Nichukue mkopo bank gani?

Nichukue mkopo bank gani?

Sio kweli, "mkopo ni kwa ajili ya kuendeleza biashara"
Unaweza ukaanza nao pia kama mtaji. Lakini sio kwa hizi biashara za kufikiria nusu saa na kwenda kufanya, hapa inahitaji wataalamu na mipango.Sio mipango ya kulala na kuamka nayo, hii tunaita business plan, ambayo imebeba kila kitu kuhusu hiyo biashara.
NB, kama biashara zetu hizi za kichwani. Kwa namna ulivyojieleza usichukue mkopo mkuu, ni mchezo wa hatari sana huo. uwezekano wa kushinda ni kama 10%.
Lakini sio kwamba haiwezekani.Ukichukua huwa inakuwa hivi, biashara haijakua benki wanataka rejesho la kwanza 😁, hapa ndipo njiapanda ya kupotea, Umepambana umejazilizia na mtaji, rejesho la pili hili hapa,umepigiwa simu unachelewesha rejesho, uanaanza kukopa tena ili ulipe mkopo😁, Mwisho wa siku bank inakudai kiasi na wadau wanakudai kiasi, Na kule biashara lazima iyumbe kwa kukosa usimamizi.
Sio kwamba tunakatishana tamaa, la hasha! tunajaribu kuambizana ukweli kwa mazingira yetu, uwezekano wa kuuziwa nyumba ni mkubwa kuliko kupata mtaji kupitia mkopo bila kujipanga.
Tafuta namna, ukishatengeneza msingi wa biashara, chukua mkopo kutegemeana na mtaji ulionao.
 
Mi nafikiri asset ndio mtaji wako uza nyumba au pangisha nyumba mwenyewe usiwape benk nyumba yako take that risk Kama unasehem ya kuiweka familia yako pangisha nyumba kwa mwaka mmoja na upewe cash miezi 10 au mwaka
 
Usikatishwe tamaa. Kopa benki kulingana na uhitaji wako. Zingatia haya

1. Kila mia inayoingia uitunze.
2. Matumizi mengine yote yasitoke kwenye biashara yako.
3. Kopa fedha kidogo hata kama unauwezo wa kupewa nyingi. Hii itasaidia hata ukikwama kurejesha unaweza kwenda kwa jirani au ndugu akakudhamini hiyo hela.

4. Kama biashara yako ni ya bidhaa za hapo ulipo, nenda kwa anayeuza jumlajumla umweleze nia yako anaweza kukupa bidhaa ukawa unauza na kurejesha kwa kadri mtakavyokubaliana kwa udhamini wa nyumba badala ya kwenda benki. Uaminifu unatakiwa.
NB: Hakikisha eneo la biashara ni salama kwa wezi, majambazi na vibaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu wakuu.

Nina idea ya biashara ila nina changamoto ya mtaji, hivyo nimeshawishika kuingia bank kupata mkopo kwa dhamana ya nyumba yangu.. swali ni, je?

Bank gani itakuwa option bora zaidi kwa maana ya unafuu wa masharti, udogo wa riba na uharaka wa kupata mkopo wenyewe.

Natanguliza shukrani zangu
sio vizuri kukopa mtaji, hua tunakopa ku ku scale-up business ila sio kuanziaa new business aisee maybe if it’s >90% chance of success or ulishaifanya and uka close unataka ku resume.

Business requires skills like other professions out there. You’ll be having some lows and highs in your journey and that will give you some new challenges which you didn’t anticipate, you’ll be depressed due to loan pressure.

Business is strategies, start with your small capital, if it shows some kind of growth, seek loan, and it grows even bigger eventually.
 
Habari zenu wakuu.

Nina idea ya biashara ila nina changamoto ya mtaji, hivyo nimeshawishika kuingia bank kupata mkopo kwa dhamana ya nyumba yangu.. swali ni, je?

Bank gani itakuwa option bora zaidi kwa maana ya unafuu wa masharti, udogo wa riba na uharaka wa kupata mkopo wenyewe.

Natanguliza shukrani zangu
ACHANA NA MAMBO YA BENKI,HEBU SEMA UNATAKA SHI NGAPI NA UTAZIRUDISHA LINI?
 
Huwezi pata kirahisi bila biashara, maybe uongee na mtu mwenye biashara myajenge ukope kupitia leseni yake (kama mnaaminiana
 
ACHANA NA MAMBO YA BENKI,HEBU SEMA UNATAKA SHI NGAPI NA UTAZIRUDISHA LINI?
Aiseee
Screenshot_20230717-203233.jpg
 
Bank ni nyingi tembelea moja moja usikie vigezo na masharti yao then utaamua baada ya hapo.
 
Back
Top Bottom