Boeing 747
JF-Expert Member
- Mar 30, 2018
- 3,515
- 9,415
Ndugu yangu hawa wamiliki wa magari ya toyota usitegemee wakupe sababu zaidi ya hizi..Mngesaidia zaidi kwa kutoa sababu kwa nini aende kwa gari hii na si ile... Ni jukwaa la wengi na elimu haina mwisho.
1..Watakuambia toyota ndiyo inauzika....sasa sina uhakika kama kila mtu ananunua gari ili auze.
2. .watakuambia toyota zina spea za bei rahisi, hapa huwa nashindwa kuelewa...kwa sababu kuna mtu akiambiwa spea inauzwa milioni 3 kwake si tatizo bora iweinapatikana.
Mtazamo wangu..
Magari mengi yanayoanzia model za mwaka 2005 kupanda juu, haijalishi kampuni mfano Toyota, Nissan, Subaru n.k....spea zake si bei rahisi na ni magari yenye teknolojia kubwa kwenye mifumo ya umeme.
Both Toyota crown na Nissan fuga are great sedans....Powerful, comfortable, luxury e.t.c.
Wadau mngemchambulia mtoa mada technical specifications za Nissan fuga na Toyota crown.
Mwisho wa siku achague mwenyewe kitu roho yake inapenda. Kuhusu kuuzika na spea za bei rahisi, ningeshauri tusimpandikizie mwenzetu mawazo ya kimasikini kwa sababu hatujajua kama ananunua ili auze.
Mwisho ikumbukwe hayo magari mawili hayana best resale value huku mtaani kwa sababu ya ukubwa wa engines zake.
Sent using Jamii Forums mobile app