Sio kweli, "mkopo ni kwa ajili ya kuendeleza biashara"
Unaweza ukaanza nao pia kama mtaji. Lakini sio kwa hizi biashara za kufikiria nusu saa na kwenda kufanya, hapa inahitaji wataalamu na mipango.Sio mipango ya kulala na kuamka nayo, hii tunaita business plan, ambayo imebeba kila kitu kuhusu hiyo biashara.
NB, kama biashara zetu hizi za kichwani. Kwa namna ulivyojieleza usichukue mkopo mkuu, ni mchezo wa hatari sana huo. uwezekano wa kushinda ni kama 10%.
Lakini sio kwamba haiwezekani.Ukichukua huwa inakuwa hivi, biashara haijakua benki wanataka rejesho la kwanza 😁, hapa ndipo njiapanda ya kupotea, Umepambana umejazilizia na mtaji, rejesho la pili hili hapa,umepigiwa simu unachelewesha rejesho, uanaanza kukopa tena ili ulipe mkopo😁, Mwisho wa siku bank inakudai kiasi na wadau wanakudai kiasi, Na kule biashara lazima iyumbe kwa kukosa usimamizi.
Sio kwamba tunakatishana tamaa, la hasha! tunajaribu kuambizana ukweli kwa mazingira yetu, uwezekano wa kuuziwa nyumba ni mkubwa kuliko kupata mtaji kupitia mkopo bila kujipanga.
Tafuta namna, ukishatengeneza msingi wa biashara, chukua mkopo kutegemeana na mtaji ulionao.