Itigi.

Ninapaswa kuhudhuria hiyo harusi sasa nauliza kwa wazoefu kutoka Dar mpaka Singida hapo Itigi niandae bajeti ya mafuta kiasi gani?

Gari ni Toyota Mark II grande engine beams 2000, cc 1990 au 2ltrs wanasema wengine.

Nasubiri maoni yenu wadau.
Kama gari yako inakula vizuri Full tank inatakiwa ufike singida mjini
 
Naomba somo, mnaendeshaje 150/160kph Kwa rpm 2000, gear za chini nazo hamvuki 2000rpm mpaka mnafika hio 160kph?
 
Naomba somo, mnaendeshaje 150/160kph Kwa rpm 2000, gear za chini nazo hamvuki 2000rpm mpaka mnafika hio 160kph?
Kwasababu naendesha sana gari zenye gear nyingi, nikiamua rpm isivukw 2000 tangu mwanzo gari itafika 70kph wakati imemaliza gear zote,hence good fuel economy kwa mjini
 
Hakikisha tu unafanya service, itapunguza sana fuel consumption, two, hakikisha uendeshaji wako ni mzuri, ukiweza kuchezea kwenye RPM ya 2-3.5 utasevu pakubwa saaaana, Mafuta ya 450,000 Hadi 550,000 "yanaweza" kuwatosha. Hakikisha unajaza full tank, usijaze Robo robo pia usijaze kwenye vituo vya kihuni.

Last month nilitoka Dar, nikaenda Kwa Msisi (Mkata-Tanga) then nikaendelea na safari ya Dodoma nikaenda Matumbulu, nikaenda Manyoni Hadi Itigi.

Niliondoka saa tisa usiku Dar, nikajaza Mafuta ya 220,000 pale Mlimani city, nikaenda safari zangu, nikaja kujaza Mafuta ya 40,000 Ihumwa wakati naingia Dodoma, Kesho nikaenda Matumbulu (25km) Kutoka Dodoma mjini Ile Iringa road then mchana nikaendelea na safari nikajaza pale Total kule four ways ya 50,000 nilipofika Manyoni nikajaza ya 50,000. Nikafika Itigi nikiwa na robo tank juu kidoogo Karibu na half.

Kwa wewe unayeenda Moja kwa Moja nadhani hata 250,000 Inawezekana ikakufikisha depending na aina Yako ya uendeshaji

Nilihakikisha sizidi 4rpm kwahio karibia 90% ya safari nilikua Chini ya hapo, sikua na ligi na mtu barabarani.
Gari ilikua ni BMW salon.
mkuu k
Kwa hesabu za kilomita za Dar to Itigi ni 605 hivi na kwa kadirio la ulaji wa gari yako kama 1ltr inafika km 9 basi hapo unaweza kutumia ltr kama 67x2= 134 go & return na mizunguko ya huko ukiweka ltr10 =144 kwa hiyo hapo ukiweka 150 unakuwa na amani kabisa na kama alivyokushauri Elli hapo juu usikimbie saana cheza na RPM 2.5 /3.5utakuja kutushukuru hapa ikiwa gari yako iko sawa sawa plug na airclener iko kwenye hali nzuri.

Hilo kadirio la juu sana nililoweka hapo nilitembea na Premior old model yenye engine ya 3S dar to kahama ltr67.
mkuu kwa uzoefu wako,ni yapi mazuri na mabaya,na vitu vya kuwa makini,na service muhimu kwa gari ya engine ya 3S?,yangu naona kila baada ya km 50 oil inapungua kidogo,yangu ina jumla ya km 227000,ni noah old model,ulaji wa mafuta ni km ngapi kwa lita?msaada mkuu,gear ni automatic.
 
mkuu k

mkuu kwa uzoefu wako,ni yapi mazuri na mabaya,na vitu vya kuwa makini,na service muhimu kwa gari ya engine ya 3S?,yangu naona kila baada ya km 50 oil inapungua kidogo,yangu ina jumla ya km 227000,ni noah old model,ulaji wa mafuta ni km ngapi kwa lita?msaada mkuu,gear ni automatic.
Jee gari ina leakage yoyote ya oil?
Unatumia aina gani ya oil kwa hiyo gari yako?
Kwa hizo kilomita jitahidi ubadilishe timing belt mapema sana usiache.

Na mars nyingi hizi automatic watu hawafati jinsi inavyotakiwa kuendesha na hivyo ubadilishaji wa gia unaenda kwa kuchelewa, endesha kwa kunyaga mafuta taratibu kama hautaki vile na utakuwa unapata mabadiliko ya gia kwenye revo counter 1300 _1400.
Kwa safari za nje ya mji kama gari iko sawa inaenda 1 ltr kwa 12_14 ila kwa mimi manual ndio niliweza kupata ratio ya 1 ltr kwa 14 kwa auto itashuka kwenye 11_12, zaidi zingatia unapoanza kuondoka fata utaratibu huo, pia weka plug za sindano ila upate original.
mkuu k

mkuu kwa uzoefu wako,ni yapi mazuri na mabaya,na vitu vya kuwa makini,na service muhimu kwa gari ya engine ya 3S?,yangu naona kila baada ya km 50 oil inapungua kidogo,yangu ina jumla ya km 227000,ni noah old model,ulaji wa mafuta ni km ngapi kwa lita?msaada mkuu,gear ni automatic.
 
Back
Top Bottom